Hatima ya ubunge wa Opulukwa leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatima ya ubunge wa Opulukwa leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fikrapevu sungura, May 4, 2012.

 1. fikrapevu sungura

  fikrapevu sungura Senior Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatima ya ubunge wa Opulukwa leo

  By Habari Leo

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora leo inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Meatu katika mkoa mpya wa Simiyu yaliyompatia ushindi mgombea wa Chadema, Meshack Opulukwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

  Kesi hiyo iliyofunguliwa na mpigakura Renatus Masanja ilianza kusikilizwa Machi 12, mwaka huu mjini hapa.

  Katika kesi hiyo, Masanja anadai kuwa, katika uchaguzi huo, kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni, taratibu na maadili ya uchaguzi kutokana na dosari zilizojitokeza katika uchaguzi huo.

  Katika hati ya mashitaka, Masanja anadai kiuwa Opulukwa alitumia lugha za kibaguzi dhidi ya mgombea wa CCM, Salum Khamis “Mbuzi”.

  Pia anadai kwamba baadhi ya wasimamizi wasaidizi katika vituo vinane, walimpigia kampeni mbunge huyo na kwamba Msimamizi wa Uchaguzi alitangaza matokeo mara mbili kinyume cha taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

  Katika kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na Jaji Fredrick Wambali, upande wa mlalamikaji ulileta mahakamani hapo mashahidi 15 ili kuthibitisha madai yao huku upande wa utetezi ulileta mashahidi tisa.

  Kesi hiyo ilivuta hisia za wananchi wananchi wengi waliokuwa wakiisikiliza kutoka katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Meatu, Bariadi, Maswa na Shinyanga na leo inatararajiwa kuwa na wasikilizaji wengi zaidi.

  Katika kesi hiyo, walalamikiwa ni watatu ambao ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Opulukwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Meatu.

  Mlalamikaji alikuwa akiwakilishwa wa Wakili Kamaliza Kayaga huku Mbunge wa Meatu akiwakilishwa na Wakili Godwin Mganyizi.

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi wakiwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Tabora, Jackson Brashi, Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Jackline Mrema na Mwanasheria wa Serikali, Abraham Mohamed.
   
 2. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mungu ibariki chadema yetu.
   
 3. A

  A revolutionist Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kamanda endeleeni kutupatia updates kwa mtu aliyepo hapo mahakamani!
   
 4. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Chaguzi zikirudiwa,makaburi yanachimbwa...
   
 5. B

  Bukutonaga JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wana JF nipo maswa katika viunga vya mahakama makamanda na wananchi wengi wametoka meatu kuja kumuunga mkono mpiganaji Dr Opulukwa,ila napata mashaka maana mnamo saa 1 na dk 40 ziliingia gari 3 zikiwa zimejaza maaskari chini ya usimamizi wa RCO wa mkoa wa shinyanga - Mr.Kashinje so sielewi hapa maswa tunao askari wa kutosha ya nini tena tuletewe wengine kutoka shy KIFUPI NAANZA KUPATA MASHAKA NA HUKUMU HAKI INAWEZA KUTOTENDEKA,

  kumbukeni walalamikaji ambao ni wapambe wa jamaa alomwagwa ni kwamba Mhe. aliwaambia wananchi wasimchague kwani ni mwarabu,hiyo ndo kesi ilivyo na kweli mgombea alikuwa mwarabu ni mambo kama ya Arusha wanaoshikia bango ni wengine tofauti na aliye galagazwa!

  Nawasilisha!


  SOURCE: Mimi mwenyewe toka eneo la tukio.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Lete taarifa!
  Kama mambo ni hayo basi ni masikitiko mengine kwa wana cdm!
  Watatumia precedence ya kesi ya Lema!
   
 7. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Duh!! Leta updates mkuu!!
   
 8. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Iko karibu na ukweli!
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Meatu hata kama CDM wakisimamisha kinyesi kitashinda kwa wingi!
   
 10. g

  ghoroo Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vp hukumu
   
 11. O

  Omulangira JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Endelea kutujuza kamanda
   
 12. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Bukutonaga mbona umepotea kamanda? Please tujuze yanayojiri huko
   
 13. B

  Bubona JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hukumu inatarajiwa kusomwa saa ngapi?
  Kama upo eneo la tukio, endelea kutupa updates!
   
 14. B

  Bukutonaga JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nakuja mda si mrefu wakuu
   
 15. B

  Bukutonaga JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wakuu jaji bado anaendelea kusoma,so tuwe na subira!
   
 16. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,996
  Likes Received: 2,651
  Trophy Points: 280
  CCM na mbinu chafu,lakini watashindwa tu.
   
 17. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mungu atamtangulia tuko pamoja
   
 18. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tupe muhutasari mpaka sasa kakubali ngapi na katowa nje ngapi sio unatuambia tu jaji anaendelea kusoma
   
 19. e

  enhakkore Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunasubiria kwa hamu kujua
   
 20. G

  G. Activist JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Tujuzeni bandugu
   
Loading...