Hatimae Mastering studio kurudi BASATA

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
1,467
513
Nichukue fursa hii kumpongeza Mh. makala, baada ya Sugu kukomaa na hii studio iliyotolewa na Rais kwa kikundi cha fleva unit kupelekwa baraza la sanaa ili kuwanufaisha wanamuziki wote serikali kupitia kwa naibu waziri huyu imekiri kuwa itabidi wamshauri rais airudishe basata. Kuonyesha hiki kikundi kuomba studio hiyo pia waliomba walipiwe kodi ya pango ya studio, Rais akatoa mil 9, jamaa wakaomba hela ya ukarabati na ya mtaalam. kodi imeisha wanaomba tena walipiwe du? kwahiyo yale majibu mepesi waliyokuwa wakimjibu sugu kuwa walioomba ndo waliopewa ina maana hawakujua haya? mbona ilikuwa wazi? Mi sikumwamini kabisa Mh alipoteuliwa ila kwa hili nakuona umethubutu. Hongera
 
Wale clouds wanaandaa hadi birthday ya rais. nafikiri ndo maana wakapewa. na ile THT nayo inabidi irude basata. hili ni pigo kwa ruge.
 
kikundi kilichoundwa na baadhi ya wasanii wa bongo fleva, walimface JK wakaomba studio ya kuboresha nyimbo, wakakisajili kikundi kama kampuni wakapewa. wasanii wengine wakalalamika through Sugu bungeni kwa kama 3 years, walijibiwa several times waliiomba ndo waliopewa. Hatimeye leo kwenye majibu baada ya budget ya wizara husika wamekubali irudishwe serikalini yani BASATA. Imeongelewa sana hii issue mkuu!
 
kiasi umenifumbua macho mkuu,kipindi cha bunge nilikuwa naangalia simba anavyofungwa
 
Hongera Mh SUGU!
Sasa Mh Sugu anzisha na hili la mashirika ya hifadhi (PPF, NSSF, PSPF, LAPF, GEPF) kushikilia pesa zetu eti hadi tufikishe miaka 55 au 60!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom