Makwizi Band
JF-Expert Member
- Aug 19, 2024
- 2,691
- 4,056
Huyu Mondlane ana uhusiano wowote na rais wao wa kwanza aliyeuawa kwa kupigwa bomu?
Mapinduzi yeyote au mabadiliko yeyote lazima yawe na gharama. Miongoni mwa gharama hizo ni watu baadhi kufa na wengine kuwa walemavu katika mtifuano sababu wenye madaraka hawatataka kuachia kirahisi.H
Hapa ndo mjue siasa za ki Frica ni upuuzi sentence ina sema hivi kiongozi wa upinzani anaamulu maandamano huku akuwa mafichoni alikokimbilia baada ya kuuawa kwa aliyekuwa mqasheria wake maana yake yeye anapenda kuishi ataki kufa au kuumizwa kulemazwa lkn anaotaka kuwatawala ana waamulu waandamane ili??alafu wakifanikisha hayo maandamano kwa kuumizwa na kulemazwa atakuja kumtawala Nani? Na kwanini nayeye asije kuandamana Kama watu wengine Kama akiumizwa ionekane kaumizwa au kafa kwa kutetea haki za watu wake?
Bongo kila mtu anataka aishi haijalishi anaishije ila hataki tabu na mtu. Unategemea kuna maandamano humo! Mnategemea CCM iondoke madarakani kwa dua?🤣Sio mwa fisiem vs sisi manyumbu.. Unadhani bongo nyoso kiongozi akae ufichoni atoe maelekezo kuna mtu ataingia road, sisi ni maiti zinazotembea, labda vizazi vijavyo, wakikuta population tushagota kwenye milioni 100 huko, badari ishauzwa kwa mwarabu, gesi ya mchina.. Miradi yote imebinafsishwa, mfagizi wa ofisi ni muhindi, mbuga zote za wanyama zimepigwa bei, madini wameachiwa wachache, asilimia 10 tu ndio wanafaidika the rest kula ugali maharage ni anasa huenda hawa wakawa wamefufuliwa na ujio wa nabii issa.
Utajiri wa CCM ni uwoga na ujinga wa mtanzania.Bongo kila mtu anataka aishi haijalishi anaishije ila hataki tabu na mtu. Unategemea kuna maandamano humo! Mnategemea CCM iondoke madarakani kwa dua?🤣
Kwani wanayo hatimiliki ya maisha?Vibaka wa ccm wanaadai watatawala milele
Inasemekana hao FRELIMO walipewa muongozo wa wizi wa uchaguzi na wabobevu chichiemu. Kama imebuma huko hata kwa walimu wao ni suala la muda tuHatimaye FRELIMO iko matatani, mwisho wake umefika!
We ngedere pambana na chagadema yenu, CCM watanzania bado wanaipenda na kuiamini, our country cannot be lead by dogs. CCM mpaka miaka 100 ijayo itakuwepoNi swala la muda tu, hata hawa majangili wa kijani nao watafurumushwa. Maana kama kuchokwa, tushawachoka. Imebaki kutolewa kwa mateke tu.
Lema ? Kwl nyie ni wehu. Yule mvuta bangi mwizi wa magari aweYatatoka tu. Unajua ccm wana-survive kwa sababu hatuna chama imara cha upinzani. Ukitaka kuona cdm kinaimarika mtoe Mbowe pale juu muweke Lema au yule jamaa wa Mkoa wa Mara
Even life, is not PermanentNimeipenda hii comment.
Wala dini siyo ishu. Changamoto ni jeshi la polisi kufungamana na watawala. Hapo ndio utata maana watu kupigwa kuumizwa hawataki ila wanataka mabadiliko.Hapa kwetu yametuweza. Tumezamishwa kwenye dini kama mambumbumbu. Akishika mkristo anatetewa na Wakristo na waislamu hivyo hivyo. Hata kama ni ujinga unafanyika.
Watanzania sio wajinga hilo nakataa, watanzania wanapenda kuishi gwana allergies na kipigo cha mwna koko.Utajiri wa CCM ni uwoga na ujinga wa mtanzania.
Hii haiwezi kubadilika kwa kizazi chetu sisi.
Tatizo lenu CHADEMA Mboe akitangaza maandamano hamufiki pale Boma na badala yake munaandamana humu JF.Kwa wanaofuatilia siasa za Mozambique, hali ni mbaya kwa chama tawala cha Frelimo pamoja na serikali iliyoko madarakani. Baada ya uchaguzi kuisha na serikali kujitangaza kushinda kwa wastani wa asilimia sabini, wananchi wameikata, wakiongozwa na kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane.
Kinachotokea sasa hivi ni kwamba huyu kiongozi wa upinzani ndiye mwenye nguvu na sauti kuliko serikali; yeye ndiye anayeamuru nini kifanyike. Anaratibu maandamano akiwa mafichoni, baada ya kukimbia nchi kufuatia mauaji ya wakili wake.
Hali si shwali. Mfano jana, ameamrisha kufanyika maandamano kwa siku tatu bila kupumzika, akilenga bandari kufungwa pamoja na mipaka. Kumeitikiwa kwa muitikio mkubwa katika miji yote mikubwa ya Maputo, Beira, na Nampula pamoja na miji mingine midogo, huku karibu watu 40 wakiwa wameuwawa na polisi.
Inchi inaongozwa na mtu aliyeko mafichoni, huku Rais Nyusi akiwa hana sauti. Ukiona mwenzako ananyolewa.
Soma, Pia: Yanayojiri kwenye Uchaguzi Mkuu wa Msumbiji: FRELIMO (Chama rafiki ya CCM) kushinda Uchaguzi 09 Oktoba?
Hii ndo Raha ya taifa kuwa na wapinzani wa kweli na sio wapinzani uchwara kama wa bongoUtukufu wa Mungu ni wa ajabu sana!
Hata Mozambique polisi walikuwa kalibu sana na watawala lakini sasa hivi pumzi inakata, nisema hawa kilichowasaidi ni ile vita ya wenyewe kwa wenyewe, sasa hivi wanamkumbuka Alfonso dhalakama kama alikuwa mtu sahihi kwao wanamlani Chissano ndiye alieasisi wizi, dhuluma na umaskini waliyokuwa naoWala dini siyo ishu. Changamoto ni jeshi la polisi kufungamana na watawala. Hapo ndio utata maana watu kupigwa kuumizwa hawataki ila wanataka mabadiliko.
Macron hakuiba kuraHata Mackron alikutana na maandamano!
Mkuu,Akishika mkristo anatetewa na Wakristo na waislamu hivyo hivyo.