Hatimae amepatikana nyonga mkalia ini na mahabuba wangu

mcrounmj

JF-Expert Member
Feb 26, 2016
380
885
Habari zenu wakuu. Nimewiwa kuwasimilia safari yangu ya mahusiano hatimae kuja kumpata aliyesubiriwa kwa miongo kuwa Mrs A.

Mimi ni aina ya wale vijana wa kiume wanaoamini kwenye kujitafuta kwanza kiuchumi kabla ya kuingia kwenye majukumu ya familia. Ninazo ndoto za kuwa na familia bora, watoto na mke mzuri. Nikiri tu kuwa falsafa hii nimeishi nayo kwa miaka sasa....toka nikiwa chuoni, sikutaka kuingia kwenye mtego huu wa kujikuta naoa kwa bahati mbaya.

Kama binadamu wengine, mimi pia ni mkware ninayetongoza na kuingia kwenye mahusiano. Nimepitia mahusiano tofauti tofauti, nikiwa na tahadhali kubwa ya kutompa mwanamke yeyote mimba. Wazo hili nilililaani vibaya mnoo kwani sikutaka kuwa na watoto wa nje ya ndoa. Hivyo nilihakikisha hakuna mahusiano ambayo yangezaa ujauzito licha ya kwamba tulikuwa tunavunja amri ya sita.

Safari ya mafanikio siyo nyepesi kama ambavyo huwa tunafikiri. Katika namna ya kuwaza na kupanga, kuna tofauti kubwa mno ukienda kwenye uhalisia. Muda mwingine tunawaza makubwa kwenye maisha lakini tunapokea robo au kuduchu mnoo. Katika hali yoyote ya upambanaji, zipo changamoto nyingi ambazo wakati wa kuwaza na kupanga huwa hatuzizingatii lakini hujitokeza wakati wa utendaji.

Katika namna ambayo niliamini ningeweza kutoboa ndani ya mwaka au miaka miwili, it was impossible. Changamoto ziliibuka na kunirudisha chini. Miaka ilisogea. Hata wale niliowapa matumaini ya kuwaoa wanivumilie kwa muda, walichoka kunisubiri na kuamua kuolewa kwingine. In short, life was so tight and there was no hope.

Jambo moja niseme, katika vitu ambavyo huwa naviona ni kama neema kwangu ni kuwa, huwa sikati tamaa na nikikosa leo naamini kesho ninayo nafasi ya kujaribu bahati nyingine. Hii nai dedicate kwa wote wanaopambana lakini bado hakijaeleweka. Waamini kesho pia ni yao. Guys, don't give up.

Nilifanya kazi kama punda. Nilijituma, ilifika wakati nikaweka professional yangu kabatini. Nilifanya kazi yoyote ya halali. Hatimae niliibukia migodini ambako nako nilijituma kupita maelezo. Ikumbukwe kuwa baada ya kumaliza chuo ndipo maisha yalianza kwenda kombo kiuchumi na kupelekea hata kuachwa na aliyekuwa mpenzi wangu wa kipindi hicho.

Safari yangu ya migodini ilikuwa na neema. Kutoka kuwa mfanyakazi anayeshuka maduarani chini ya ardhi zaidi ya mita mia moja, mpaka kuwa mmliki wa mgodi, siyo kazi ndogo. Hii ni story ya siku nyingine, ila tu nimegusia hiki ili kuonyesha kuwa kutoka kuwa kibarua wa chini kabisa inawezekana siku moja ukaketi meza moja na wafalme.

Baada ya hali yangu kuimarika kiuchumi, kasheshe ilikuwa kumpata the ideal woman, mwanamke wa ndoto zangu. Ikumbukwe kuwa mademu zangu wa chuo wote kwa nyakati tofauti walinitema. Because of too much expectations ambazo zilikuwa hazitimii. Sasa nikiwa niko poa kiuchumi sikuwa na demu tena wa kuja kumuoa.

Wapo wanawake ambao nilikutana nao. It was hit and run! Kwa sababu hawakufika vigezo vya mwanamke niliyetaka awe mke wangu. Nilitumia mitandao ya kijamii kumsaka huyo an ideal woman. Jamii forum pia nimeweka mabandiko mara kadhaa kutangaza nia ya kuopoa jiko. Nikiri tu kuwa, wanawake niliowapata kupitia jukwaa hili, hawakuwa na vigezo nilivyovitaka. I did this several times with no good results.

