MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Huwezi kuamini lakini ni kweli kuwa takribani siku sita tokea Sumaye alazwe hospitalini, aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Lowassa ambaye wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu alimgeuza Sumaye kuwa kama msemaji wake wa karibu ameenda kumtembelea hospitalini.
Ninaamini safari za viongozi wakuu wa serikali na CCM kufika hospitalini kumtembelea Sumaye zimechochea uamuzi wa Lowassa kufika hospitalini as soon as possible!
Viongozi wakuu wa serikali na CCM wameonyesha ukomavu wa kiwango cha juu kifikra na kimtazamo wa kisiasa kwenda kumtembelea Sumaye haraka iwezekanavyo kabla hata ya viongozi wakuu wa CHADEMA baada ya kupata habari hasa ikichukuliwa mazingira ya hali ya kisiasa nchini.
Ama kweli, akufaaye kwa dhiki...
Aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, Edward Lowassa na mkewe, Mama Regina Lowassa wakimpa mkono wa pole, Waziri Mkuu mstaafu ambaye alikuwa ‘’mpiga debe’’ wake wa karibu wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, Frederick Sumaye, kwenye taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ya Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, Januari 13, 2016.

Last edited by a moderator: