Hatimaye COET-UDSM yafungwa baada ya mgomo wa siku 4

menyidyo

JF-Expert Member
Oct 9, 2010
1,339
194
wahandisi wamefukuzwa chuo baada ya kugoma baada ya mwanafunzi mwenzao kufukuzwa chuo.
 
DU yaani maprofesar sijui wanafikiria nini maana uwezi kumdisco 4thyr so ndio spirit ya kihandisi maana nchi hii wanataka wafahidi wao tu kila sehemu ni ufisadi mpaka ktk elimu nyaoro uwezi lazimisha wahandisi wafikirie kama unavyofikiria mbona wewe mtoto wako amekushinda umempeleka uk huko ni kulewa kwenda mbele kama unathan alikuwa na akili ungemleta hapo coet unapo fundisha wewe nyaoro tunakujua sana si DIT kote roho mbaya utapata malipo hapa2 dunia
 
ndio alikuwa amekuwa discontinued baada ya kubabikiwa kesi ya kucheat kwenye mtihani. jamaa ana gpa ya zaid ya 3.5. na pia mwalimu nyaoro ambaye ndie alileta hayao mashitaka analalamikiwa pia kuwa ni mwalimu asiye na ushirikiano kwa wanafunzi.
 
Hivi mnafikiri haya mambo hayakuwepo in the 70s and 80s???

Wameshazoea hayo mambo hao Maprof wenu
 
wahandisi wamefukuzwa chuo baada ya kugoma baada ya mwanafunzi mwenzao kufukuzwa chuo.

Duh, ni nouma jamaaani,je hao coet wanachogomea wana hakika nacho au ni kufuata mkumbo tu,halafu inabidi waondoke waende makwao ,wasije wakajaza bure chumba pale mabibo hostel.,anyways best of lucky coet
 
This is very sad.

Why this?? mie nilidhani hii kitu inafanywa sana na tutorial assistant na Madokta, kumbe maprof nao wamo?
Pole sana kijana, MUNGU ATAKUJALIA. Kibaya zaidi hata akirudishwa watamdisco mbele kwa mbele.
 
ndio alikuwa amekuwa discontinued baada ya kubabikiwa kesi ya kucheat kwenye mtihani. jamaa ana gpa ya zaid ya 3.5. na pia mwalimu nyaoro ambaye ndie alileta hayao mashitaka analalamikiwa pia kuwa ni mwalimu asiye na ushirikiano kwa wanafunzi.

Unauhakika kuwa alibambikizwa?

Kwa namna utaratibu wa wanafunzi "kujilipua na madesa" ndani ya vyumba vya mitihani ulivyokomaa, sintashangaa kama jambo hilo ni la kweli!!
 
tuweni objective, amefanya kosa au hakufanya, kama hakufanya basi na walaaniwe walombambikizia na kama amefanya.......!
 
Coet wamevuma walichopanda, ona sasa wengine nawaona huku slab wametimuliwa hata kwakwenda hawajui wanabaki wakirandaranda wakidhani labda senate itabadili maamuzi, Bgup kwa mangwini maana coet walijidai wao ndo wao sasa wanakiona.
 
Jitihada, nziriye nina wasiwasi na uwezo wenu wa elimu. Kwenye hili ni kama mna chuki binafsi na CoET. Mini ni mwanafunzi wa IKR, mchongo mzima naupata, na fitna za Nyaoro hata wahandisi wakongwe wanazijua, ni muda wa kuondoa watu wa namna hii hata kwa kuwapa vilema vya maisha. Inauma dudes, serikali itukandamize, hata sisi kwa sisi jamani. Hebu jiweke kwenye nafasi ya Mbabara afu ufikirie inakuwa aje?
 
Jamani tuache kudakia mada kiushabiki lazima ufuatilie mambo vyema kujua kilichojiri kupata uhakika na utafiti huo ujibu maswali yafuatayo:-

