Hatimaye Danguro Zakhem Mbagala- Dar labomolewa na serikali

Hatimaye Danguro Zakhem Mbagala- Dar labomolewa na serikali

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
danguro--april19-2014.jpg



  • Dada poa waduwaa..wananchi washangilia
Hatimaye serikali imelibomoa eneo lililogeuzwa kuwa danguro la wazi, ambako vitendo vya ngono vilikuwa vinafanyika hadharani, Mbagala Zekhem, jijini Dar es Salaam.

Bomoa bomoa hiyo ilifanywa juzi na Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya gazeti hili kuandika habari ya kiuchunguzi ambayo ilibaini watu wa rika mbalimbali kujihusisha na biashara ya ngono ya wazi katika eneo hilo.

Eneo hilo lililopo Mbagala Zakhem, limekuwa maarufu baada ya watu kuugeuza uwanja uliojengwa vibanda vya mbao kwa ajili ya biashara ya chakula, kuwa kama eneo huru la kufanyia vitendo vya ngono.

Katika kuonyesha kuwapo idadi kubwa ya wanaoshiriki kwenye biashara hiyo, kila sikuinaelezwa kukusanywa ndoo tatu ya mipira ya kiume (kondomu) iliyotumika.
Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo, wameliambia NIPASHE Jumamosi kwamba bomoabomoa hiyo ilifanyika juzi saa 7:30 mchana kwa kutumia magari mawili aina ya kijiko huku polisi wakiweka ulinzi mkali.

"Kila mtu hakufahamu kama wangekuja hawa jamaa kubomoa sehemu hii, tuliona magari na polisi yakivamia na kuanza kubomoa," alisema Abdallah Saidi.
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, alisema amekerwa na vitendo vya kinyama vinavyofanywa na watu hao, hivyo ameamua kupambana nao.

Alisema aliposikia kwamba kuna watu wanafanya ngono hadharani kwa makundi aliumia sana, kwani miongoni mwao wapo watoto. "Haingii akilini kuona watu wazima wanafanya mapenzi hadharani, ni jambo baya na linaharibu watoto wetu ni lazima kuchukua hatua kali," alisema.

Alisema tayari wamebaini kuwapo na madanguro mengine ya aina hiyo (hakuyajataja), kinachofanyika ni kuwa yanafuatiliwa kwa makini, kisha hatua zichukuliwe kuyatokomeza.

"Ukiachana na kukerwa kwangu, pia kwa sasa tupo kwenye zoezi la kusafisha jiji, hatutakubali kuona eneo la wazi linachafuliwa," alisema.
Hata hivyo, Mjema aliwataka wajumbe wa Bunge maalum la katiba mpya, kuhakikisha wanatunga sheria ya ngono ambayo itapiga vita vitendo vya aina hiyo pamoja na ushoga.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kiondo, alisema kazi wanayofanya ni kusimamia sheria na sio kuwakamata watu wanaojihusisha na biashara hiyo.
Alisema kazi ya kupambana na biashara ya ngono inatakiwa uangalifu wa hali ya juu ili kuifanikisha.

Awali mwandishi wa gazeti hili alishuhudia jinsi idadi kubwa ya wanaume wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 50 wenye hadhi tofauti, wakipigana vikumbo kwa kuingia na kutoka kwa ajili ya kupata huduma hiyo chafu.

Aidha, uchunguzi ulibaini kuwa mwanamke mmoja alikuwa akishiriki vitendo vya ngono na wanaume zaidi ya 20 kwa malipo ya Sh. 3000 kwa mkupuo mmoja.
Awali, eneo hilo wazi lenye ukubwa kama mita 25, watu walikuwa wakifanya ngono ya wazi huku wanaume wengine wakiwa wamejipanga wakisubiri wenzao kumaliza ili na wao wajinafasi.

Mmoja wa wanawake hao (Jina linahifadhiwa) alisema wapo wanawake zaidi ya 30 na wana uwezo wa kuwahudumia wanaume kati ya 100 hadi 300, hivyo inakuwa kazi ngumu kutumia eneo dogo kwa sababu itawapotezea muda.

WANANCHI WASHANGILIA
Baadhi ya wananchi waliokutwa katika eneo hilo, wamesema wamefurahishwa na hatua hiyo kwa sababu watoto wao walikuwa wakiharibiwa.

Walisema walikuwa wakipata taabu kuwaangalia watoto wao kutokana na baadhi yao kubainika huenda eneo hilo.

Christopher Mtandi (25) alisikika akilipongeza gazeti la NIPASHE kwa kuanika uchafu huo na kueleza kuwa hatua hiyo imesababisha serikali kufahamu na kuchukua hatua.

"Kila siku ikifika majira ya jioni eneo lote hili linajaa mipira ya kondomu, sasa tutapumzika kuona uchafu ule ukiendelea," alisema.
Naye Amina Mwenyimvua alisema wanaume wengine waliokuwa wakishiriki vitendo hivyo walikuwa na umri chini ya miaka 18.

