Hatimaye wafanyakazi wa Dezo Civil Contractors Ltd wakombolewa

mkadiriajimajenzi

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
549
613
Baada ya kuvumilia kwa muda mrefu manyanyaso, dharau, ubaguzi, ukiuwaji wa haki za ajira na dhuluma walizokua wakipata kutoka kwa wahindi ambao ni wamiliki wa kampuni ya ujenzi inayojulikana kwa jina la Dezo Civil Contractors Ltd na yenye ofisi zake jijini Dar es salaam, Leo imekua siku nzuri kwao baada ya Naibu waziri wa kazi na ajira kufika katika ofisi hizo baada ya kupigiwa simu na baadhi ya wafanyakazi walioamua kufanya mgomo ili kuishinikiza kampuni hiyo iwatekelezee haki zao kama wafanyakazi.

Baada ya kuwasili katika ofisi hizo wahindi walikimbia huku na kule pamoja na baadhi ya ya watanzania wawili ambao walikua ni wasaliti, baada ya purukushani za hapa na pale wafanyakazi hao walianza kumueleza naibu waziri kuhusu madai yao ambapo walilalamikia kuhusu mishahara midogo isiyokidhi wanayolipwa, kufanya kazi bila mikataba, kufanya kazi mpaka siku za sikukuu bila kulipwa, kufukuzwa kazi ghafla bila notice n.k ndipo Naibu waziri akaamuru kuitwa mkurugenzi wa kampuni hiyo ambaye alikuwa akitetemeka kama mtu aliyenyeshewa na mvua...

Baada ya naibu waziri kumuuliza maswali aliyoshindwa kuyajibu aliamuru kwamba madai yote ya wafanyakazi yatatuliwe ndani ya siku saba.

Habari kamili tazama Itv leo usiku

1457367698425.jpg
1457367713905.jpg
 
Dah huyo yanki mbona anakodolea macho hayo maziwa.

Dezo kweli
 
Unadai hela huku kampuni inaitwa DEZO?

naibu waziri wa afya anahusika na malalamiko ya wafanyakazi?
 
Back
Top Bottom