1. Mwanafunzi anaitwa nani?
2. Huyo Mwalimu ni nani? Ameshatajwa kuwa ni Dr. Nyaoro. Ila hawajasema kuwa alikuwa mwenyekiti wa UDASA baada ya Chachage. Ili uwe mwenyekiti wa UDASA lazima uwe mtetezi wa wote wanafunzi na walimu.
3. huyo aliyefukuzwa kafukuzwa, kafukuzishwa au kajifukuza?
4. Huyo Nyaoro anayesemwa ndiye mwalimu wa somo husika au alikua msimamizi wa mtihani? Kiukweli alikua msimamizi.
5. Mwalimu na mwanafunzi wanaugomvi? kama ndiyo ni upi na una uhusiano gani na swala lake?
6. Je huyo mwalimu mwenye miaka zaidi ya Ishirini ya kufundisha chuo amemuonea huyo tu? Anajua mwanafunzi mwenyewe alivyojibu kwenye senate ambayo ndiyo sehemu ambayo mwanafunzi anapata utetezi wa hali ya juu na akiboronga hapo ndiyo basi hata akienda mahakamani hawezi fanikiwa.
7. Kama mwalimu ana ugomvi naye au amemfukuza au amemfukuzisha kama wengi mlivyodai, je yeye ndiye mwenye uamuzi wa kumfukuza mwanafunzi au Baraza bada ya kushauriwa na senate?
8. Unasema hata DIT anawafanyia hivyo je DIT hamna senate?
9. Majuzi walimfuata nyumbani kutaka kumpiga kama binadamu kwa hasira na anahasira na huyo mwanafunzi si angemlipua au kumwita mwizi?
10. Sawa tumeambiwa huyo ndugu ana 3.5 kuwa amefaulu sana ila hatuambiwi out of ngapi, tutajuaje kama alizipata kwa njia ya kucheat ama la na Je tunataka wahandisi wasio na vigezo wenye kujenga miundombinu isiyo kidhi viwango?

Swala la wengine wanaosema mwanae kaenda ulaya kwa kuwa hajui kitu ni sawa kuwa ameelewa hilo na ndiyo maana hakumleta maana mwisho wa siku atacheat au kudisco.

Lingine ni swala la mprofesa kutotaka wenzao wawe maprofesa. Jamani ili mtu awe profesa ni lazima awe amezalisha PhD za kutosha na awe amefanya kazi ya ziada katika Utafiti, Kufundisha na kutoa ushauri wa Kitaaluma sasa akichukia mtu kuwa profesa atampaje PhD? Kingine kwani huyo wa leo ndiyo wa kwanza kufukuzwa chuo akiwa mwaka wa mwisho? Niwape siri mtu wa kwanza kurudia mwaka na kama ingekua utaratibu wa miaka ya 70's angefukuzwa kabisa alikua Arnold Kileo ambaye ni mmoja wa first 14 lakini mwenzie mkenya alidisco kabisa kwahiyo katika kundi la wanafunzi 14 wa mwanzo walihitimu 12 tu.

Sasa niwape uchunguzi wangu na anayebisha abishe kwa uchunguzi na siyo porojo za kuoneana huruma wakati huyo si mwanafunzi wa kwanza kufukuzwa chuo.

1.Tarehe 12 Novemba, 2010, wakati wa mitihani ya marudio (Supplementary Examinations), mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Koleji ya Uhandisi na Teknolojia aitwaye Jamson Babala alikutwa na karatasi, kinyume na taratibu za mitihani. Msimamizi wa mtihani alipomtaka mwanafunzi huyo kumpa karatasi hiyo, mwanfunzi Babala alikataa. Badala yake aliiweka mdomoni na kuimeza. Kufuatana na taratibu za mitihani, msimamizi wa mtihani alimtaka mtahiniwa andike na kutia saini tamko kwenye kijitabu chake cha kujibia maswali kuthibitisha yaliyotokea, na mtahiniwa akafanya hivyo. Kisha akaruhusiwa kuendelea na mtihani wake hadi mwisho, kama taratibu za mitihani zinavyoelekeza.

