Hatimae 2019 RAV 4 imepata muonekano mpya wa kiume

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
67,033
173,713
Naweza kusema Toyota ameanza kurudi kwenye mstari wa kutengeneza vyombo vya uhakika baada ya kutoka kutufyatulia uchafu kadhaa kati ya miaka 2012-2017 hapo.

Wale designer wa gari ambazo hazitazamiki nadhani watakuwa wameshapangiwa kazi nyingine mpaka sasa kama sio kuwa fired kabisa. Kuna mabadiliko makubwa katika muonekano wa gari za Toyota za sasa.

Hatimae 2019 tu design mpya ya RAV 4 ambayo imekaa kiume binafsi nimeielewa sana na naweza kuhamia katika hio brand panapo majaliwa. RAV 4 nilikua sizikubali kabisa licha ya fuel economy ila shepu yake ya kike ilikuwa inanikera hata hazipimpiki yani.

Ichekini 2019 Rav 4 hapa.
 
2019-Toyota-RAV4-front-three-quarter-1.jpg


2019-Toyota-RAV4-rear-three-quarter-01-1.jpg
 
Back
Top Bottom