Hatimae; Jeetu Patel akiri kumiliki kampuni iliyochota fedha za EPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimae; Jeetu Patel akiri kumiliki kampuni iliyochota fedha za EPA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 29, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,766
  Trophy Points: 280
  Jeetu Patel akiri kumiliki kampuni iliyochota fedha za EPANa Nora Damian

  WAFANYABIASHA Jayant Kumar maarufu kama Jeetu Patel na Devendra Patel ,wamekiri mahakamani kuwa Kampuni ya Bencon Internatinal Limited, inayodaiwa kujipatia fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni ya kwao.

  Wafanyabiashara hao walikiri hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati walipokuwa wakisomewa maelezo ya awali ya kesi yao.

  Maelezo hayo yalisomwa na wakili wa serikali, Timon Vitalis, mbele ya jopo la mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Ruwaich Meela, Grace Mwakipesile na John Kahyoza.

  Washtakiwa hao walikiri kuwa wao ni kati ya wakurugenzi wa kampuni hiyo iliyoanzishwa hapa nchini Aprili 4 mwaka 2005.

  Pia Jeetu Patel na mshtakiwa mwingine Amit Nandy, walikubali kuwa kampuni hiyo ilianzishwa nchini Aprili 4 mwaka 2005 na kwamba wao ndio waliokwenda kufungua akaunti benki.

  Maelezo mengine yalisomwa, lakini yakakataliwa na ni ya kughushi hati za uhamishaji deni kati ya kampuni yao na kampuni za Matshusta na Marubeni za Japan.

  Wakili wa serikali Vitalis alidai kuwa kati ya Agosti 12 na Septemba mosi mwaka 2005, mshtakiwa Nandy aligushi hati ya uhamishaji deni la Sh 2,599,944,458.12 kuonyesha kuwa kampuni yao imepewa deni na kampuni ya Matshusta ya Japan.

  Alidai kuwa kati ya Oktoba 18 na Novemba 2 mwaka 2005 Nandy alighushi hati nyingine akionyesha kwamba kampuni yao, imepewa deni la Sh 7,962,978,372.48 na kampuni ya Marubeni ya Japan.

  Pia alidai kuwa mshtakiwa huyo ni Mkurugenzi wa fedha wa kampuni ya Bencon International Limited.

  Upande wa mashtaka ulidai kuwa kutakuwa na mashahidi 18 watakaotoa ushahidi katika kesi hiyo. Baada ya kusikiliza hoja zote Mwenyekiti wa jopo la mahakimu wanaosikiliza kesi hiyo, Hakimu Meela aliahirisha kesi hiyo hadi itakapoanza kusikilizwa Agosti 3 hadi 14 mwaka huu.
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Breaking NEWS? You must be kidding!!!
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  this is obvious
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,195
  Trophy Points: 280
  Didy hakuna jipya hapa lakini hakuna wa kumgusa maana anajua uchafu uliofanyika katika kampeni za kuwania Urais 2005 uliofanywa na wana mtandao. Wanajua fika wakimgusa tu jamaa anaweza kutoa data zote maana wahindi hawa wameshajizatiti na ni wazuri mno kwa kuweka kumbukumbu, sasa hivi wakiguswa tu basi kutakuwa na patashika nguo kuchanika.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,766
  Trophy Points: 280
  Yaani hiiiiii nchi we acha tuuuuuuuuuuuuuuuu mungu pekee

  nasikia jakaya anaifwatilia hiiiii kesi kwa udi na uvumba na ole wake hakimu atakae wawashia mooto cha moto atakiona...mnamkumbuka mwankenja.....alianza na moto we.anajua alichoambiwa

  kweli wa madhabahuni ale madhabahuni
   
 6. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ebanaeee

  aliambiwaje?
   
 7. J

  Jafar JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Yaaani hii ni OVIASI, hakuna jipya na wala si breaking nyuzi. Kesi hii inaweza kufika 2014 na kuonekana hawana hatia.
   