"Vijana wengi hapa Mbagala wamekwenda eneo lile kupata huduma ya mapenzi, hatujui athari itakayotokea kwani nina uhakika wengi hawajui mbinu ya kujikinga na Ukimwi," alisema Amina.

DADA POA WAPATWA NA KIGUGUMIZI
Baadhi ya wanawake wanaojihusisha na biashara ya kujiuza katika eneo hilo, walijikuta wakiwa na simanzi baada ya kushuhudia hali hiyo.

NIPASHE iliwashuhudia wanawake wapatao watano wakiwa wamesimama juu ya kifusi cha matofali na mbao zilizovunjikavunjika wakiwa wameshikwa na mshangao.
"Siamini kilichotokea, hatuna la kufanya kwani tulitegemea tutafanya kazi kwa hali kama hii hakuna kitu tena," alisika mmoja wao akisema.

Hata hivyo, mwandishi wa gazeti hili alipojaribu kuwadodosa wanazungumziaje zoezi hilo, waliondoka haraka huku wakisema hawana muda wa kuongea na mtu.
"Sisi tunajadili mambo yetu, wewe hayakuhusu, tena usitake kutuharibia siku zetu nenda kawaulize wale walioshuhudia tukio zima," alisikika mmoja wao akifoka.

TUMEANZA KAZI: POLISI
Kamanda wa Mkoa wa kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema kazi iliyofanyika ni ya kawaida katika kuboresha mazingira, lakini wameanza kulishughukia tatizo la madanguro.
"Kwa ufupi tumeanza kushughulikia maeneo ya madanguro, hatuna haja nao Changudoa maana wanahitaji elimu ili kujua kazi wanayoifanya ni haramu," alisema Kamanda Kiondo.

Scource: Nipashe publication


 
Nakumbuka nilipoleta mada hii hapa kutoka chanzo cha Nipashe publication wiki iliyopita, kisha mbunge Ndugulile wa eneo hilo alienda eneo husika na kuchukua picha kicha kutuletea ushahidi wa taswira za eno husika hapa, kuna waliomrushia madongo kuwa hatua gani anachukua, nikamtetea kwamba kuna taratibu ambazo anatakiwa kufanyia kazi nao watendaji wa vyombo husika ndipo hatua stahiki ifanyike. Hapa ni ushahidi kwamba mbunge huyo kafanya kile ambacho wengi walikuwa hawajui kama anawajibika kwa kufuata taratibu.

Napongeza juhuzi zilizofanywa na uongozi wa wilaya ya Temeke, na kinachotakiwa kufanyika sasa kuna aina za biashara ambazo zinaleta taswira mbaya za kuashiria ngono maeneo ambayo ni maskani ya kifamilia, nako kufanyiwe kazi kama wizara husika ilivyobainisha mwezi uliopita kwamba kuna mkakati wa kuhakiki biashara na leseni zake kama zinaendana na sheria pia maelekeo na miiko yake.
 
Ngono zembe zilikuwepo tangu waqt wa mkoloni waqt huo dada poa wakiitwa WAHAYA. Sio rahisi kkukomesha hii biashara ila inaweza ikadhibitiwa isifanywe kizembe. Tatizo viongozi wetu wengi wanapenda uroda lkn hawako tayari kukubali hilo hadharani
 
Ngono zembe zilikuwepo tangu waqt wa mkoloni waqt huo dada poa wakiitwa WAHAYA. Sio rahisi kkukomesha hii biashara ila inaweza ikadhibitiwa isifanywe kizembe. Tatizo viongozi wetu wengi wanapenda uroda lkn hawako tayari kukubali hilo hadharani
happyBucket.jpg happyBucket.jpg happyBucket.jpg
Ndoo tatu zilizojaa condom daily zilikuwa zinakusanywa

Ngono zembe zipo wakati wote na popote lakini si hadharani. Huko mafichoni wanakojua wenyewe waachwe na hakuna anayewafuatilia huko. Lakini hili la hadharani kama wapo kwenye vilabu vya pombe huku watoto wakishuhudia, hapana. Mbaya zaidi habari zinasema wateja wakubwa walikuwa ni vijana chini ya umri wa miaka 18. Napongeza hatua waliyofanya. Kujipanga msitari kweupe kana kwamba wanaenda kupakuliwa bakuli la maharage? Hili la ukusanyaji wa ndoo tatu za condom kila siku inaonyesha dalili ya kilichokuwa kinaendelea hapo, ni sodoma haswa.
 
Wenyeji tulikuwa tunapata mpaka za kuonja na nyongeza kwenye eneo hili bila kusahau tulisikilizwa tukipungukiwa na mikopo ilikuwepo.

Supply imepungua nafikiri bei itapanda
 
Wenyeji tulikuwa tunapata mpaka za kuonja na nyongeza kwenye eneo hili bila kusahau tulisikilizwa tukipungukiwa na mikopo ilikuwepo.

