Hatimaye Rais Barrow arejea nchini Gambia

Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,946
3,685
Rais Mteule wa Gambia Bw.Adama Barrow leo anarejea Nchini Gambia baada ya kuridhishwa na hali ya Usalama nchini humo.

Barrow ambaye aliapishwa kwenye ofisi za ubalozi nchini senegal ameapa kupambana na ufisadi wowote uliotendwa na mtu yeyote hata kama ni Rais mstaafu Yahya Jammey aliekimbilia uhamishoni Guinea Bissau.Bw.Yammey inasemekana ameiba zaidi ya Dola Bilioni 12 za Marekani kutoka Hazina ya Serikali.

Jumuia ya Ushirikiano ya Afrika Magharibi(ECOWAS) imesema haijaongelea swala la kinga ya kutoshtakiwa ya Jammey hivyo anaweza kushtakiwa kwa madhila na ufisadi wowote alioufanya Gambia.

Nae Makamu wa Rais mteule Bi.Fortunatha Mtambajani ameomba jumuia za Mataifa kuzirudisha mali zote anazomiliki Barrow.

Leo Sherehe za kumkaribisha Barrow zitafanyika katika uwanja wa Uhuru mjini Banjul.
 
Kuzirudisha Mali anazomiliki Barrow? Rekebisha hapo.Mali zote anazomiliki Jammeh
 
Sasa utashangaa hao nao badala ya kuwaza namna ya kuboresha maisha ya watu wata anza kushughulika na Rais aliye pita, bas ndio miaka mitano itapotelea humo humo.
Viongozi wa Afrika bhana
 
hapo kwenye dola bilion 12.....hapana nadhani ni dola mil 12. nchi ndogo km gambia haiwezi kuwa na reserve ya dola bil 12 hazina.
 
Back
Top Bottom