kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,190
- 24,620
Donald Trump akiri kuchukiwa sana duniani, Obama akosoa siasa zake
Rais Donald Trump wa Marekani amekiri kwamba hatua yake ya kutekeleza siasa dhidi ya uhamiaji, zimemfanya achukiwe sana duniani.
Trump ameyasema hayo akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi katika mji wa Houston ndani ya jimbo la Texas wakati akitetea siasa zake dhidi ya uhajiri ambazo zimesababisha ukosefu wa ajira na usalama nchini Marekani. Trump ambaye siasa zake dhidi ya uhajiri nchini Marekani zimekabiliwa na ukosoaji mkubwa na kupingwa kwa kiasi kikubwa kimataifa, amedai kwamba juhudi zake zimekuwa na taathira chanya kwa uchumi na usalama wa Marekani. Hii ni katika hali ambayo matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni nchini humo yanaonyesha kwamba, kiwango cha kutokuwa radhi Wamarekani na siasa za Trump kimezidi kuongezeka. Uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na kanali ya televisheni ya CNN, unaonyesha kwamba, asilimia 58 ya Wamarekani hawafurahishwi na utendajikazi wa rais huyo nchini Marekani.
Wakati huo huo Barack Obama, Rais wa zamani wa Marekani amekosoa siasa za serikali ya Trump kwamba hazizingatii maisha ya watu masikini nchini humo. Obama ameyasema hayo katika mkutano wa kampeni za uchaguzi kati ya wafuasi wa chama chake cha Democrat katika mji wa Las Vegas, jimbo la Nevada na kuwataka wanachama wa chama hicho kushiriki katika uchaguzi kwa kutumia busara ili kuirejesha Marekani kwenye siasa zake za huko nyuma. Obama ameongeza kwamba siasa za kodi za Trump zimewanufaisha tu matajiri na kuwafanya masikini kuishi katika hali ngumu zaidi.