Nikiwa desperate, sijui nimuoe yupi, nikijaribu karata yangu kwenye kila engo ya mitandao ya kijamii, Hatimae nimekuja kukutana na an ideal woman, mwanamke wa ndoto zangu FACEBOOK. Yes Facebook imenipa mke. Mwanamke niliyemngoja kwa zaidi ya miaka tisa sasa hatimae nimekuja kukutana nae Facebook. Naiamini mitandao ya kijamii ila siyo facebook. Facebook ni ya washamba, watu wa kijijini, watu wa mjini wanapatikana huko mjini Instagram, jamii forum na Twitter hukoo. Lakini huku Facebook, mmmmh!!

Wakuu nikisema an ideal woman nadhani mnaelewa. Jina anaitwa Alice (siyo jina lake halisi). Alice is beautiful, smart, disciplined and intelligent. Chenyewe anadai kwa muumba ni msambwanda tu ndiyo hajabalikiwa. Kitu kizuri zaidi, mimi mwenyewe siyo mtu wa kupenda vishundundu, hivyo is like Alice ameumbwa kama order yangu. Tangu nimekutana nae maisha yangu yameongeza value.

Wapendwa wanawake wazuri wa tabia bado wapo. Alice ni mmoja wao. She is a wife material. Tangu nimemuoa nyumba yangu imekuwa safi. Vitu vimepangwa kwenye mpangilio, nguo zangu, za kwake, vyombo vya ndani. Kiujumla mwonekano wa pale ndani unavutia. She is happy all the time, yaani tunaishi kwa amani. Siku sijaenda kazini nashinda tu ndani na my baby, she is so sweet.

Nyie asikwambie mtu, mpendane harafu pesa ipo, Mnaanzaje kuchokana. Aliyekwambia pesa siyo kila kitu kwenye mapenzi alikudanganya. Tafuta pesa ili ufurahie maisha ukiwa na umpendaye kwenye mitaa ya Juliana, Element na Samaki Samaki. Au msafiri kwenda kula raha za duniani huko Ibiza ama Dubai. About love, money is everything.

Sasa Alice ni mjamzito na nimemfungulia duka. Nimeamua ku share hapa ili kuwa inspire wale ambao wako block na mapenzi. Sijaandika kwa ajili ya kujikweza ila ni namna ya kuwafanya wengine wajifunze na kuchukulia changamoto walizo nazo ni za muda. Pia kuwafanya wadada wengi kuwa akina Alice. Cha mwisho naweza kusema love is an art, you can create it rough or smart.
 
Habari zenu wakuu. Nimewiwa kuwasimilia safari yangu ya mahusiano hatimae kuja kumpata aliyesubiriwa kwa miongo kuwa Mrs A.

Mimi ni aina ya wale vijana wa kiume wanaoamini kwenye kujitafuta kwanza kiuchumi kabla ya kuingia kwenye majukumu ya familia. Ninazo ndoto za kuwa na familia bora, watoto na mke mzuri. Nikiri tu kuwa falsafa hii nimeishi nayo kwa miaka sasa....toka nikiwa chuoni, sikutaka kuingia kwenye mtego huu wa kujikuta naoa kwa bahati mbaya.

Kama binadamu wengine, mimi pia ni mkware ninayetongoza na kuingia kwenye mahusiano. Nimepitia mahusiano tofauti tofauti, nikiwa na tahadhali kubwa ya kutompa mwanamke yeyote mimba. Hili nililaani vibaya mnoo kwani sikutaka kuwa na watoto wa nje ya ndoa. Hivyo nilihakikisha hakuna mahusiano ambayo yangezaa ujauzito licha ya kwamba tulikuwa tunavunja amri ya sita.

Safari ya mafanikio siyo nyepesi kama ambavyo huwa tunafikiri. Katika namna ya kuwaza na kupanga, kuna tofauti kubwa mno ukienda kwenye uhalisia. Muda mwingine tunawaza makubwa kwenye maisha lakini tunapokea robo au kuduchu mnoo. Katika hali yoyote ya upambanaji, zipo changamoto nyingi ambazo wakati wa kuwaza na kupanga huwa hatuzizingatii lakini hujitokeza wakati wa utendaji.

Katika namna ambayo niliamini ningeweza kutoboa ndani ya mwaka au miaka miwili, it was impossible. Changamoto ziliibuka na kunirudisha chini. Miaka ilisogea. Hata wale niliowapa matumaini ya kuwaoa wanivumilie kwa muda, walichoka kunisubiri na kuamua kuolewa kwingine. In short, life was so tight and there was no hope.

