Hatimaye Tanzania imeruhusu KQ kuingia nchini humo

Tony254

JF-Expert Member
May 11, 2017
16,017
16,427
Baada ya Watanzania kupiga domo jana kuwa Tanzania haitaruhusu KQ kuingia humo hadi mwakani, Tanzania imeshindwa kungoja hata wiki moja ili kufunza Kenya adabu kama mlivyokuwa mkisema.

Yaani hata masaa 24 hazijaisha kabla Kenya kuruhusu malazy kuingia huku, tayari TZ imeruhusu KQ kuingia. Hio haraka ni ya nini? Hii inaonyesha kuwa Tanzania ni nchi yenye utoto sana. Mnanuna kila wakati. Si mngengoja hata wiki moja ili sisi Wakenya tupate adabu kama mlivyosema? Kenya babu yenu.

=======

Tanzania lifts ban on Kenyan airlines

Kenyan carriers will resume flights with immediate effect after Tanzanian regulator lifts ban.

Kenyan airlines can now fly to Tanzania

File | Nation Media Group

Kenyan airlines have finally been allowed to land in Tanzania, bringing an end to the airspace feud between the two countries.

This is after the Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA) announced that it had lifted the suspension that hit Kenyan airlines.

In a statement, TCAA director general Hamza Johari said the authority was acting on reciprocal basis after its Kenyan counterpart, the Kenya Civil Aviation Authority (KCAA), included Tanzania on a revised list of countries exempted from the 14-day mandatory quarantine upon arrival.

“In view of that and on a reciprocal basis, Tanzania has now lifted the suspension for all Kenyan Operators namely, Kenya Airways, Fly 540 Limited, Safarilink Aviation and AirKenya Express Limited,” TCAA director general Hamza Johari said.

Mr Johari said Kenyan carriers can resume of flights immediately.

Last month, Tanzania nullified its approval for Kenya Airways to land in the country with effect from August 1, 2020 after Kenya excluded it from a list of about 111 countries whose passengers are allowed to enter its territory without being quarantined for 14 days.

A few days later, Tanzania banned three more Kenyan carriers - AirKenya Express, Fly540 and Safarilink Aviation - from flying into the country as it piled pressure on Kenya to ease its Covid-19 travel restrictions.

The tit-for-tat between the two countries was precipitated by different approaches that they have taken to tackle the Covid-19 pandemic.

While Kenya has ranked Tanzania on its red list, the latter has always maintained that it is Covid-19 free.
 
Dalili kwamba Tanzania hatuna nia mbaya wala ajenda ya siri kama mlivyoaminishwa kwamba Tanzania inalengo la kuvuruga uchumi wa Kenya.
 
Ukisikia nyuzi za kike ndio hizi umwamba ulifanywa na TANZANIA Kwa mara ya pili kuilazimisha Kenya ifuate matakwa ya TANZANIA kuanzia kule namanga mpaka hili la anga hulioni unachoona wewe eti TANZANIA umeshindwa hata kusubiri wiki wakati wenye mamlaka upande wa Tanzania walishasema siku nyingi hatutaruhusu ndege za Kenya mpaka pale watakapoiondoa tu TANZANIA kwenye orodha ya watu wake kuwekwa karantini tena walisema sio Kwa kuteta walisema waziwazi ,sasa leo mumefata masharti walioweka TCAA sasa wang'ang'anie nini tena ndo ujue serikali ya TANZANIA inajitambua inachosema ndio unachofanya huo ndio msimamo hakuna ubabaishaji hapa.
 
Wewe kweli bwege. Kama masharti ya Tz yametekelezwa unataka Nini Tena. This shows Kenyans that Tz had no problems with Kenyans. Mkimwaga sukumawiki sisi tunamwaga pilau, mkitenga pilau sisi tunatenga sukuma wiki. Hii ni sera ya jino kwa jino na mkono kwa mkono. Umeelewa?
 
Welcome back Jirani sasa uwe na akili kumkichwa sio kudeal na mambo kwa hisia, Sisi hatuna tatizo tunaweza kujifungia na maisha yakaenda ila nyinyi wa kenya hamuwezi kufanya ivo na siku zote mjue sisi ndo muamuzi mkuu wa huu ukanda na mnatuhitaji zaidi ya sisi tunavyowahitaji
 
Tushasema hatupimi, na caranteen hatukai na mmefuata tunachotaka tena mmeomba msamaha usiku na mchana na mmebembeleza kila wakati tumewaonea huruma msife njaa
mbn watz hampendi karantin! wakati wasafi wanaimba na kukata maunoo...karantiiiin!!😂
 
Dalili kwamba Tanzania hatuna nia mbaya wala ajenda ya siri kama mlivyoaminishwa kwamba Tanzania inalengo la kuvuruga uchumi wa Kenya.
Si mlisema kuwa mtatucharaza viboko. Mlisema kuwa mtatufunza adabu. Mlisema KQ haitatua Dar hadi tupige magoti. Sasa tena mnasongeza goli. Baba yenu ukanda huu anajulikana
 
Si mlisema kuwa mtatucharaza viboko. Mlisema kuwa mtatufunza adabu. Mlisema KQ haitatua Dar hadi tupige magoti. Sasa tena mnasongeza goli. Baba yenu ukanda huu anajulikana
Sisi wananchi wa kawaida tumechoshwa na tabia za viongozi wa Kenya, tungependa sana serikali yetu ingechelewa kuwaruhusu. Ilichofanya serikali yetu ni busara za kiuongozi na kuwaonyesha kwamba serikali ya Tanzania haina nia yoyote ile mbaya na Serikali ya Kenya.

Jambo na funzo ambalo limepatikana kutokana na mzozo huu ni kwamba, Tanzania hata siku moja haitoanzisha chokochoko na majirani wake, ila yeyote atakayeanzisha, tutajibu siku hiyohiyo.
 
Back
Top Bottom