 8. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  enhee! hapo patamu babaa! cjui kama hili litawezekana iwapo mmiliki kitanzi anaweza kujinyonga, bt kama ni ndotoni na ardhi nyingine tofauti na hii basi itawezekana! tulilazwa na nusu kaputi watanzania, tunaamshwa na wezi walewale walotupiga nusu kaputi je inawezekana kuwahisi wao ndo chanzo cha ucngizi we2, ni ngumu hiyo wakubwa 2jipange kivingine, kwani iliyo tamu ndimini itaendelea kulambwa! watadhalilika siku moja tuwepo au wawepo we2 sie!
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,766
  Trophy Points: 280
  ilichobaki ni watanznaia kujipanga upya na kuangalia wapi walipokula kihalali wapi wasipostahili kupagusa then tudumbukie wote humo........
  hakimu mwankenja alikuwa shujaa sana alipogusa mboni ya jicho kidogo .......
  tteeennette mete
   
 10. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  asante kwa habari hii nadhani wakati umewadia sasa kwa 'wahusika' kuwaendea wote wenye hela za BoT na walio na hela za NBC mimi nimesema ni watanzania wachache mno wenye hela ya halali ya kupita. embu tu jiulize wanazitoa wapi iwapo miradi yenyewe aizunguki hata dar-es-salaam nzima let alone the whole country yet unakuta mtu ana maisha utadhani yuko mbinguni ukilinganisha na mlalahoi.

  i dont want to sound like a socialist, because im all for capitalist lakini hii function on the basis of a capital society tunaua nchi kuwapa hela watu ambao hawa invest back. mi ni kijana wa kitanzania (mwafrika) nina rafiki yangu yuko huko bongo mwenye asili ya kimanga ni best wangu siwapi jina. jamaa alikuja mwaka juzi kununua magari yake ya biashara (ma-lorry) ana umri kama wangu early 30's tayari ameshapewa mkopo wa millioni mia nane. hapo hapo baba yake ni tajiri tayari kitu cha kwanza baada ya kupewa mkopo baba alipewa VX mpya na mama akalalamikaa akapewa na yeye ya kwake mpya. Yaani awana nia ya kulipa na ni wengi mno ambao wanafanya michezo hii.

  kama uko nje ya tanzania au hata waliopo tanznania ni wadosi wangapi au wamanga wangapi unawaona mlimani. ukija ulaya wadosi wakitanzania wanaosoma huku hawarudi wakisha pata elimu yao. wamanga wanaoenda shule kwa kweli ni wachache wao kuoana tu ndio walichoweka mbele. alafu ukirudi unakuta wao ndio wenye hela eti wanakipaji cha biashara what a stupid explantion. ni hela hizo za benki ndio zinawapa head start kibaya in most cases azilipwi zote. i have been saying this for sometime but people dont want to see what is obvious.

  tunarudi tena unakuta watu design ya 'EL' wanasapoti vitu hivi on a greater scale kiasi ambacho hiyo hela ingewasaidia watu wengi mno. hivi mnajua kuna watu tanzania hata kuwasha hii computer awajui. kuna watu wanaishi pembeni ya madibwi ya maji machafu, kuna ma albino wanauliwa polisi wanashidwa kuwa protect, kuna watu wana amka awajui leo mlo unatoka wapi, kuna watoto yatima wanajilisha wenyewe na mengineo mengi utakayo yafikiria ya kimaskini wakati hapo juu hela inayotajwa kuisoma nimeona tabu.

  tatizo sio hawa wezi wa kihindi wala wa kimanga kwa sababu kuna waafrica pia wengi tu, tatizo ni watu mnao watetea EL sio mwana siasa jamaa ni mwizi na inabidi atolewe kabisa kwani hana mapenzi na Tanzania inaeleweka Monduli watafunga macho kwa sababu ni wa kwao lakini Tanzania si Monduli kwanza iko nje kabisa ya Arusha. its time to look on the perspective of the whole rather concentrate on individual tunao wasomi wengi mno at the moment nje na ndani ya nchi things have to change tatizo sio Jeetu Patel and co tatizo ni tabia za viongozi wetu hawana mapenzi LONG LIVE TANZANIA
   
  Last edited: May 29, 2009
 11. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Tanzania kuna watu wa aina mbili tu. Wanaotengeneza mavumbi na wanaokula mavumbi.
   
 12. K

  Kachero JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli kama hali halisi ndio hii tunakazi kubwa ya kufanya Tanzania ili matunda ya uhuru yawe kwa faida ya wengi na sio mafisadi wachache kama ilivyo sasa.
   
 13. K

  Kachero JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani Tanzania kama vile tumeleweshwa na hatujijui tunakoelekea,watu wanakuja kutoka huko nje hawana kitu.Wanatuibia tena kimachomacho huku wakisaidiwa na vibaraka wachache na sisi tunakodoa macho tuu,hivi kweli sisi watanzania wazima?

  Hata kama JK anafuatuilia hapa hatoki mtu,wametudanganya,wametuibia,sasa tumeamka wa watanzania wa leo sio wa jana, ni ama zao mafisadi ama zetu, hatoki mtu hapa.
   
Loading...