Hatimaye Academy yaanza taratibu za kumchukulia Will Smith hatua za kinidhamu

Kosa sio kumpiga kofi, kosa ni kumpiga kofi hadharani tena stejini.

Sikubaliani na kitendo cha kushambulia na vile vile sikubaliani ni Chris Rock kumtania Jada ilhali ni mgonjwa.
Kwan rock alikua anamdhalilisha na kumsimanga jada sirini au hadharani? Bas na kofi alipewa hapo hapo.

Kwanza ilibidi amkate mtama aanguke chini avunjike uti wa mgongo msieeeew zake.
 
Ulikua hujui kama Binaadam ni kundi la Wanyama,
Hao Mabwana zako unaowatukuza unawaitaje huko Urusi na Ukraine???

Huyo unaemuona mwamba hivi sasa yupo kwenye kutilisha huruma tu, Kama alichokifanya ni sahihi asingekuwa anaomba radhi. Amejiadhirisha na kuonekana pimbi, na kumzidizishia umaarufu mwenziwe.
 
Wabongo mshazoea kupigana, mnapigwa kuanzia nyumbani kwa wazazi na walimu shuleni…. hivyo mnaona lile kofi kwanza halitoshi.

Wenzenu hawapo huko, na wala hizo opinion zenu haziafekti chochote maamuzi yao kisheria.
 
Kwan rock alikua anamdhalilisha na kumsimanga jada sirini au hadharani? Bas na kofi alipewa hapo hapo.

Kwanza ilibidi amkate mtama aanguke chini avunjike uti wa mgongo msieeeew zake.
Mmmh kamsimanga na kumdhalilisha kivipi? Na kwan alikua anajua jada ni mgonjwa?
Kwani chris hajadhalilishwa kupigwa kofi hadharani?
 
Wabongo mshazoea kupigana, mnapigwa kuanzia nyumbani kwa wazazi na walimu shuleni…. hivyo mnaona lile kofi kwanza halitoshi.

Wenzenu hawapo huko, na wala hizo opinion zenu haziafekti chochote maamuzi yao kisheria.
Wenzety hata watoto wanaenda shitaki kama wamepigwa na wazaz wao
 
Ila wazungu wamejua kuing’ang’ania Hii ishu,,,walianza kumshawishi Chris kwenye mitandao amfungulie mashtaka ila aligoma,,,jamaa alijidai kulia ili aonewe huruma haha ila kamfanya mwenzake ajaze uwanja Kwenye tours zake!
 
Wengi hawajaulewa utani wa Chriss. Ji jane ni movie inayomuelezea mwanamke aliyekuwa anakatishwa tamaa na jamii kumwekea vikwazo kutokana na imani kwamba atafeli mazoezi magumu ya kikosi maalumu cha jeshi alichojiunga nacho. Ji Jane alipambana kufa na kupona mpaka akanyoq nywele zake na akatoboa akawafunga midomo.

Issue hii inareflect kwa Jada kutokana na ugonjwa alokua nao na wakati mgumu anaopitia. Chriss alimpa moyo na kumfananisha na JI Jane akimaanisha kwamba mbali na changamoto za maradhi anazopitia, atashinda na atafaulu. Hivyo maana ya JI Jane 2 ndio hiyo aliyomaanisha Chriss.

Will alikurupuka na hatua ya kumpiga mwenzio kofi hadarani tena kwenye stage maarufu inayotazamwa na mabilion ya watu ulimwenguni haifai hata kama kakukosea vipi na ukizingatia Chriss ni comedian by profdession. Hili ndilo lilomfanya Will aombe samahani ila baya zaidi ni kukataa kutoka ukumbini baada ya kuamriwa na uongozi kwa kufanya tukio la aibu.

Kuhusu suala la tuzo, angepewq tu kwa masababu matokeo hayapangwi pale. Ilikua halali yake kwa sababu alishashinda pale ilikua kutangazwa tu.

HII NI KWA MUJIBU WA UELEWA WANGU
 
Unawaza kupukutishwa pesa kuliko kumdefend Mkeo???

Ukishakua ukawa na Familia ndio utaelewa "how to protect your family and family comes first".
Duuh kumdifendi mkewe Kweli?

Willy ni Boya tu amechanganyikiwa kwa mkewe, ndoa imekwisha mshinda Jada anamegwa na kutanua na vibenten mchana kweupee Halafu Masikiij ya Mungu Willy anakuja kufanya ujinga mbele ya hadhara kujaribu kumridhisha mkewe ana mjali

Lakini ndio hivyo tena
 
Wajinga hao,

Hata wakimpokonya hicho kituzo chao Will bado atabaki kua Muigizaji bora of all the time na Dunia itamkumbuka kama Mume aliyemtetea Mke wake katika kudhalilishwa.

Will Smith angekuwa bongo tungesema yule mwananmke kamlisha limbwata; itakuaje leo hivi yule mwanamke amtamkie mum ewe kuwa alikuwa anatembea nje na mumewe anamchekea tu? Kila mtu anamshangaa Jinsi Will Smith anavyotendewa na huyo mwana mama!! Mwanaume wa Nguvu amemfanya aonekana kama hanithi!!!
 
Back
Top Bottom