Hatimaye Shamshi Vuai Nahodha Apata Nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye Shamshi Vuai Nahodha Apata Nyumba

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Salimia, Jul 3, 2011.

 1. S

  Salimia JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hatimaye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamshi Vuai Nahodha ambaye amekuwa akiishi hotelini kwa miezi nane sasa atahamia kwenye nyumba yake kuanzia wiki ijayo, NIPASHE Jumapili imebaini. Habari tulizo nazo ni kwamba nyumba hiyo ambayo ilielezwa kuwa haikidhi, hivi sasa imekamilika kwa kiwango alichokuwa anataka yeye mwenyewe. Awali, chanzo cha kuaminika kililiambia gazeti hili kwamba Nahodha alikataa kuhamia kwenye nyumba yake kwa maelezo kuwa haikuwa na hadhi ya Waziri Kiongozi mstaafu. Kutokana na hali hiyo, serikali ililazimika kutumia mamilioni ya shililingi, kumlipia Nahodha chumba katika hoteli ya New Afrika, jijini Dar es Salaam. Taarifa zilieleza kwamba Nahodha ameendelea kuishi hotelini kwa sababu nyumba haikuwa na samani za kutosha. Chanzo hicho kikalidokeza gazeti hili kwamba pamoja na mambo mengine, Nahodha alikosa nyumba ya serikali kwa kuwa aliyekuwa anashikilia wadhifa huo, Laurence Masha, alikuwa akiishi nyumbani kwake. Kutokana na hali hiyo, Wakala wa Ujenzi (TBA), ililazimika kumjengea Nahodha nyumba ambayo imekamilika lakini samani hazikutosheleza ukubwa wake. Nahodha ambaye anaishi hotelini tangu Novemba mwaka jana baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, inaelezwa kwamba ameshindwa kukaa kwenye nyumba za mawaziri wa kawaida kwa kuwa alihitaji nyumba kubwa inayoendana na hadhi ya Waziri Kiongozi mstaafu. Nahodha anaishi kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam, ambayo gharama ya chumba kwa siku ni kati ya dola za Marekani 140 na dola 160, kwa vyumba vyenye hadhi ya kawaida (standard) wakati vyumba vyenye hadhi ya juu (executive suite), ni dola za Marekani 280 kwa usiku mmoja. Imedaiwa kuwa kutokana na nyumba aliyojengewa kutokuwa na samani za kutosha, Nahodha alilazimika kukaa hotelini mpaka mahitaji ya nyumba hiyo yatakapokamilika. Msemaji wa Wizara hiyo, Isaac Nantanga, alipoulizwa na NIPASHE Jumapili ikiwa kuna uwezekano wa Nahodha kuhamia kwenye nyumba yake, alisema yupo nje ya ofisi na kwamba hana taarifa za kina kuhusiana na suala hilo. “Tuwasiliane Jumatatu ijayo ili niwe na taarifa za uhakika za kukupa…nipo nje ya ofisi kwa sasa,” alisema Nantanga. Hata hivyo, pamoja na kwamba Waziri Nahodha anahamia kwenye nyumba yake wiki ijayo, uchunguzi unaonyesha kwamba bado Mawaziri kadhaa wataendelea kuishi hotelini. Baadhi yao ni Naibu Waziri wa Maji, Gerson Lwenge anayeishi Abla Hotel apartments, zilizopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam. Uchunguzi wa gazeti hili umebaini pasi na shaka kwamba, Naibu Waziri huyo tangu ateuliwe kushika wadhifa huo hajapewa nyumba ya serikali. Kutokana na hali hiyo, kiongozi huyo anaishi Abla ambako analipiwa dola 3,000 (sawa na Sh. 4,800,000), kila mwezi kama gharama ya pango la nyumba. Utafiti umebaini kwamba Naibu Waziri huyo, ameishi Abla kwa takribani miezi mitano na hivyo amekwishatumia zaidi ya Sh. 60 milioni mpaka sasa. Kabla ya Abla, alikuwa anaishi kwenye moja ya hoteli ya kifahari jijini hapa. Kwa mujibu Abla, gharama za apartment kwa mwezi zinatofautiana kulingana na siku ambazo mpangaji ataishi. Inaelezwa kwamba ikiwa mgeni atakaa kwa siku moja ni dola za Marekani 250, kwa mwezi ni dola 3,000 wakati mgeni atakayeishi kwa miezi mitatu anapatiwa punguzo la dola 900 hivyo atalipa dola 8,100. CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kikwete hana huruma kabisa na nchni hii yani wakati watoto wanakufa mahospitalini bado wanaparuwa kidogo kilichopo kiasi hicho, hao watu wana umuhimu gani? hasinge wateuwa mpaka nyumba zipatikane maana wawepo wasiwepo ni sawa tu hamna tofauti yeyote.
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  DU aendelee tu kuishi hotelini kwani mi sioni faida yeyote au hasara yoyote akiiishi huko hotelini,kwani hyo hela itaingizwa kwenye account yangu? AENDELEE KUISHI TU HUKO HOTELINI NA MAWAZIRI WENGINE WAENDE TU HOTELINI WOTE 56 WAENDE TU WAKAISHI HOTELINI NDO SAFIII
   
 4. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwani yeye alikuwa ameteuwa kama waziri kiongozi?
  kama anajari hivyo cheo chake cha zamani imekuwaje kakubali kuwa waziri wa mambo ya ndani?
  huyu ni Jeuri, katili, mbinafsi , mwenye choyo na uchu wa madaraka naona jk hana kauli kwa mawaziri wake

  MASLAHI YA TAIFA KWANZA
   
 5. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Usomaji wangu wa hii thread umeathiriwa na avatar ya mleta mada. CCM ina vituo kama vya salimia waziri kupata nyumba mpaka.....