2.Tarehe 6 Desemba 2010 suala hili la uvunjifu wa taratibu za mitihani lifikishwa katika kikao cha Kamati ya Masomo ya Shahada za awali, yaani Senate Undergraduate Studies Committee, ambapo mtahiniwa Babala pamoja na msimamizi wa mtihani husika na pia msaidizi wake walihojiwa. Katika kikao hicho mtahiniwa Babala alikiri kumeza karatasi ambayo alisema hata hivyo haikuwa na kitu chochote kinachohusiana na mtihani, bali aliikota kutoka sakafuni. Wasimamizi wa mtihani walipohojiwa walieleza kwamba siku ya tukio, kabla ya kuwaruhusu wanafunzi kuingia kwenye chumba cha mtihani, wao walikagua chumba na kuhakikisha kwamba hakukuwa na karatasi au kitu kingine kinachoweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa taratibu za mitihani. Ndipo wakawaruhusu watahiniwa kuingia ndani na kuanza kufanya mtihani. Msimizi mkuu akafafanua zaidi kwa kusema kwamba awali alimwona mtahiniwa akibabaika kama mtu mwenye wasiwasi. Ndipo alipomhamisha kwenda kwenye dawati linguine. Lakini wakati anapita kuangalia vitambulisho vya watahiniwa kwa uthibitisho kwamba watahiniwa wote walikuwa halali, alimkuta mtahiniwa Babala na karatasi, ambayo alikuwa amieficha kwenye kitabu cha kujibia masomo. Alipotaka kuikagua karatasi hiyo ndipo mtahiniwa akiitia mdomoni na kuimeza. Kutokana na majibu ya mtahiniwa na ushahidi wa watahiniwa wawili, Kamati iliona mtahiniwa ana hatia na hivyo ikiapendekeza kwa Seneti aachishwe masomo, kadiri ya maelekezo ya kanuni za mitihani.

3.Pendekezo la kumwachisha masomo mwanafunzi Babala lilifikishwa katika kikao cha Seneti ya Chuo, kilichofanyika tarehe 15 Decemba 2010. Baada kulijadili suala hili kwa kina, Seneti ya Chuo ilikubaliana na pendekezo hilo na hivyo kupitisha uamuzi wa kumwachisha masomo Jamson Babala. Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lifahamishwa kuhusu uamuzi huo katika kikao chake kilichofanyika tarehe 27 Januari 2011 na likaridhia.

4.Kufuatia uamuzi wa Seneti, tarehe 17 Januari Jamson Babala alimwandikia barua Makamu Mkuu wa Chuo akiomba radhi kwa yaliyotokea na kusihi kwamba adhabu yake ipunguzwe kwa kuwa yeye sasa ni mwanafuni wa mwaka wa nne na kwamba wastani wa matokeo yake ya mithihani iliyopita ni wa kuridhisha. Kwa kuzingatia kanuni za mitihani na sheria nyinginezo, ombi hilo halikukubaliwa. Hivyo Jamson Babala akawa si mwanafunzi tena wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

5.Katika matukio yasiyotegemewa, kuanzia tarehe 4 Februari mwaka 2011 kikundi cha wanafunzi wa Koleji ya Uhandisi na Teknolojia wamekuwa wakivuruga madarasa na kuwatisha wahadhiri, wakishinikiza Jamson Babala arudishwe chuoni. Licha ya Mkuu wa Koleji kuongea na wanafunzi hao kuwaelimisha kuhusu hali iliyosabisha Babala kuachishwa masomo, na hata baada ya Makamu Mkuu wa Chuo kukutana nao tarehe 8 Februari 2011, wanafunzi hao wameendelea kuvuruga masomo na kuhatarisha usalama wa watu na mali katika Koleji ya Uhandisi na Teknolojia.

6.Suala hilo lilijadiliwa katika kikao cha dharura cha Baraza la Chuo kilichafanyika jana tarehe 8 mwezi Februari, 2011. Baraza liliagiza kwamba ikiwa vurugu zinazoendela hazitasitishwa masomo ya shahada za kwanza katika Koleji ya Uhandisi na Teknolojia yasimamishwe na wanafunzi husika waondolewe chuoni.

7.Kutokana na kuendelea kupamba moto kwa vurugu katika Koleji ya Uhandisi na Teknolojia, leo tarehe 9 Februari Chuo kimechukua uamuzi wa kutekeleza maelekezo ya Baraza la Chuo la kusimamisha masomo ya shahada za kwanza katika Koleji ya Uhandisi na Teknolojia na kuwaondoa wanafunzi husika chuoni.

Ingekua mimi ningekataa katakata kutenda kosa mwanzo mwisho hata nidanganywe vipi. Maana naskia jamaa alidanganywa na wenzie eti ukikubali kosa ndiyo utasamehewa wakati mambo yameshatinga senate yeye angekuabaliana na mambo kwenye college level kama amekana kutenda kosa mwanzo angekana mpaka mwisho.

