Hatimae mpambano wa CCM na Mh Lowasa umewadia.

Hatimae mpambano wa CCM na Mh Lowasa umewadia.

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
1,911
Reaction score
1,320
Kama alivyoimba Mwana dada na nguli wa muziki wa bongo fleva Judith Wambura,"Siku hazigandi ". Ule mpambano wa kukata na shoka kati ya CCM na Mh Lowasa umewadia. Kila upande kwa nafasi yake umekuwa ama ukikwepa au ukisita kuingia katika mpambano. Mara ya kwanza ilikuwa ni kwenye bunge la jamhuri pale" caucus "ya chama ilipokubali ripoti ya Richmond kujadili bungeni. Mh Lowasa alipopewa nafasi ya kujitetea bungeni aliahilisha mpambano kwa kuamua kujiuzuru Uwaziri mkuu. Wengi turidhani kwa kuwa wao walimwaga mboga basi yeye angemwaga ugali. Mara ya pili ni pale ripoti ya ndg Mkama ambae alikuja kuwa katibu mkuu wa CCM iliposema chama kimepoteza mvuto kwa kuwakumbatia mafisadi. Ili kujisafisha ilibidi kujivua gamba na mmoja wa waliotakiwa kujivua alikuwa Mh Lowasa. Hata hivyo kujivua gamba kulimalizika huku CCM na Mh Lowasa kila mmoja akionekana kumkwepa mwenzake. Mara ya Tatu ilikuwa ni hatua ya chama kuwasimamisha makada wake kujihusisha na siasa kwa miezi 12 (Mh Lowasa alikuwa miongoni mwa waliosimamishwa)). Miezi 12 iliisha na mpambano ukawa umeahirishwa. Safari hii Mh Lowasa akiwa anajipambanua (kwa kauli na matendo yake) kama mgombea bora na mwenye mvuto kuwazidi wenzake ndani ya CCM, Chama kinasisitiza hakiwezi kusimamisha "mgombea mwenye kumwosha kwa dodoki". Mpambano huu umekuwa ukiahirishwa lakini safari hii lazima ufanyike. Huku Chama kule Mh Lowasa (na team yake). Sijui nani atashinda.
 
Kwakweli kazi ipo maana ameshasema hategemei kushindwa,wala hafikirii kukatwa jina kwa kauli hizi jamaa hatakubali jina lake likatwe!
 
Kwakweli kazi ipo maana ameshasema hategemei kushindwa,wala hafikirii kukatwa jina kwa kauli hizi jamaa hatakubali jina lake likatwe na kikao chochote cha chama!
 
Tafadhali Meridian Bet Ingizeni Hii Mechi Kwenye Systems Zenu Watu Tupo Tayar Kwa Betting
 
Ili kujua ni chama gani hiki cha siasa, lazima herufi zote 3 zionekane kwenye chama cha mapinduzi, yaani ccm. Ukiondoa herufi moja tu hapo, hiyo sio ccm.
Sasa basi, CCM bila Lowasa, sio ccm. CCM ni Lowasa na Lowasa ndiye CCM. Huwezi kumwondoa Lowasa CCM ipone, na huwezi kuiondoa CCM Lowasa apone.
Walimlea wenyewe, akala kile kiini cha ccm. Hivyo, hawatakaa waweze tena kumng'oa. Labda ajiondoe mwenyewe. Wamesha chelewaaaaaaa:llama::llama:
 
Kwakweli kazi ipo maana ameshasema hategemei kushindwa,wala hafikirii kukatwa jina kwa kauli hizi jamaa hatakubali jina lake likatwe na kikao chochote cha chama!
Huyu fisadi asitishe watu, kama alikuwa na uhakika wa kutokatwa na kikao chochote asingekuwa na haja ya kujaza form, bali angejitangazia urais moja kwa moja
 
Hii habari ina uhusiano gani na MMU?
 
Ccm hata waweke jiwe wanashinda maana wana wapambe ambao huwezi kuwaambia kitu xo lowasa anaweza akatoswa na atakayesimama akashinda tu
 
Lowassa ni Kama kaa la moto ndani ya ccm, kilitema shida kulimeza balaaa ...

Huyu mtu anatakiwa apewe nchi tu awanyooshe kina Nape
 
Mbona kama hii kitu imepotea njia au mods wamelala?
 
Kusema Lowassa vs CCM sijui unamaanisha nini wakati 75%ya wanachama na wajumbe wa vikao muhimu vya Ccm wanamkubal?
 
Edo Edo Edo kila kukicha...........sijui hata kwanni nimechangia hapa huu. U.pu.pu
 
Kusema Lowassa vs CCM sijui unamaanisha nini wakati 75%ya wanachama na wajumbe wa vikao muhimu vya Ccm wanamkubal?
Nadhani CCM huijui vzr, jitahidini kusoma historia ya chama. Kwani Karume mdogo wakati anapewa fursa ya kugombea alikuwa amekubaliwa na wajumbe wa vikao. Mzee Malesela wakati jina lilipokatwa wajumbe walikuwa hawamuungi mkono?
 
Nadhani CCM huijui vzr, jitahidini kusoma historia ya chama. Kwani Karume mdogo wakati anapewa fursa ya kugombea alikuwa amekubaliwa na wajumbe wa vikao. Mzee Malesela wakati jina lilipokatwa wajumbe walikuwa hawamuungi mkono?

Kama Mimi siijui CCm basi ni sawa na kusema CCM haijulikani, Unapozungumzia CCM kwa uelewa wako ni nini? Sema hakubali kwa baadhi viongozi wajuu wa CCM sio kuwa hakubaliki na wana CCM, umetumia mifano ya Karume na Malecela mi naongezea Jk hakukubalika kwa viongozi wa juu wa CCm I.e Mkapa, Mangula na Malecela mwaka 2005 lakini ndio Mwenykt na Rais wa Nchi
 
Mpambano huu sio wa ndani ya chama tuu' hata nje ya chama kazi itakuwepo. Ana ushawishi kwa wagombea wengi wa nafasi za ubunge na Udiwani ndani ya ccm' anaweza kukatwa na kukaa kimya lakini watu wake wakishinda kwenye uchaguzi kuna hati hati ya kuwa wanakwamisha mambo mengi ya serikali kwa makusudi na dhamira ovu
 
Hamna kitu kama hicho, ofcoz wazalendo tunaback up chama hata sie ambao uko Ukawa, mwanachama hawezi kuota pembe akawa zaidi ya chama hata ZZK alikwenda hivyo na mwishowe alipewa stahiki yake
 
Mpambano gani.? Mbona kilakitu kiko wazi na mteremko kabisa.

Kama ulovo msalaba kwa Wakristo. .. kama ulivyo Mwezi kwa Waislamu. Edo ni Ufisadi kwa CCM.

Kwa kuwa CCM haiko tayari kujimaliza yenyewe kwa kuwa extinction kwenye mazingira ni mchakato usiozuilika kibinadamu na kwa kuwa Ufisadi umefikia mahali unabidi uingie kwenye extinction process ... Niambie kuwa ugumu uko wapi hapo.

Wala hakuna mijinguvu mingi inayohitajika ..!

Uzao mpya wa Uongozi ndani ya Tanzania uko Tayari.
 
Back
Top Bottom