Supply imepungua nafikiri bei itapanda

Sikujua msongamano kwenye madaladala ya Mbagala hadi watu kuning'inia milangoni kumbe walikuwa wanawahi biashara huko Zakhem.
 
Kujipanga msitari kweupe kana kwamba wanaenda kupakuliwa bakuli la maharage? Hili la ukusanyaji wa ndoo tatu za condom kila siku inaonyesha dalili ya kilichokuwa kinaendelea hapo, ni sodoma haswa.

huduma nzuri unapata kwa foleni mzee, hapa tulikuwa tunajali afya zetu tulikuwa tunavaa tatu kwa tendo. Ila serikali wametukata stimu, kwani wangeweza kuuza hata hiyo byproduct mbele inahitajika.
 
Sikujua msongamano kwenye madaladala ya Mbagala hadi watu kuning'inia milangoni kumbe walikuwa wanawahi biashara huko Zakhem.
mkuu tulikuwa tunawahi, si unajua ukichelewa pombe inatiwa maji, ila hapo walitia ndimu.

mbagala tutakosa watalii wa ndani toka sinza/mwenge na maeneo kama hayo, hawa walikuwa wanatuungisha huduma za dada zetu hapo uwanjani, bodaboda, chips tulikuwa tunawakaba pia.
 
sasa hawa wahudumu na wateja watatawanyika hovyo, hivyo kabla ya kuvunja wangewaandalia watoa huduma shughuli mbadala.
 
serikali ya mtaa ilikuwa haikusanyi ushuru kweli hapo...?
 
Nahisi hadi diwani wao alikua mteja hapo. ina maana bila nipashe tusingejua?!
 
naipongeza serekali kwa kazi nzuri walioanza kuifany, watoto wengi san wamekuw wakipotea kutokan n madanguro haya.
 
Jambo lamaana.niliwahi kuandika humu hii habari .dar kama sodoma nagomora.wapo walionibeza wengine walinipa ushirikiano.napongeza sana mamlaka husika kwa hatua mliochukua.pamoja na jf kulirusha hewani
 
Nakumbuka nilipoleta mada hii hapa kutoka chanzo cha Nipashe publication wiki iliyopita, kisha mbunge Ndugulile wa eneo hilo alienda eneo husika na kuchukua picha kicha kutuletea ushahidi wa taswira za eno husika hapa, kuna waliomrushia madongo kuwa hatua gani anachukua, nikamtetea kwamba kuna taratibu ambazo anatakiwa kufanyia kazi nao watendaji wa vyombo husika ndipo hatua stahiki ifanyike. Hapa ni ushahidi kwamba mbunge huyo kafanya kile ambacho wengi walikuwa hawajui kama anawajibika kwa kufuata taratibu.

Napongeza juhuzi zilizofanywa na uongozi wa wilaya ya Temeke, na kinachotakiwa kufanyika sasa kuna aina za biashara ambazo zinaleta taswira mbaya za kuashiria ngono maeneo ambayo ni maskani ya kifamilia, nako kufanyiwe kazi kama wizara husika ilivyobainisha mwezi uliopita kwamba kuna mkakati wa kuhakiki biashara na leseni zake kama zinaendana na sheria pia maelekeo na miiko yake.

Mbunge Ndugulile huyu huyu tunayewinda nae ma-babies kila siku au mwingine? Kweli mtu asiye mnafiki hawezi siasa za Bongo!
 
Itafikia hatua sasa ukienda nchi za watu wakikagua passport kama umetokea Tz kwanza utaanza kupigwa sachi kama una madawa ya kulevya,pili kupimwa Ukimwi
 
Hongera sana jeshi la polis temeke,huku kinondoni ndo kuna mabaa na madanguro mengi sana ,jeshi polis kinondoni fanyeni hivyo
 
Hili jambo mi naona halizungumzwi katika mawanda yanayostahili. Danguro hilo lilikuwa nyuma ya ukuta wa Dar live, ukumbi unaomilikiwa na ndg Erick Shigongo ambaye anamiliki utitiri wa magazeti hapa nchini. Ni dhahiri kuwa biashara hiyo ilifikia kileleni mara tu ukumbi huo ulipoanzishwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu eneo hilo nyakati za usiku. Magazeti ya huyu jamaa yapo kwenye OPERESHENI FICHUA MAOVU (OFM). Na mara nyingi waandishi wa magazeti hayo hupatikana katika ukumbi ule sasa kwanini hawakuwahi kufichua maovu yanayotendeka upenuni mwa ukumbi wao? Wanahaha kufichua ufuska unaofanyika vyumbani mwa watu ile wanauacha unaofanyika hadharani tena upenuni mwa eneo lao. Hawa watu ni wanafiki sana. Nahisi ni vyema hii ishu iishe katika hali ambayo Shigongo atabaki na majeraha ili awe na weledi katika kazi za magazeti yake.
 
Back
Top Bottom