Nwasilisha bila chenga.
 
mphamvu naomba nielewe kihivi zaidi, sipo hapa kwa lengo la kufurahia babala adisco sawa! Bali kero yangu ni kwa vitendo vinavyofanywa na wanacoet karibia wote especially maboys, ukiangalia kwa kina hapa chuo wao wamejivisha mamlaka yote ya decision makers. Sakata la babala ni kama limekuwa ni kero badala ya kuwa solidarity, nasema hayo ni kutokana na tangu kunji la coet lianze tumekuwa hatuna raha raia wengine, huwez ukasema niende japo nkanunue hata maji kule coet basi ukifka pale getin ni lazima ubaguliwe kama wewe sio mcoet, na ukilazimisha japo kupita basi wako ladhi wakupige na hayo maji usifanikiwe kwenda kuyanunua, yaan kiufupi taswila ya wao wa coet na sisi wa ungwini walianza kuiibua wao, chukulia hata mpasuko wa mgomo mkuu wa hapa chuoni umepasuliwa na wana coet yaan hawakuwa tayari kutoa support kwa kile tunachokigomea.
 
@Jitihada. Yap hiyo hali hata mimi yamenikuta jtatu, niliingia vizuri kwenye cafe yao. Ila kutoka ikawa ishu, ikabidi nipite geti dogo la kule uwanjani. Ila wanaofanya hayo ni wapumbavu wachachE kwa jina la CoET! SOLIDARITY FOREVER!
 
Jitihada, nziriye nina wasiwasi na uwezo wenu wa elimu. Kwenye hili ni kama mna chuki binafsi na CoET. Mini ni mwanafunzi wa IKR, mchongo mzima naupata, na fitna za Nyaoro hata wahandisi wakongwe wanazijua, ni muda wa kuondoa watu wa namna hii hata kwa kuwapa vilema vya maisha. Inauma dudes, serikali itukandamize, hata sisi kwa sisi jamani. Hebu jiweke kwenye nafasi ya Mbabara afu ufikirie inakuwa aje?

bwana mzee,usiwe na wasiwasi juu ya elimu yangu ,of course i graduated at udsm in 2009-2010 academic year and when i was in the first year i took certain course pl-111 knwn as critical thinking and argumentation ,cjui kama umeshaisoma ?kama sio then ungeelewa kwanini nilitoa hoja ile,of course kama umefanya kosa then unapaswa kupewa adhabu accordingly,na bwana mphamvu matukio ya cheating ktk mitihani yapo mengi hayo nimeyaona pale udsm when i was there,venues like nkrumah,atb,ata,sr na za kule coet kama a102,a104 zote zinachochea kucheat ktk mitihani,kwa hyo mzazi huyo kiumbe kama kweli amecheat tena kameza karatasi ushahidi upotee then let him face the music of cheating,...katika maisha yangu huwa napenda haki itendeke ,so bwana mphamvu kama nimekukwaza am sooooory,nawasilisha.
 
DU yaani maprofesar sijui wanafikiria nini maana uwezi kumdisco 4thyr so ndio spirit ya kihandisi maana nchi hii wanataka wafahidi wao tu kila sehemu ni ufisadi mpaka ktk elimu nyaoro uwezi lazimisha wahandisi wafikirie kama unavyofikiria mbona wewe mtoto wako amekushinda umempeleka uk huko ni kulewa kwenda mbele kama unathan alikuwa na akili ungemleta hapo coet unapo fundisha wewe nyaoro tunakujua sana si DIT kote roho mbaya utapata malipo hapa2 dunia

Dr. Nyaoro amefundisha wahandisi wote waliosoma UDSM katika kitivo cha uhandisi wa ujenzi na mazingira jengwa tangu enzi, hivyo ni vizuri watu msishabikie mambo, anafahamika kwa misimamo yake katika kutetea haki ya kila mtu. haki ni pamoja na adhabu pindi unapotenda kosa, alichokifanya Nyaoro ni kumtendea haki kijana huyo BABARA baada ya kukamatwa anatafuna karatasi wakati wa mtihani. Binafsi nimekuwa sioni mantiki ya vijana wa COET kugomea masomo kushinikiza kijana huyo kurudi, ila ninachokiona ni wanafunzi hao kujaribu kutumia siasa katika mambo ya msingi. kwa uelewa nilionao vijana hawa watapotea wengi zaidi ya huyo aliyejipoteza mwenyewe kwa kutaka cheating. au mnataka majengo yapolomoke mjini kisha muanzae kupiga makelele mainjinia gani hawa, kumbe ni kina BABARA wanaoangalizia mitihani. narudia tena Dr. Nyaoro ni mtetezi wa haki ya kila mtu wala hawezi kumuonea kijana huyo.
 
