Wakati Freeman Aikaeli Mbowe anachukua nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Taifa kutoka kwa mzee Bob Nyanga Makani, alikuta kuna Wabunge wa 5 na Madiwani wasiozidi 75 nchi nzima. Wabunge wasioweza hata kujaza sebule yenu hapo.
Leo tukielekea kwenye uchaguzi mkuu mwingine wa ndani wa CHADEMA, Mwezi Desemba, 2019 CHADEMA kuna Wabunge zaidi ya 65 madiwani zadi ya 1500 nchi yote, halmashauri za kutosha na wanaunda kambi ya upinzani bungeni (KUB)
Hivyo ni vyema wewe "kijana - baro baro" wa leo mwenye kuendeshwa na "mihemko" kutambua haya mafaniko makubwa kabla ya kusema "Mbowe ameiua CHADEMA", inawezekana hujui hata CHADEMA imefikaje hapa ilipo leo, sio miujiza, ni STRATEGIES!
Kuna Vijana wa leo, labda kwa mihemko na juhudi za kutumika hawajui nguvu iliyotumika, jasho lililomwagika hadi kuifanya leo CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani. Wanadhani ni kitu rahisi kama kucheza 'BIKO na TATU MZUKA'
Hatusemi kwamba Freeman Mbowe ni malaika, kwamba hakuna dosari na makosa kwenye uongozi wake, hapana, isipokuwa jasho, damu na machozi yake yamemwagika kwa ajili ya CHADEMA, tuhuma zenu zinapaswa kuwa 'Valid' wakati wa kumkosoa, tuhuma za JINAI zithibitishwe!
Freeman Aikaeli Mbowe ni mwenyekiti halali wa CHADEMA, na ataondoka madarakani siku wanachama wa CHADEMA wakisema "imetosha" kupitia mkutano mkuu, sio kwa sababu "Kuna kelele za CCM na mapandikizi" huko nje za "Mbowe ondoka! Mbowe ondoka!"
Mzee Bob Makani alikuwa na kadi namba Tatu ya CHADEMA, kadi namba Mbili ilikuwa ya Mzee Brown Ngilulupi na kadi namba moja ya Mzee Edwin Mtei, hawakukosea kamwe kumuona Freeman Mbowe na kumkabidhi CHADEMA ambayo ameifanya kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania.
Mwisho, kimsingi, CHADEMA imebarikiwa kuwa na mwenyekiti kama Freeman Mbowe, wengine tuliopata fursa ya kufanya nae kazi au kukutana nae, tunajivunia sana, he's a man and a-half!
Stay blessed Chairman!
Mbowe Tano Tena Uchaguzi Mkuu 2019
Tatizo ni nini??Kila kwenye neno chadema weka..Tanzania
kila kwenye neno mbowe weka CCM
wachawi ni sisi
1. Mkuu katiba mpya inavyoandikwa ni kusaka maoni upya kabisa, mnakuja na framework mpya kabisa hivyo huwa vipengele vingi sana vipya vinakuja na vingi vya zamani kuondoka. Yaani mfano katiba ya warioba ilikuja na vitu vipya kabisa mfano muundo wa serikali tatu ambayo yalikuwa maaoni ya wananchi sasa kivipi mtu atokee aseme warioba alifuta serikali mbili??? Ilihali alianza kitu kipya kabisaa kwa maoni na mchakato na mfumo mpya. Kwahiyo ni kweli kipengele hicho hakipo kama ambavyo vipengele zaidi ya 100 havipo na vingine zaidi ya 100 vimeongezwa sasa sielewi kwanini hoja ijengewe kwenye kipengele cha ukomo tu na sio vingine?? Na hiyo kamati iliongozwa na Prof Baregu na katibu wake mnyika sasa kivipi tena atajwe mbowe ambaye alikua hana mizizi CHADEMA enzi hizo??
2. Sahivi wanatumia katiba iliyoanza 2006 ambayo haina kipengele cha ukomo cha nafasi ya uenyekiti sababu haikuwemo kwenye maoni ya wanachama kwenye kuandika katiba mpya.
3. Jaman ukomo upo ni kila baada ya miaka mitano uenyekiti unaisha na lazima uchaguzi ufanyike ili uweze kuwa mwenyekiti, tofauti tu ni kwamba Kutokuwepo ukomo wa mihula haimaanishi utawale milele bila iliwekwa ili kutoa fursa ikitokea mtu bado anauwezo kuendelea kuongoza basi anaweza chaguliwa na wanachama kuendelea kuongoza kwa kipindi kingine.
Mbowe kwa minajili hiyo ukomo wa uenyekiti ni mwaka huu na kama atataka kuwa mwenyekiti tena ni lazima wanachama wakubali,wampitishe na agombee na ashinde uchaguzi ambapo ndio demokrasia inapofuatwa hapo na inapopimwa.
Kasome misingi 11 ya demokrasia uone kama ukomo ni mmojawapo alafu urudi hapa kuujengea hoja. Ila CCM wao wana ''ukomo'' wa uenyekiti kila miaka 10 ila je umewahi ona uchaguzi wa mwenyekiti unafanyika kwa watu kuchukua fomu na kugombea?? Je hapo kuna demokrasia licha ya kuwa kuna "ukomo" wa mihula ya kuwa mwenyekiti wao??
Ni hayo tu
Huko kupisha ndiyo kukoje?
allantence kwa mfano ile Katiba Pendekezwa iliyopitishwa na Bunge la Katiba ingepigiwa kura ya Maoni na kuwa Katiba yetu Rasmi, Jee ungeendelea kunukuu vipengele vilivyokuwa kwenye Katiba iliyotungwa mwaka 1977?
