Hujanikwaza Yummy ucjali.
Mwanangu ana miaka miaka mitatu. Kwakweli sijaingia kwenye mahusiano na sipo tayari kwa sasa, nimeomba mawazo yenu kwani mi naona hii situation imekaa strange kidogo kwangu.kwanza ni rafiki ambaye sijawahi kumuwazia hayo mambo, pili ni mdogo kwangu tatu yeye mawazo yake yako mbaali kwenye ndo nikimjibu vinginevyo baasi nimenuniwa for that day.
Asante kwa ushauri ila hata iweje na Mungu aniepushie siwezi kumrudia jamani duuh huwezi jua what i went through. for now nina concentrate na maisha yangu na mwanangu tu.
Vip na wewe huna hata chembe chembe ya upendo kwake??????
what if akibadirika na ukaona kabisa kabadirika, kuna tatizo gani la kurudiana nae mzazi mwenzako? Au usikute kijana rafiki yako alitia sumu kali hadi huwezi kusamahe. Ni vizuri sana kukaa na baba wa mtoto wako.. huwezi jua huyu jamaa atakuja kukaa vipi na mwanao.. sasa hivi anaweza ku act akitaka tunda, akikutia mikononi ndo utajua haswa yuko vipi.Tumia muda huu kumsoma na uwe makini sana.Mimi mwanaume najua tunapotaka kuua tuna fanya nini.. we can do anything... na kwa wewe sasa hivi uko vulnerable kwani umetoka kwenye maumivu moyo wako unahitaji pumziko, na pia mwili wako soon utahitaji kupozwa kama bado.
Pole dada kwa yaliyokukuta na hongera kwa kuepusha msongamano na kuamua kujiweka pembeni. Huyo side B naomba muendelee kuwa marafiki tu, hata kama yeye anazungumzia masuala ya ndoa, wewe ni mwanamke bado unaweza kumpa majibu mazuri tu amabyo hayatamkwaza. Naungana na member wengine wote waliosema utulie kwanza, jipe muda atleast hata mwaka hivi ndo uanze kuangalia masuala ya mahusiano tena, sawa mwanangu? (Mwanangu coz unajina kama la mwanangu) Mungu akutangulie ma babygirl
kubadilika kwake kunahitaji maombi aisee maana mh iko kwenye damu.akibadilika niko tayari kumrudia
nini nini hicho kilico kwenye damu, noella weka wazi hapa kuna watu wengi engine wamewahi kuwa na issue kama yako na wameweza kutatua, sidhani kama kuna tatizo ambalo ni wewe wakwanza kulipata.. na hamna anayekujua weka wazi feel free.
kwanza kabisa hatukuwa tumeoana, tulizaa na kila mmoja aliishi kivyake, kila siku ni ahadi tuu mwakani mwakani nikiaccomplish hiki nikiaccomplish kile.tatizo ni kwamba yeye ni mtu wa kugomba tuu for no good reason,hata ufanye nini kizuri ye anagomba, ni mtu anagombana mpaka na ndugu zake na anaweza asiongee nao hata mwaka mzima, ni mtu anaweka kinyongo for years, ni mtu muongo anapenda kuishi maisha artificial na kudanganya marafiki sometimes hata ndugu so siku akisahau kuniambia ni kwamba ninapata aibu kwa maana nitasema vinginevyo.ni mtu wa kusikiliza maneno ya kijiweni then ana apply kwangu, kwa mfano alianzisha tabia ya kunipiga then baadae akaconfess kwamba alisikiliza maneno ya kijiweni wakisema mwanamke usipompiga hatokuheshimu.ni mtu ambaye haoni tofauti ya mkwe na rafiki anadiriki kutuma msg za ajabu ajabu kwa mama yangu mzazi na ndugu zangu pale tunapokuwa tumehitilafiana mpaka nikaambiwa "huyu mtu hakufai" wakati angekaa kimya hakuna mtu angejua weakness zake zaidi yangu mimi. Ndo maana nikasema labda kwa maombi.