Coet wamevuma walichopanda, ona sasa wengine nawaona huku slab wametimuliwa hata kwakwenda hawajui wanabaki wakirandaranda wakidhani labda senate itabadili maamuzi, Bgup kwa mangwini maana coet walijidai wao ndo wao sasa wanakiona.

hayo maneno niliyobold hapo juu yananiboa sana, lakini kwa sasa ndio ukweli wenyewe, sijajua nini kimewakumba wahandisi, hawawezi tena kufikiria sawasawa, kwa sasa wanazidiwa hata na mangwini!!. inabidi walimu wa Engineering wawe wakali zaidi ya hapo. la sivyo kina BABARA watakuja kututia aibu ya kuangusha majengo na kuua watu.
 
Jamani tuache kudakia mada kiushabiki lazima ufuatilie mambo vyema kujua kilichojiri kupata uhakika na utafiti huo ujibu maswali yafuatayo:-

1. Mwanafunzi anaitwa nani?
2. Huyo Mwalimu ni nani? Ameshatajwa kuwa ni Dr. Nyaoro. Ila hawajasema kuwa alikuwa mwenyekiti wa UDASA baada ya Chachage. Ili uwe mwenyekiti wa UDASA lazima uwe mtetezi wa wote wanafunzi na walimu.
3. huyo aliyefukuzwa kafukuzwa, kafukuzishwa au kajifukuza?
4. Huyo Nyaoro anayesemwa ndiye mwalimu wa somo husika au alikua msimamizi wa mtihani? Kiukweli alikua msimamizi.
5. Mwalimu na mwanafunzi wanaugomvi? kama ndiyo ni upi na una uhusiano gani na swala lake?
6. Je huyo mwalimu mwenye miaka zaidi ya Ishirini ya kufundisha chuo amemuonea huyo tu? Anajua mwanafunzi mwenyewe alivyojibu kwenye senate ambayo ndiyo sehemu ambayo mwanafunzi anapata utetezi wa hali ya juu na akiboronga hapo ndiyo basi hata akienda mahakamani hawezi fanikiwa.
7. Kama mwalimu ana ugomvi naye au amemfukuza au amemfukuzisha kama wengi mlivyodai, je yeye ndiye mwenye uamuzi wa kumfukuza mwanafunzi au Baraza bada ya kushauriwa na senate?
8. Unasema hata DIT anawafanyia hivyo je DIT hamna senate?
9. Majuzi walimfuata nyumbani kutaka kumpiga kama binadamu kwa hasira na anahasira na huyo mwanafunzi si angemlipua au kumwita mwizi?
10. Sawa tumeambiwa huyo ndugu ana 3.5 kuwa amefaulu sana ila hatuambiwi out of ngapi, tutajuaje kama alizipata kwa njia ya kucheat ama la na Je tunataka wahandisi wasio na vigezo wenye kujenga miundombinu isiyo kidhi viwango?

Swala la wengine wanaosema mwanae kaenda ulaya kwa kuwa hajui kitu ni sawa kuwa ameelewa hilo na ndiyo maana hakumleta maana mwisho wa siku atacheat au kudisco.

Lingine ni swala la mprofesa kutotaka wenzao wawe maprofesa. Jamani ili mtu awe profesa ni lazima awe amezalisha PhD za kutosha na awe amefanya kazi ya ziada katika Utafiti, Kufundisha na kutoa ushauri wa Kitaaluma sasa akichukia mtu kuwa profesa atampaje PhD? Kingine kwani huyo wa leo ndiyo wa kwanza kufukuzwa chuo akiwa mwaka wa mwisho? Niwape siri mtu wa kwanza kurudia mwaka na kama ingekua utaratibu wa miaka ya 70's angefukuzwa kabisa alikua Arnold Kileo ambaye ni mmoja wa first 14 lakini mwenzie mkenya alidisco kabisa kwahiyo katika kundi la wanafunzi 14 wa mwanzo walihitimu 12 tu.

Sasa niwape uchunguzi wangu na anayebisha abishe kwa uchunguzi na siyo porojo za kuoneana huruma wakati huyo si mwanafunzi wa kwanza kufukuzwa chuo.

