Hatima ya Tanzania 2025-2050

Hatima ya Tanzania 2025-2050

CARDLESS

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2017
Posts
7,867
Reaction score
15,990
Leo hii ni Tarehe 16/08/2025, ninaandika hapa hatima ya nchi yetu hii pendwa (TANZANIA).

Hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania, hapa ni kwetu, hapa ndipo tunapojivunia kama watanzania.

Kabla ya kuwa Juma au Patrick au Patel au Nakamura au Masanja ulianza kuwa Mtanzania, Yes sisi ni watanzania na hakuna kitu kitatuondolea hilo la Utanzania wetu.

Lakini kuna sehemu tumeteleza, na sehemu hiyo imetufanya tutiririke mbali sana, yaani ni mbali na kwamba tuko na stage moja tu kama Tanzania tutaingia kwenye matatizo makubwa sana.

Mimi kwa kusoma historia za nchi mbalimbali, falme mbalimbali na tawala mbalimbali, kuna kitu nilijifunza very technical.

Tangu tunapata uhuru hii nchi yetu kuna kitu hatukukidhibiti, yes na hapo ndipo lilipo tatizo.

Tatizo hilo ni DINI. Yes ni DINI. Kama nchi lazima tukae chini turekebishe sheria zetu hasa hisi za taasisi za Dini, hizi taasisi zimemea hadi sasa kila mtu anaweza kuwa Shekhe, au anaweza kuwa Mchungaji au Askofu nk. Watanzania wengi wamekuwa wahanga wakubwa wa hawa viongozi wa DINI, mara kadhaa DINI imekuwa mwamvuli wa kutetea mabaya, au Kupanga njama za kupendelea au kuondoa kundi fulani tofauti na dini au dhehebu fulani.

Narudia imebaki step moja tu sisi kuingia kwenye mgogoro mkubwa na usioweza kutatulika kirahisi wa UDINI. Hatujachelewa, we can do something good ili kudhibiti hatari iliyopo mbele yetu.

Kwa kuangalia mazingira na kwa namna nchi zetu za Kiafrika na hata akili zetu zilivyo, nishauri Serikali ifanye mambo yafuatayo ili kudhibiti aina hii ya hatari inayokuja kwa kasi kwa mrengo wa DINI.

1. VIGEZO VYA MTU KUWA SHEKHE au MCHUNGAJI au ASKOFU lazima awe anafanya kazi au bishara zingine nje ya DINI.

2. Kusajili Msikiti/Kanisa lazima kuwe na uchunguzi wa Mwaka 1 na Ada isiyopungua mil 10.

3. Kuondoa msamaha wa kodi kwenye taasisi za Dini.

4. Shekhe au Mchungaji/Askafu kabla ya kuruhusiwa kufanya miujiza lazima kwanza afanye miujiza sehemu atayopangiwa ikiwa ni kuthubitisha unabii au unajimu wake. Kushindwa kufanya hivyo asipewe nafasi yoyote ile ya kuwa na kanisa au Kuongoza Msikiti.

5. Masomo ya Dini yafundishwe kuanzia Kidato cha Tano na Sita, kipindi ambacho watu wamekomaa kiakili na wanaweza kutengenisha uongo na kweli.

6. Mtu yeyote atakayetumia DINI kujaribu kuwakusanya watu kwa mrengo wa kisiasa, kushawishi au kundi lake limuonee huruma au kufata upande wake basi kuwe adhabu ya wazi ya KIFO. Watu watangaze Dini kama njia ya upendo sio kufanya Dini kama nyenzo ya mtu, kutapeli, kudanganya watu, kutafuta influence ya kukaa au kuondolewa madarakani.

7. Misikiti na Makanisa iwepo sehemu maalum tu with minimum number, yatengwe maeneo ya watu kuswali na Kusali kama tunavyotenga mazingira ya Viwanja vya michezo.

8. Viongozi wa Dini wasipewe Airtime kwenye shughuli za kisiasa na pia serikali iruhusu mikesha miwili tu kwa mwaka kila Dini. Waislam (MAULID na EID EL FITR) Wakristo (PASAKA na X MASS) WAHINDU (DIWALI) na siku zingine zote Sala ziishe saa 6 kamili usiku with minimal volume.
Kama watanzania lazima tunuse hatari ya UDINI, hili tunalichukulia kawaida ila lipo sana, na bahati mbaya sisi waafrika tunaamini kabisa kuwa hizi DINI ni za kweli hivyo hazistahili kuwekewa sheria kwamba tunamchukiza Mungu. Lkn ukweli ni kwamba watu wamefanya DINI kama mwamvuli wa kuwaweka watu wanaowataka kutawala na wala hizi Dini haziko kwa ajili ya kutusaidia kimaisha.
Tuungane tukatae utapeli wa DINI. Kwa hali ilivyo, ukimsikiliza Gwajima kwa umakini utagundua amechukua nafasi ambayo anahitaji nguvu ya Wakristo ili kunusuru kile anachoona yeye hakifai, lkn madhara yake yapo hapo karibu ambapo na hawa waswali sunni (Wavaa kobaz) wamesikilizia huo mziki nao waweke mdundo ili sasa tupate Segere la maana hapo step ijayo.
Serikali haina Dini na si mara ya Kwanza nyumba za Ibada kufungwa pale inapoonekana kuna shida sehemu.

Tusipoliangalia hili kwa umakini na tukifuata kwa mkumbo kwa imani za Dini na sio kwa akili zetu basi hatupo mbali sisi kuwa kama nchi ya Afrika ya Kati, Nigeria nk ambapo Dini huwagawa watu wake.

Kama tusiporekebisha hawa akina GWAJIMA na MAZINGE au MWAIPOPO au KITIMA ambapo wao huona wanahaki juu ya MAISHA ya wengine na kwamba wao wametumwa na MUNGU (INACHEKESHA SANA) basi siku moja, wewe utapigana na rafiki yako, Classmate wake, mfanyakazi mwenzako, jirani yako ambaye mlikuwa mnasaidia kwa shida na raha kisa tu kauli hizi za hawa WAPUMBAVU wa DINI.

TUKO NA STEP MOJA KUFIKIA VURUGU ZA DINI. TUJIPANGE KUKABILIANA NAZO au TUZUIE SASA HIVI ZISITOKEE KWA KUWEKA SHERIA KALI, IKIWA NI PAMOJA NA KUWALAZIMISHA VIONGOZI KUSAINI HATI NA SHERIA ZA MAADILI ZENYE KUWAONESHA ANY MISTAKE ADHABU YAKE NI KIFO.
 
Back
Top Bottom