Basi katiba ya CHADEMA inayotumika sasa ni ile ya Mwaka 2006 Iliyopitishwa pale kwenye ukumbi wa PTA. Kwenye Katiba hiyo hakuna ukomo wa muda wa Uongozi wa vipindi viwili vya miaka mitano mitano!!Hapana nisingenukuu .
Kwa nini hakuna Demokrasia!?Kwa style hii ndo mnataka kutuaminisha kuwa mnademokrasia.....hahahahahah
Basi katiba ya CHADEMA inayotumika sasa ni ile ya Mwaka 2006 Iliyopitishwa pale kwenye ukumbi wa PTA. Kwenye Katiba hiyo hakuna ukomo wa muda wa Uongozi wa vipindi viwili vya miaka mitano mitano!!
Maneno haya akiambiwa jamaa yenu huwa mnasema ametukanwa!?Mbowe apumzike, uwezo wake wa uongozi umefikia kikomo
Indeed , astaafu sasa aachie damu changa ipambane aisee.Mbowe apumzike, uwezo wake wa uongozi umefikia kikomo
Unajua Trump ama miaka mingapi na mpinzani wake toka Democrat Bwana Joe Biden ana miaka mingapi? Trump ana miaka 73 na Joe Biden 76.Indeed , astaafu sasa aachie damu changa ipambane aisee.
Kwa mtazamo wako wewe unadhan Mbowe anastahili tena kugombea baada ya mafanikio aliyoipa CHADEMA ?allantence kwanza elewa mifumo ya uandishi wa Katiba. Alichosema zitto junior ni kwamba katiba iliyoletwa kwa wanachama ni toleo jipya lililoacha mambo mengi na kuingiza mambo mengi na siyo kipengele kimoja pekee kilichoachwa.
Ujerumani hawana ukomo wa muda wa Kansela kukaa madarakani lakini Marekani wanacho. Maa yake ni kwamba ukomo wa uongozi huwa una sababu zake.
Mwalimu Nyerere yeye alikaa Ikulu miaka 23 lakini alipotoka aliacha Katiba yenye ukomo wa Muda wa vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Hoja yake ndiyo hoja ya watu wengi Afrika, kwamba watawala wa Afrika huwa hawaachii dola kirahisi kwa hiyari yao.
Kwenye CHADEMA siyo kwamba Uchaguzi haufanyiki ama wengine huzuiwa kugombea, bali Mbowe huwashinda anaoshindana nao. Hiyo ni Demokrasia na kama wengine wengekuwa wanazuiwa kugombea ili agombee Mbowe peke yake hapo ndipo ingekuwa kosa.
Miaka 3 iliyopita watu waliokwenda kumshawishi Lissu agombee uenyekiti kwa hoja ya Mbowe kukaa muda mrefu madarakani walishangazwa na majibu ya LIssu. Lissu aliwaambia kuelekea 2020 CHADEMA inamhitaji Mbowe kuliko wakati mwingine wowote ule.
Kuongoza nchi na chama ni vitu viwili tofauti. Kuna wana CCM eti wanasema kama Mbowe ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA basi na Magufuli naye aendelee kuwa madarakani mpaka achoke.
Suala hapa si kukaa madarakani bali hayo madaraka yanapatikanaje??
Haijalishi lakini mwenyekiti kafanya mengi kwa chama , ametumikia na kupambana vyema kuiweka taasisi imara , sasa ni muda umefika kumpa kijiti mwingine .Unajua Trump ama miaka mingapi na mpinzani wake toka Democrat Bwana Joe Biden ana miaka mingapi? Trump ana miaka 73 na Joe Biden 76.
Hapa ndipo hoja ya wana CCM inapofia. Kugombea ni utashi wa mtu. Kama wana CHADEMA wengine watajitokeza watapimwa na wenzao lakini haiwezekani kuokoteza watu ili mradi ionekane kwamba eti CHADEMA imebadilisha Mwenyekiti wake wa Taifa ili kuwafurahisha CCM.Unadhan kuwa hakuna mwenye uwezo mwingne zaidi ya mwenyekiti kuitoa CHADEMA hapa ilipo sasa na kuipeleka sehemu nyingine?
Ni kweli kabisa kwamba Demokrasia ni maamuzi ya watu na miongoni mwa maamuzi hayo ni utunzi wa Katiba. Katiba haidondoki toka mbinguni bali hutungwa na watu kwa kuangalia matakwa yao na ya vizazi vijavyo.Basi hata mkulu wa nchi ngoja atawale mbaka wananchi tuseme basi
CHADEMA itaishi kwa falsafa zake , na zinafahamika, hivi samahani kidogo tume ya uchaguzi wa chama inateuliwa na Nani? Walioteuliwa na Nani?Hapa ndipo hoja ya wana CCM inapofia. Kugombea ni utashi wa mtu. Kama wana CHADEMA wengine watajitokeza watapimwa na wenzao lakini haiwezekani kuokoteza watu ili mradi ionekane kwamba eti CHADEMA imebadilisha Mwenyekiti wake wa Taifa ili kuwafurahisha CCM.
Hivi CCM imewahi kuhoji ni kwa nini hakuna ukomo wa muda wa mtu kuwa Mbunge!!??
Kwanza kwenye CHADEMA huwa hakuna mgombea mmoja. Kwa ivo watakaochukua fomu mwisho wa siku hushindanishwa.Nakuuliza hayo kwa sababu kama atateua na anamkono itakuwa maajabu apitishwe mgombea ambae anagombea na mteuaji.