1.Tarehe 12 Novemba, 2010, wakati wa mitihani ya marudio (Supplementary Examinations), mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Koleji ya Uhandisi na Teknolojia aitwaye Jamson Babala alikutwa na karatasi, kinyume na taratibu za mitihani. Msimamizi wa mtihani alipomtaka mwanafunzi huyo kumpa karatasi hiyo, mwanfunzi Babala alikataa. Badala yake aliiweka mdomoni na kuimeza. Kufuatana na taratibu za mitihani, msimamizi wa mtihani alimtaka mtahiniwa andike na kutia saini tamko kwenye kijitabu chake cha kujibia maswali kuthibitisha yaliyotokea, na mtahiniwa akafanya hivyo. Kisha akaruhusiwa kuendelea na mtihani wake hadi mwisho, kama taratibu za mitihani zinavyoelekeza.

2.Tarehe 6 Desemba 2010 suala hili la uvunjifu wa taratibu za mitihani lifikishwa katika kikao cha Kamati ya Masomo ya Shahada za awali, yaani Senate Undergraduate Studies Committee, ambapo mtahiniwa Babala pamoja na msimamizi wa mtihani husika na pia msaidizi wake walihojiwa. Katika kikao hicho mtahiniwa Babala alikiri kumeza karatasi ambayo alisema hata hivyo haikuwa na kitu chochote kinachohusiana na mtihani, bali aliikota kutoka sakafuni. Wasimamizi wa mtihani walipohojiwa walieleza kwamba siku ya tukio, kabla ya kuwaruhusu wanafunzi kuingia kwenye chumba cha mtihani, wao walikagua chumba na kuhakikisha kwamba hakukuwa na karatasi au kitu kingine kinachoweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa taratibu za mitihani. Ndipo wakawaruhusu watahiniwa kuingia ndani na kuanza kufanya mtihani. Msimizi mkuu akafafanua zaidi kwa kusema kwamba awali alimwona mtahiniwa akibabaika kama mtu mwenye wasiwasi. Ndipo alipomhamisha kwenda kwenye dawati linguine. Lakini wakati anapita kuangalia vitambulisho vya watahiniwa kwa uthibitisho kwamba watahiniwa wote walikuwa halali, alimkuta mtahiniwa Babala na karatasi, ambayo alikuwa amieficha kwenye kitabu cha kujibia masomo. Alipotaka kuikagua karatasi hiyo ndipo mtahiniwa akiitia mdomoni na kuimeza. Kutokana na majibu ya mtahiniwa na ushahidi wa watahiniwa wawili, Kamati iliona mtahiniwa ana hatia na hivyo ikiapendekeza kwa Seneti aachishwe masomo, kadiri ya maelekezo ya kanuni za mitihani.

3.Pendekezo la kumwachisha masomo mwanafunzi Babala lilifikishwa katika kikao cha Seneti ya Chuo, kilichofanyika tarehe 15 Decemba 2010. Baada kulijadili suala hili kwa kina, Seneti ya Chuo ilikubaliana na pendekezo hilo na hivyo kupitisha uamuzi wa kumwachisha masomo Jamson Babala. Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lifahamishwa kuhusu uamuzi huo katika kikao chake kilichofanyika tarehe 27 Januari 2011 na likaridhia.

4.Kufuatia uamuzi wa Seneti, tarehe 17 Januari Jamson Babala alimwandikia barua Makamu Mkuu wa Chuo akiomba radhi kwa yaliyotokea na kusihi kwamba adhabu yake ipunguzwe kwa kuwa yeye sasa ni mwanafuni wa mwaka wa nne na kwamba wastani wa matokeo yake ya mithihani iliyopita ni wa kuridhisha. Kwa kuzingatia kanuni za mitihani na sheria nyinginezo, ombi hilo halikukubaliwa. Hivyo Jamson Babala akawa si mwanafunzi tena wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

5.Katika matukio yasiyotegemewa, kuanzia tarehe 4 Februari mwaka 2011 kikundi cha wanafunzi wa Koleji ya Uhandisi na Teknolojia wamekuwa wakivuruga madarasa na kuwatisha wahadhiri, wakishinikiza Jamson Babala arudishwe chuoni. Licha ya Mkuu wa Koleji kuongea na wanafunzi hao kuwaelimisha kuhusu hali iliyosabisha Babala kuachishwa masomo, na hata baada ya Makamu Mkuu wa Chuo kukutana nao tarehe 8 Februari 2011, wanafunzi hao wameendelea kuvuruga masomo na kuhatarisha usalama wa watu na mali katika Koleji ya Uhandisi na Teknolojia.

