Hatimaye posho mpya za wabunge zafutwa rasmi

Itakuwaje kwa wale wabunge tulioambiwa wameshaanza kuzichukuwa? Je watarudisha?
 
Inawezekana Mkuu watu wanapima upepo wanaweza kuirudisha kimya kimya!!!!!


Mkuu hii ngoma itachezwa kimyakimya.Wakati JK anaingia madarakani ilikuwa hivihivi,watu wakapiga makelele kuipinga hadi Rais wakati anaongea na wazee wa Dar akijidai kusema eti wabunge ni watu wazima na wamesikia,,,,,kilichofuata Mzee wa mikakati Samwel Sita akasubiri upepo utulie akaicheza kimyakimya.
 

Jamani eeh, someni vizuri hapo kwenye red. Suala hapa ni Rais bado hajatoa kibali, ila anaweza kutoa kibali kwa muda wake mwenyewe kwakuwa suala bado liko mezani kwake halijaondolewa, nani anasema zimefutwa? Hivi anayezifuta posho hizo ni yule aliyeziomba (kwa kuwithdraw maombi yake) au yule aliyepelekewa kuidhinisha? Mimi naona hii ni sanaa tu!
 

Nadhani kwa sasa suala si kufuta posho...HAPA CHA KUJUA NI KWA NINI VIONGOZI WA SERIKALI HAWAELEWANI KIKAULIIII???
 
Hurreeeeeeeiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…