Hatimaye nimefanikisha

Hatimaye nimefanikisha

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,728
Reaction score
4,172
Ndugu hivi karibuni nilikuja na nyuzi za kulalamika kuhusu matatizo yalionikumba.

ISSUE ILIKUA HIVI
Nilikua kwenye gari binafsi natoka arusha kwenda iringa.nilikua na kiasi cha pesa kwenye gari kama 45 million kwa ajili ya shamba na kununua gari mtu anayeniuzia yupo iringa na ndiye aliyenichezea mchezo.

Baada ya kufika Iringa tuliuziana gari nilimpa million 12 nkabakiwa na 33 million. Usiku huo nililala kwa huyo jamaa aliyeniuzia gari nikaamka na kuanza safari nikiwa na gari niliyoinunua kwenda kununua drip pipe za shambani nikiwa njiani kwanza nilikamatwa kwa kosa la gari kuwa na spotlight.

Pili nilikuwa sina leseni(umri wangu mdogo ulichangia mimi kusumbuliwa zaidi).nililipa faini na kuondoka kwa speed kali nikiwa na hasira

Kufika eneo la tanangozi mbele yangu kulikuwa na gari kubwa na kuna njiapanda inapandisha juu mkono wa kulia kuna jamaa alikuwa na noah ghafla baada ya gari kubwa kupita akaingia barabarani kwa kuwa nilikua kasi sana nikamgonga ubavuni gari yake ikarushwa ng'ambo ya barabara, yangu ikachomoka tyre la upande wa kulia na ikaendelea kwenda na mbele kuna basi la New force limesimama.

Gari ilikuwa inavutia barabara nikajtahidi kuitoa ikaenda kupindukia kwenye kabonde kushoto niliumia uti wa mgongo nikachubuka na mkononi kidogo.

Basi maaskari wakaja kupima pale wakakuta mi sina leseni na yule jamaa wa kwenye noah hana leseni mi nikapelekwa hospitali.

Matatizo yalianza kwani niliibiwa pesa zangu zote pale kwenye ajali lakini cha kushangaza yule jamaa aliyeniuzia gari alichukua gari lile na kwenda kulitengeneza huku akiwaambia watu sikumpa hela yote hivyo bado ananidai.

Wiki mwanamke wangu(sijamuoa ni msichana nilikuwa naishi nae tu kishkaji)eti akauza baadhi ya vitu na kurudi kwao Bukoba kwa kweli nilichanganyikiwa pesa niliyoitafta kwa shida leo narudi kuwa fukara.

Baada ya kuandika uzi hapa nikiomba msaada kuna jamaa ni wakili alinisaidia kunihamisha hospital na nilivyoruhusiwa baada ya kutoka alinipa pesa za kuanzia upya maisha kama laki tatu hivi.

Namshukuru Mungu nipo mtaani napambana upya ila Koku bado nakupenda Mumy uje tuishi pamoja.

Raymond gari nilikumalizia hela yote sikutaka tuandikishane sababu nakujua ila nakudai unasema nikupe million saba, ya nini bro? nitakachokufanyia hutonisahau bado napambana na maisha upya ila kaa ukijua nitapambana na wewe hata ukiwa maiti.

Kitu nitakachokufanyia itabaki historia kwa kizazi chako chote sitakuacha salama, nakuahidi ukoo wako wote watanilaumu kwa nitakachokifanya.
 