6.Suala hilo lilijadiliwa katika kikao cha dharura cha Baraza la Chuo kilichafanyika jana tarehe 8 mwezi Februari, 2011. Baraza liliagiza kwamba ikiwa vurugu zinazoendela hazitasitishwa masomo ya shahada za kwanza katika Koleji ya Uhandisi na Teknolojia yasimamishwe na wanafunzi husika waondolewe chuoni.

7.Kutokana na kuendelea kupamba moto kwa vurugu katika Koleji ya Uhandisi na Teknolojia, leo tarehe 9 Februari Chuo kimechukua uamuzi wa kutekeleza maelekezo ya Baraza la Chuo la kusimamisha masomo ya shahada za kwanza katika Koleji ya Uhandisi na Teknolojia na kuwaondoa wanafunzi husika chuoni.

Ingekua mimi ningekataa katakata kutenda kosa mwanzo mwisho hata nidanganywe vipi. Maana naskia jamaa alidanganywa na wenzie eti ukikubali kosa ndiyo utasamehewa wakati mambo yameshatinga senate yeye angekuabaliana na mambo kwenye college level kama amekana kutenda kosa mwanzo angekana mpaka mwisho.

Nwasilisha bila chenga.

Huo ndio ukweli. umetoa majibu mazito kwa maswali mepesi
 
@Jitihada. Yap hiyo hali hata mimi yamenikuta jtatu, niliingia vizuri kwenye cafe yao. Ila kutoka ikawa ishu, ikabidi nipite geti dogo la kule uwanjani. Ila wanaofanya hayo ni wapumbavu wachachE kwa jina la CoET! SOLIDARITY FOREVER!

asante kwa kunisoma mphamvu, nami pia naamini sio coet wote wenye matatizo bali haohao wachache hasa maboys ndo wasumbufu. Naongea kwa machungu maana binafsi naishi kitaa(yaan mtaani) sasa nna kawaida ya kukatiza coet kila asubui nnapokuja chuo, kitendo walichonifanyia leo hao wana coet, yaan nimepita vizuri kuanzia geti maji hadi nkafika geti la kutokea kuanza kuingia hyo njia inayo panda hadi FoL, huwez amin vidume vimenkomalia hakuna kulivuka geti ila nirudi nkazunguke ground au nizungukie road hadi UCC, binafsi iliniuma sana ukizingatia nimetembea toka geto hadi chuo sababu ya kuishiwa boom. Ikabidi kidume nkubali kuzunguka ground huku akina dada baadh wakisikitika kwa jinsi nlivyoonewa, ona sasa coet hawapo na amani imerudi na nnakatiza huku coet kurud zangu kitaa bila usumbufu. SOLIDARITY MANGWINI,,,,
 
Jitihada, nziriye nina wasiwasi na uwezo wenu wa elimu. Kwenye hili ni kama mna chuki binafsi na CoET. Mini ni mwanafunzi wa IKR, mchongo mzima naupata, na fitna za Nyaoro hata wahandisi wakongwe wanazijua, ni muda wa kuondoa watu wa namna hii hata kwa kuwapa vilema vya maisha. Inauma dudes, serikali itukandamize, hata sisi kwa sisi jamani. Hebu jiweke kwenye nafasi ya Mbabara afu ufikirie inakuwa aje?

Stop it please!! acha politics, nimesoma coet ikiwa bado inaitwa foe ikabadilika ikawa pcet, namfahamu Nyaoro na amenifundisha, kwa suala la BABARA engineering hamjatumia thinking yenu ya 3-D, kwa kifupi mmetumia matope na hayo matope hayatawafikisha popote zaidi ya kuwapoteza wengi zaidi kwa kutetea ufisadi wa elimu. mnachotetea ni ufisadi wa elimu, engineer hawezi kukamatwa anaangalizia mlazimishe arudishwe kwa kumtoa sadaka Dr. Nyaoro, ingekuwa hata vyema Civil wote mfukuzwe kuliko kumtoa Dr. Nyaoro. tena nimewasikia kwa masikio yangu mkimwambia ameeingia choo cha kike, (HAMNA ADABU KABISA) kwa taarifa yenu nyinyi ndio mmeingia choo cha kike tena mmekutana na mama mkwe chooni.
 
Back
Top Bottom