  Sasa huo new africa hivyo vyumba ni dnio ukubwa wake unaligana na hadhi ya waziri kiongozi mstaafu.


  hahhahaha Tanzania Ni comedy tosha . Na huko zanzibr uute bado ana nyumba ya serikali huku bara pia . haya .......  Inabidi tujue standards za nyumba za

  • Rais mstaafu
  • Wziri mkuu mstaafu
  • Jaji mkuu
   
 6. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu POSHO Kwa hili Rais ndiye mwenye matatizo! Hakupaswa kumteua Nahodha katika post yake ya sasa. Kwani hata kama MHA ni Wizara ya Muungano hakuona Mzanzibari anayefaa kwa post hiyo zaidi ya Nahodha? Tuoneane huruma jamani, hivi hayo ndiyo matumizi halali ya kodi zettu kweli?
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Avatar yako imenikwaza nimeshindwa kusoma!! byeeee
   
 8. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sana anapewa allawance zipi?
  ninaanza kuhisi kuna mchezo mchafu hapa.
  waziri kiongozi ana allowance zake za kudumu (maisha) ina maana bado wanampa?
  na kama wanampa hali yeye ni waziri wa mambo ya ndani hapo imekaa vipi?
  pesa ya ulinzi ya huyu waziri zinatoka serikali ipi, watumishi wa ndani na dereva?
  kama zinatoka serikali ya muungano tumeibiwa tunafanya majukumu ya serikali ya ZANZIBAR
  hapa kuna maelezo mengi yanatakiwa uteuzi wa NAHODHA ni skendo
   
 9. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tanganyika ije tu mapema
   
 10. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Tanzania inahitaji maombi. Nani ataongoza maombi haya sasa maana viongozi wa dini wengi wao wanalamba miguu ya wanasiasa na wengine wapo kibiashara zaidi
   
 11. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mbona umeandika kama umeshindwa kusoma
   
 12. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mtu yeyote anayeamini katika TAIFA KWANZA kama wewe ana maswali mengi ya kujiuliza kuhusu uteuzi huo. Huyo bwana atakuwa anagonga marupurupu yote ya U-Waziri Kiongozi Mstaafu (ukiacha monthly pension) kutoka SMZ, na analamba mishahara na marupurupu yote ya U-waziri wa Mambo ya Ndani kutoka SJMT. Anayeelewa zaidi atatueleza. Kilichosababisha uteuzi ni kuiepusha Zanzibar na msukosuko wa baada ya Uchaguzi, si unakumbuka mbio zake ziliishia Dodoma? Maslahi ya "Wananchi wanyonge wa Tanzania" hayakuzingatiwa katika uteuzi wake wa sasa. Pinda alipaswa aorodheshe uteuzi wa Nahodha kuwa miongoni mwa "Maamuzi magumu."
   
 13. f

  fazili JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,192
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180
  kama unamaanisha unayoongea wewe kweli akili yako mbovu na watu kama wewe ni janga la kitaifa!!!
   
 14. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MKUU
  nimekusoma na nimekupaliana na wewe walikuwa wanaziba pengo la mbio za DODOMA bila kujari maslahi ya taifa.
  husikute hata huyo raisi wa zainzibar anavuta zote kutoka huku na kule,

  ila hiyo RED umenivunja mbavu kweli kikwete amefanya maamuzi magumu mengi, hata ya kumpa rwekatare ubunge pia
  mama wa madili

  MASLAHI YA TAIFA KWANZA
   
 15. f

  fazili JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,192
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180
  Mpaka watanzania tutakapojifunza namna ya kuchagua viongozi wetu bila ushabiki wa kipumbavu ndipo tutaanza kuona nafuu. Lakini kama tunaendelea kuchagua watu wasiojali na kwa kuwaangalia nyuso zao tutaendelea kunyonywa mpaka damu yote iishe! Kwanini tusiamue kuchagua watu tunaojua kweli hawa wako aggressive na makini haya tuendelee kuangalia dini na makabila huku tukishuhudia wadini wenzetu na wanakabila wenzetu wakiungana na wengine kututoa kafara bila huruma! Fungukeni enyi watanzania, la sivyo mtakwisha!!!!
   
 16. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wananchi hawajawahi kuchagua mtu .
  chaguzi zinachakachuliwa ni bora kupigana sasa kupata mfumo bora wa uchaguzi na tume huru
   
 17. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha haaaaa...!!!!Mkuu, inabidi tucheke kwa uchungu tu, hii nchi hovyo kabisa!Tuendelee kuchangia hoja nyingine Mkuu.
   
 18. S

  Salimia JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kaka umeathirika kwa vipi?
   
 19. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  **** hii unadhani mchezo
  anyway wacha hiyo watu watatoka kweye mada
   
 20. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kikwete anabana matumizi kwa kununua bajaj kwa wajawazito huku mamilioni yakiishia kwenye mambo ya hovyo
   
Loading...