Hatimaye John Stanley ambaye ni mwanafunzi wa Masomo ya Uongozi, chuo kikuu cha Usafirishaji, Jana ameibuka kidedea kwa kupata ushindi mnono katika uchaguzi wa shirikisho hilo uliofanyikia Chuo Cha Saut Mwanza. Zaidi ya Vyuo hamsini vilishiriki katika uchaguzi huo ulishirikisha vyuo vyote vikuu vya bara na Visiwani.