Oh oh mdomo huumba na mtu anayetaka kufanya ubaya daima hajisemi
 
Aisee
pole sana kwa yaliyokukuta mkuu kikubwa ni uzima wako pesa hutafutwa
 
ndugu hivi karibuni nilikuja na nyuzi za kulalamika kuhusu matatizo yalionikumba.
ISSUE ILIKUA HIVI
nilikua kwenye gari binafsi natoka arusha kwenda iringa.nilikua na kiasi cha pesa kwenye gari kama 45 million kwa ajili ya shamba na kununua gari mtu anayeniuzia yupo iringa na ndiye aliyenichezea mchezo.
baada ya kufika iringa tuliuziana gari nilimpa million 12 nkabakiwa na33 million.usiku huo nililala kwa huyo jamaa aliyeniuzia gari nkaamka na kuanza safari nikiwa na gari niliyoinunua kwenda kununua drip pipe za shambani nikiwa njiani kwanza nilikamatwa kwa kosa la gari kuwa na spotlight.pili nilikuwa sina leseni(umri wangu mdogo ulichangia mimi kusumbuliwa zaidi).nililipa faini na kuondoka kwa speed kali nikiwa na hasira.kufika eneo la tanangozi mbele yangu kulikuwa na gari kubwa na kuna njiapanda inapandisha juu mkono wa kulia kuna jamaa alikuwa na noah ghafla baada ya gari kubwa kupita akaingia barabarani kwa kuwa nilikua kasi sana nikamgonga ubavuni gari yake ikarushwa ng'ambo ya barabara.yangu ikachomoka tyre la upande wa kulia na ikaendelea kwenda na mbele kuna basi la New force limesimama.gari ilikuwa inavutia barabara nikajtahidi kuitoa ikaenda kupindukia kwenye kabonde kushoto .nliumia uti wa mgongo nikachubuka na mkononi kidogo.basi maaskari wakaja kupima pale wakakuta mi sina leseni na yule jamaa wa kwenye noah hana leseni mi nkapelekwa hospitali.matatizo yalianza kwani niliibiwa pesa zangu zote pale kwenye ajali.lakini cha kushangaza yule jamaa aliyeniuzia gari alichukua gari lile na kwenda kulitengeneza huku akiwaambia watu sikumpa hela yote hivyo bado ananidai.wiki mwanamke wangu(sijamuoa ni msichana nilikuwa naishi nae tu kishkaji)eti akauza baadhi ya vitu na kurudi kwao bukoba.kwa kweli nilichanganyikiwa pesa niliyoitafta kwa shida leo narudi kuwa fukara.
baada ya kuandika uzi hapa nikiomba msaada kuna jamaa ni wakili.alinisaidia kunihamisha hospital na nilivyoruhusiwa baada ya kutoka alinipa pesa za kuanzia upya maisha kama laki tatu hivi.
Namshukuru mungu nipo mtaani napambana upya ila Koku bado nakupenda Mumy uje tuishi pamoja.
Raymond gari nilikumalizia hela yote sikutaka tuandikishane sababu nakujua ila nakudai unasema nikupe million saba,ya nini bro? ntakachokufanyia hutonisahau bado napambana na maisha upya ila kaa ukijua ntapambana na wewe hata ukiwa maiti.kitu ntakachokufanyia itabaki historia kwa kizazi chako chote sitakuacha Salama,nakuahidi ukoo wako wote watanilaumu kwa ntakachokifanya
katika watu wajinga au sijui umetunga wakanza nini wewe,pesa zote hizo unatembea nazo kwenye mfuko alafu gari unayo kwenda kununua hipo mkoa jiranikwani ulipo toka au hukuona kampuni au wadau ulipo toka.simu inaweka pesa yako benki unaweza kuweka na kumlipa kwa mda wowote.biashara au pesa kwenye kulipa ikisha fika milioni sifanya kiboya kama ulivo chukilia wewe.
ndo nyie nao wasikia ukiweka benk mkifikiri kuwa mtakufa zitapotea
 
Kwa hiyo una umri mdogo?
Hizo 45m umezitoa wapi mkuu?
Au Mimi sijakuelewa?
 
Wewe ni limbukeni! Kwa nini unatembea na kiasi kikubwa cha pesa? Benki ulikuwa huzijui? Ulikuwa unataka uwaringishie walimwengu? Kwa nini unaendesha gari kwa spidi kali ihali hujajua kuendesha vizuri na huna leseni? Matatizo ya kujitafutia wala siwezi kukuonea huruma kwa haya...
 
katika watu wajinga au sijui umetunga wakanza nini wewe,pesa zote hizo unatembea nazo kwenye mfuko alafu gari unayo kwenda kununua hipo mkoa jiranikwani ulipo toka au hukuona kampuni au wadau ulipo toka.simu inaweka pesa yako benki unaweza kuweka na kumlipa kwa mda wowote.biashara au pesa kwenye kulipa ikisha fika milioni sifanya kiboya kama ulivo chukilia wewe.
ndo nyie nao wasikia ukiweka benk mkifikiri kuwa mtakufa zitapotea
ushauri murua ntautendea kazi
 
Wewe ni limbukeni! Kwa nini unatembea na kiasi kikubwa cha pesa? Benki ulikuwa huzijui? Ulikuwa unataka uwaringishie walimwengu? Kwa nini unaendesha gari kwa spidi kali ihali hujajua kuendesha vizuri na huna leseni? Matatizo ya kujitafutia wala siwezi kukuonea huruma kwa haya...
mkuu,nani kakwambia sijui kuendesha?
 
Awali ulivyoanza hii stori nilidhani kweli ila mwishoni umeharibu.
45 mil. Unadhani ni mkia kwamba kila mbuzi hupewa bure.
Na umri huu wa miaka karibia 30 sijawahi kuishika 45 cash.
Wapo under 20 walioshika 45 and and above ila karibia wote walioshika fedha nyingi wakiwa na umri mdogo jua hawajazipata kwa shida nyingi, bali walizipata kwa bahati tu.
 
pole sana mkuu...ila kuna maswali umeniacha:ulikuwa kwenye usafiri binafsi ukielekea iringa kununua usafiri(binafsi) je uliponunua la iringa la binafsi ulilotoka nalo ars uliliwacha wapi,ulimlipa ray pesa yake lakini bado ukaendelea kuwa na pesa wakati unarudi ars je ni kiasi gani out of 45 ulizotoka nazo ars
 
pole sana mkuu...ila kuna maswali umeniacha:ulikuwa kwenye usafiri binafsi ukielekea iringa kununua usafiri(binafsi) je uliponunua la iringa la binafsi ulilotoka nalo ars uliliwacha wapi,ulimlipa ray pesa yake lakini bado ukaendelea kuwa na pesa wakati unarudi ars je ni kiasi gani out of 45 ulizotoka nazo ars
Maswali MURUA KABISA...niko nimetulia hapa nasubiri haya maswali yajibiwe.
 
umri wako mdogo ndo maana huna leseni?? ina maana chini ya 18?? bado ulikua unaishi na mwanamke.. akakutenda na bado unamtaka? ukanunua gari bila kuandikishiana any docs? unaendesha gari hovyo hovyo tuuu... mmmhhh
 
Back
Top Bottom