Hatimaye Halima Mdee ametuthibitishia kuwa PhD's walizonazo Watanzania baadhi ni za hovyo kabisa!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,554
108,895
Nikichukua maelezo ya mwenye PhD yake aliyoyatoa hivi majuzi tu halafu nilivyomsikia jana Halima Mdee akichambua Kiutaalam na Kiumakini kabisa masuala ya Kiuchumi kwa Tanzania naona au nadhani inabidi Yule Mtu wa juzi ambaye kiuhalisia ni mmiliki wa Shahada ya Uzamivu ( PhD ) basi angempa tu hiyo PhD yake Halima Mdee halafu na Yeye akabaki na Elimu ya Mdee.

Mbunge wa Kawe Halima Mdee sitaki kuwa mnafiki na bila kupepesa macho wala kumung'unya maneno na kutikisa masikio kwa ule ufafanuzi wako wa jana nakupa pongezi / kongole nyingi mno kwani umeonyesha kuwa hukuenda Shule kupata tu sijui Degree au Masters au PhD bali ulienda kuongeza maarifa yako ambayo kiukweli Mimi binafsi nimeyapenda.

Mwisho nitoe tu RAI kwa Mteuzi Mkuu wa Vyeo nchini Tanzania kuwa siku zingine akiwa anateua Watu wake wa kumsaidia Kazi basi si lazima awe tu anatumia Kigezo cha kuwa na PhD bali aamini kuwa kuna wengine kama akina GENTAMYCINE mwenye Elimu tu ya darasa la Saba na akina Halima Mdee wenye sijui Degree kama siyo Masters tunaweza kumsaidia hadi akashangaa kutokana na kwamba tumebarikiwa mno akili za kuzaliwa kuliko tu za kujibia na kupigia Chabo Mitihani Shuleni na Vyuoni.

Hongereni sana wale Watanzania ambao hivi sasa mnachukua PhD's zenu huko katika Vyuo Vikuu mbalimbali duniani ila ukweli tu ni kwamba na mfahamu kuwa hadi hivi sasa kwa PhD's tulizonazo nchini Tanzania hakuna ambazo zimeweza kuleta Tija yoyote kwa Taifa letu hili hivyo mnaposoma huko tambueni tu kwamba Watangulizi wenu wameshatuonyesha huko mlipo mnapoteza tu muda.

Tanzania inahitaji Watu wenye akili za Halima Mdee kama 100 tu ili nchi iende kuliko wenye PhD's 100,000 kama za Yule wa juzi ( ambaye aliropoka pasipo kuwa na data zozote ) ambazo hazina Tija yoyote ile kwa nchi yetu zaidi tu ya kutishiana tu humu mitaani.

Naamini kwamba message sent and delivered.

Nawasilisha.
 
Wabunge wengi wa upinzani ni akili kubwa

Hoja yangu hapa siyo masuala ya UCHADEMA au UCCM Mkuu bali Mimi nimejikita hasa katika uwezo wa Mtu Kiakili na ndiyo maana unaweza kuona hata katika Content yangu sijaweka masuala ya itikadi za Kisiasa. Siku nyingine tuwe tunaelewa kwanza thread context kisha ndipo tuchangie.

Mwisho niseme tu kuwa sitaki kukubali au kukataa kwamba Wabunge wengi wa Upinzani wana akili kubwa ila niseme au nisisitize tu kwamba IQ ya Halima Mdee kwa uchambuzi wake tu ule wa jana hasa kuhusiana na masuala ya Uchumi wa Tanzania umezidi wa Yule wa juzi ambaye ni mmiliki wa Shahada ya Uzamivu ( PhD )
 
Mungu apishilie mbali...huyu anavyokicha cha ARUSHA hata JAMAICA ambako hicho kitu kinatumika kama mboga hawezi kupewa ujumbe wa nyumba kumi....KAWE wanajuta,kulia na kusaga meno...

Hoja yangu ni IQ ya Kutukuka ya Halima Mdee dhidi ya mmiliki wa PhD wa pale MAELEZO na sijazungumzia hapa suala la Kawe. Sasa nimegundua na kujua ni kwanini Watanzania wengi huwa mnafeli Mitihani yenu huko Shuleni na Vyuoni kwani huwa mnakurupuka kuliko kujibu kile ambacho mnatakiwa kukijibu.
 
Hoja yangu ni IQ ya Kutukuka ya Halima Mdee dhidi ya mmiliki wa PhD wa pale MAELEZO na sijazungumzia hapa suala la Kawe. Sasa nimegundua na kujua ni kwanini Watanzania wengi huwa mnafeli Mitihani yenu huko Shuleni na Vyuoni kwani huwa mnakurupuka kuliko kujibu kile ambacho mnatakiwa kukijibu.
Over our dead body!! utakuwa na shida sana kwenye ubongo wako kama MDEE ni mmoja wa watu unaowaweka na kuwarate wana Good Intelligence Quotient.... labda tutumie demokrasia na tukubali kwa uelewa wako na watu uliowahi kuwaelewa kutokana na limitation ya uwezo wako...
 
Back
Top Bottom