tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza ratiba ya vikao vyake vya kitaifa vitakavyofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Gabriel Makalla leo tarehe 17 Agosti 2025, kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitafanyika tarehe 21 Agosti 2025, kikifuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa kitakachofanyika tarehe 23 Agosti 2025.
Soma pia: Wajumbe katika uchaguzi wa wabunge wa Viti Maalum kupitia kundi la vijana wa UVCCM wamewachagua wagombea sita akiwemo Jesca John Magufuli kuwa wabunge
Aidha, ajenda kuu ya vikao hivyo itakuwa ni uteuzi wa wagombea wa Ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge wa viti maalum, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi viti maalum.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa vikao vyote vitafanyika jijini Dodoma.