Jambo moja niseme, katika vitu ambavyo huwa naviona ni kama neema kwangu ni kuwa, huwa sikati tamaa na nikikosa leo naamini kesho ninayo nafasi ya kujaribu bahati nyingine. Hii nai dedicate kwa wote wanaopambana lakini bado hakijaeleweka. Waamini kesho pia ni yao. Guys, don't give up.

Nilifanya kazi kama punda. Nilijituma, ilifika wakati nikaweka professional yangu kabatini. Nilifanya kazi yoyote ya halali. Hatimae niliibukia migodini ambako nako nilijituma kupita maelezo. Ikumbukwe kuwa baada ya kumaliza chuo ndipo maisha yalianza kwenda kombo kiuchumi na kupelekea hata kuachwa na aliyekuwa mpenzi wangu wa kipindi hicho.

Safari yangu ya migodini ilikuwa na neema. Kutoka kuwa mfanyakazi anayeshuka maduarani chini ya ardhi zaidi ya mita mia moja, mpaka kuwa mmliki wa mgodi, siyo kazi ndogo. Hii ni story ya siku nyingine, ila tu nimegusia hiki ili kuonyesha kuwa kutoka kuwa kibarua wa chini kabisa inawezekana siku moja ukaketi meza moja na wafalme.

Baada ya hali yangu kuimarika kiuchumi, kasheshe ilikuwa kumpata the ideal woman, mwanamke wa ndoto zangu. Ikumbukwe kuwa mademu zangu wa chuo wote kwa nyakati tofauti walinitema. Because of too much expectations ambazo zilikuwa hazitimii. Sasa nikiwa niko poa kiuchumi sikuwa na demu tena wa kuja kumuoa.

Wapo wanawake ambao nilikutana nao. It was hit and run! Kwa sababu hawakufika vigezo vya mwanamke niliyetaka awe mke wangu. Nilitumia mitandao ya kijamii kumsaka huyo an ideal woman. Jamii forum pia nimeweka mabandiko mara kadhaa kutangaza nia ya kuopoa jiko. Nikiri tu kuwa, wanawake niliowapata kupitia jukwaa hili, hawakuwa na vigezo nilivyovitaka. I did this several times with no good results.

Nikiwa desperate, sijui nimuoe yupi, nikijaribu karata yangu kwenye kila engo ya mitandao ya kijamii, Hatimae nimekuja kukutana na an ideal woman, mwanamke wa ndoto zangu FACEBOOK. Yes Facebook imenipa mke. Mwanamke niliyemngoja kwa zaidi ya miaka tisa sasa hatimae naenda kukutana nae Facebook. Naiamini mitandao ya kijamii ila siyo facebook. Facebook ni ya washamba, watu wa kijijini, watu wa mjini wanapatikana huko mjini Instagram, jamii forum na Twitter huko. Lakini huku Facebook, mmmmh.

Wakuu nikisema an ideal woman nadhani mnaelewa. Jina anaitwa Alice (siyo jina lake). Alice is beautiful, smart, disciplined and intelligent. Chenyewe anadai kwa muumba ni msambwanda tu ndiyo hajabalikiwa. Kitu kizuri zaidi, mimi mwenyewe siyo mtu wa kupenda vishundundu, hivyo is like Alice ameumbwa kama order yangu. Tangu nimekutana nae maisha yangu yameongeza value.

Wapendwa wanawake wazuri wa tabia bado wapo. Alice ni mmoja wao. She is a wife material. Tangu nimemuoa nyumba yangu imekuwa safi. Vitu vimepangwe kwenye mpangilio, nguo zangu, za kwake, vyombo vya ndani. Kiujumla mwonekano wa pale ndani unavutia. She is happy all the time, yaani tunaishi kwa amani. Siku sijaenda kazini nashinda tu ndani na my baby, she is so sweet.

Nyie asikwambie mtu, mpendane harafu pesa ipo, Mnaanzaje kuchokana. Aliyekwambia pesa siyo kila kitu kwenye mapenzi alikudanganya. Tafuta pesa ili ufurahie maisha ukiwa na umpendaye kwenye mitaa ya Juliana, Element na Samaki Samaki. Au msafiri kwenda kula raha za duniani huko Ibiza ama Dubai. About love, money is everything.

Sasa Alice ni mjamzito na nimemfungulia duka. Nimeamua ku share hapa ili kuwa inspire wale ambao wako block na mapenzi. Sijaandika kwa ajili ya kujikweza ila ni namna ya kuwafanya wengine wajifunze na kuchukulia changamoto walizo nazo ni za muda. Pia kuwafanya wadada wengi kuwa akina Alice. Cha mwisho naweza kusema love is an art, you can create it rough or smart.
Nyongo mkalia ini, hongera Sana sana

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom