Hatimaye naanza kuona amani ya moyo

Hatimaye naanza kuona amani ya moyo

Jing chu

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2019
Posts
385
Reaction score
592
Habari za wakati huu wakuu. Rejea hapa kwanza

Wakuu picha zima liko hapa Nafikiria kufanya maamuzi haya magumu japo naumia sana

Ikumbukwe bado nampenda kama hiki kipindi ambacho niko mbali nae atajirekebisha sitamuacha lakini asipojirekebisha nitaachana nae mazima.

Hakika sasa naiona amani ya moyo baada ya kukaa takribani siku tatu bila kuonana na mke wangu (nimetoka home na kwenda kuishi asipopajuwa)

Siku natoka sikumuaga alinisubili ilipofika saa 6 usiku akapiga simu nikamwambia nipo mitaa ya karibu hivyo ningerudi nyumbani muda mfupi, akauliza mbona haoni baadhi ya vitu vyangu nikamjibu navojuwa alielewa lakini kwa mashaka.

Nikazima simu nikaja kuwasha asubuhi ya kesho yake, kumbe wasiwasi umemjaa hajalala usiku mzima asubuhi kaenda kuripoti police kwamba hajui nilipo duuh.

Nimekuja kupata simu ya mama mmoja akijitambulisha kuwa yeye yuko kwenye kitengo cha ustawi wa jamii na kuwa amepewa taarifa na mke wangu kuwa sionekani.

Nikamjibu ,,,huyo kakurupuka mimi nipo sijapotea na anajuwa nilipo na mimi ni mzimawa afya wala msijali kabisa nikaongezea kwamba nitamtaarifu tena kama kasahau yaliyotokea na aliyokuwa anayafanya akitegemea mimi sina akili timamu. Ofisa akakata simu.

Kiufupi kwa sasa niko na amani nimempigia mara kadhaa kumsalimia na kuongea na mtoto japo mtoto bado hajajuwa kunyoosha maneno, nakula nashiba na nahisi moyo mtulivu zile kelele za kero sisikii tena hadi najiona nitafanikiwa mapema sana kwenye issue zangu.

Hakika nimeelewa kwa nini wengi walinambia ondoka,ondoka, ondoka ikiwezekana usigeuke nyuma bali hudumia mtoto tuu.

Nimepigiwa simu na rafiki yake anadai mke wangu hana amani kabisa. Nikamwambia anakudanganya nadhani now anafurahi kwamba nimeondoka.

Ahsanteni.
 
Hongera kwa kufanya hilo akili itakaa vizuri
 
Hakika sasa naiona amani ya moyo baada ya kukaa takribani siku tatu bila kuonana na mke wangu (nimetoka home na kwenda kuishi asipopajuwa.

Ungeandika baada ya miezi .. ningekupa pongezi kidogo.. miezi 3.. ningeongeza pongezi tena kidogo.. n.k.

Siku tatu eti unampigia simu zote hizo 🤔🤔🤔wewe ndiwe unaumia zaidi..

tuliza boli utafakari kwa kukaa kimya muda mrefu.. ukiendelea na yako.. then rudi kutuwambia unaendeleaje..

Unatia huruma.. unatenda yale huyawezi..
 
Sasa ni muda wa kuvuta chombo kipya, kikizingua nacho unakipiga chini...

Wachuchu ni kama sahani tu, ikizingua unazama kabatini unachomoa sahani nyingine...no stress at all
Huu ndio muda wa kuanza kutumiwa majini na mizimu sasa bado vita haijaisha..😂
 
Ungeandika baada ya miezi .. ningekupa pongezi kidogo.. miezi 3.. ningeongeza pongezi tena kidogo.. n.k.

Siku tatu eti unampigia simu zote hizo wewe ndiwe unaumia zaidi..

tuliza boli utafakari kwa kukaa kimya muda mrefu.. ukiendelea na yako.. then rudi kutuwambia unaendeleaje..

Unatia huruma.. unatenda yale huyawezi..
Sikupingi kwa mawazo yako , sioni kama kupiga simu ni ishara ya udhaifu bali pia nina target zangu. Eniwei iwe hivyo kwako but i m strong enough.
 
Sasa ni muda wa kuvuta chombo kipya, kikizingua nacho unakipiga chini...

Wachuchu ni kama sahani tu, ikizingua unazama kabatini unachomoa sahani nyingine...no stress at all
Kabisa
 
Mdau hapo kasema kweli tupu, mkuu maamuzi uliyofanya ni sahihi kabisa kwa mwanaume. Ila inaonekana yakutesa.

Kwenda mbele huendi nyuma hurudi na kati pia haupo, em kua na msimamo sasa, hizo simu nyingi za nini. Mwache apige yeye wewe timiza wajibu wako wa kuhudumia mtoto, kama inatakiwa kila mwezi kiasi kadhaa basi toa hicho kiasi kwa tarehe husika.

Ukimcheki mara moja kwa mwezi kujua hali ya mtoto si mbaya, sio simu za mala kwa mala na mtoto mwenyewe hata kuongea hawezi unampigia simu nani sasa.
 
Majini hutumwa hata na mtu asiye mke/mume...

Wanawake wa siku hizi wamejisahau sana, na kauli mbiu ya fursa sawa kwa wote wengi wameshindwa ielewa...
Hatamimi nikiamua natuma hayo majini kwani bei gani
 
Mdau hapo kasema kweli tupu, mkuu maamuzi uliyofanya ni sahihi kabisa kwa mwanaume. Ila inaonekana yakutesa.

Kwenda mbele huendi nyuma hurudi na kati pia haupo, em kua na msimamo sasa, hizo simu nyingi za nini. Mwache apige yeye wewe timiza wajibu wako wa kuhudumia mtoto, kama inatakiwa kila mwezi kiasi kadhaa basi toa hicho kiasi kwa tarehe husika.

Ukimcheki mara moja kwa mwezi kujua hali ya mtoto si mbaya, sio simu za mala kwa mala na mtoto mwenyewe hata kuongea hawezi unampigia simu nani sasa.
Sawa mkuu, nilitaka ajue sijamkimbia na wala simuogopi napiga sio kumuumiza bali ajue nipo na hana namna ya kunifanya.
 
Hakuna kitu cha muhimu kama kuwa na Amani ya nafsi mkuu, hizo pilipili za ndoa zinawashaga mda mwingine hadi unasema huyu mke au kituko gani
 
Back
Top Bottom