Hatimaye ngoma sasa ni Lowassa vs Magufuli

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,571
Reaction score
53,586
Hii ndio nafasi ya kipekee UKAWA kuchukua uongozi Tanzania, inanikumbusha msisimko tuliokua nao mnamo mwaka wa 2002, tulivyoangusha KANU na kuanza kujenga nchi upya. Yaani CCM wakikwepa hii na kuponea, basi ndio kabisa watabaki uongozini. Lazima walijua Lowassa atahamia upinzani na wapo wamejipanga pia. Yetu macho, tujionee siasa ya Bongo.

 
Hata tukisema tusiongelee tuhuma nzito za ufisadi zinazomkabili Lowassa, ni wazi kuwa Watanzania wana imani kubwa sana na Dk. Mafugufuli..
Wapinzania wameamua kuchukua hii nafasi nawao wanufaike na pesa za Lowassa
 
Hata tukisema tusiongelee tuhuma nzito za ufisadi zinazomkabili Lowassa, ni wazi kuwa Watanzania wana imani kubwa sana na Dk. Mafugufuli..
Wapinzania wameamua kuchukua hii nafasi nawao wanufaike na pesa za Lowassa
Magufuli yupi huyo unayemuongelea anayepelekwa kulinda maovu ya Kikwete, Mkapa na wenzie? Una imani naye peke yakoo....:A S-rap:
 
Huyo Lowassa si ni hivi majuzi tu aliapa kutoachana na CCM? Ni vipi tena? Yaani huu urais atautafuta kwa udi na uvumba, hata kama ni kwa kulisaliti chama kilichomjenga kisiasa na kuungana na kile ambacho kimekuwa kikimtuhumu yeye kwa ufisadi!

Huyu Lowassa hana jipya kabisa ya kuwapa watanzania, manake nafkiri sera zake hazitatofautiana kabisa na zile za CCM, chama ambacho alikuwa akihudumia hadi hivi majuzi.

Tanzania, hili linasikitisha sana ya kwamba hamna alternative nyingine kabisa. Either ni Magufuli au Magufuli ndiye atakaye kuwa rais.
 

dogo ulianza vizuri umemamliza hovyo,lowasa atakuwa chini ya sera za ukawa. huwezi kupata malaika ndani ya kundi la mashetani.huwezi kuonekana msafi ikiwa umesimama jalalani
 

Iconoclastes Siasa ni unafiki na uchafu, hamna jipya, hawa UKAWA walimponda sana Lowassa akiwa CCM, wakamhusisha sana na ufisadi, sasa kwa yeye kuvuka na kuhamia kwao, wamemgeuza kuwa mweupe kama pamba. Huu upuzi upo hadi hata hapa kwetu, sasa hivi akina Wetangula na Kalonzo ndio malaika na nikikumbuka jinsi walivyokuwa wanapondwa na upinzani kipindi kile wakiwa kwenye serikali.

Hata Obama ameongea kuhusu hili, walivyomzuia kuingilia mambo ya Kenya halafu sasa wapo kwenye upinzani na wanamgeukia na kumwomba.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…