Hatimaye mpenzi wangu amekubali kusuluhisha

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
376
Habari wanajamii?

Leo nina furaha sana. Baada ya misukosuko mingi kati yangu na mpenzi wangu, leo amekubali kutafuta suluhu. Kama mtakuwa mnakumbuka nilikuja hapa mara kadhaa kuomba ushauri juu ya mpenzi huyu.

Toka mwaka jana mwezi wa nne tulikuwa ni watu wa kulumbana. Mimi binafsi nikiwa sijui tatizo liko wapi. Kila nilipojaribu kuomba kujua chanzo, mwenzangu hakuwa akinipa sababu kuu. Hajawahi kunikuta na mpenzi mwingine achilia mbali hata msg au simu. Makosa ninayo ingawa ni ya kuongeleka.

Ilifika kipindi alinitamkia kwa simu kuwa hanipendi tena na niendelee na yangu. Nilijikuta nakuwa mpole na kumuuliza shida iko wapi. Akajibu kwa ufupi kuwa amenichoka. Siku hiyo nilipata hasira na kujibizana kwa simu maneno mabaya. Yeye akinisema vibaya nami nikimsema vibaya.

Baada ya hasira nilirudi kuomba msamaha na kuomba anijulishe wapi nimekosea. Hakunijibu kabisa. Nilijisikia vibaya sana. Nikalazimika kwenda kwake kuonana naye. Bahati nzuri alikuja na tulionana ambapo alinikaribisha kwa maneno mabaya hata nikajikuta nikilia sana.

Sijui nini kilimpata ndipo akanieleza shida kuwa tangu alipogombana na kaka yangu amekosa amani nami lakini yu radhi kwenda kumuomba msamaha kwani ni yeye alimkosea ndipo atakuwa comfortable kuwa nami na ataacha kabisa kunifanyia mambo mabaya.

Ninashukuru kwa hatua hii nami nikaona nilete humu kwa ushauri ama lolote.
 
Ni jambo la kumshukuru mungu kwani siku zote hakuna lenye mwanzo likakosa kuwa na mwisho.

Ila ndio mjifunze sasa ugomvi gani huo wa zaidi ya nusu mwaka hauishi. Siku zote watu wakigombana huwa wanakaa chini na kuyazungumza yanakwisha sasa nyie miezi yote hiyo mmmhh.

Kama yatakwisha mbadilike aisee
 
Hongera sana. Mungu azidi kukutetea na kukupigania ktk mahusiano yako.
Mtu yyte akikujibu ovyo usimrudishie, kaa kimya itakuongezea kitu sana, kujibishana naye utaonekana mtu wa ajabu sana.
Mfanye haraka mfunge ndoa, kumegana ndani ya ndoa kuna raha sana.
Have a nice day
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom