Hatimaye Drogba Aoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye Drogba Aoa

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, Jun 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  [TABLE="width: 491"]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]Baada ya kuishi na mpenzi wake kwa muda mrefu, nyota wa soka wa Chelsea na Ivory Coast, Didier Drogba amefunga pingu ya maisha na mpenzi wake katika harusi ya kukata na shoka ambayo masupastaa wa R&B, wacheza soka na nyota wa NBA walihudhuria.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Mfumania nyavu wa Chelsea, Didier Drogba ameamua kumuoa mpenzi wake wa muda mrefu ambaye amezaa naye watoto watatu kwa kufunga ndoa ambayo sherehe yake ilihudhuriwa na masupastaa mbalimbali.

  Drogba mwenye umri wa miaka 33, alifunga ndoa na mama watoto wake, Lalla Diakite mjini Monaco, Ufaransa.

  Mmiliki wa Chelsea, bilionea Roman Abramovich ndiye aliyeiongoza harusi hiyo huku Salomon Kalou na Florent Malouda wakiwa wapambe wa bwana harusi.

  Nyota wa RnB, Akon na masupastaa wa mpira wa kikapu wa NBA walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika harusi hiyo.

  Fally Ipupa toka Jamhuri ya Kongo naye alikuwepo kwenye harusi hiyo sambamba na nyota wa muziki wa Nigeria, J Martins ambaye alipewa usafiri wa bure na Drogba ili aweze kupafomu na Ipupa wimbo wake wa Jupa Remix.

  Michael Essien naye alitia maguu kwenye harusi hiyo baada ya kupanda pipa toka Nigeria ambako alishiriki mechi maalumu pamoja na mastaa mbalimbali wa soka duniani kumuaga rasmi Nwako Kanu ambaye amestaafu soka rasmi baada ya miaka 16 ya kulisakaka kabumbu kimataifa.  droghba.jpg [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Jamaa ni matawi ya juu!
   
 3. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 3,058
  Trophy Points: 280
  Haina utamu ht, watoto watatu juu aaah
   
 4. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Commitmet muhimu! Amechelewa sana! Miaka 33????
   
Loading...