Serikali ya awamu ya Tano imeamua kuchukua uamuzi wa kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Mkoani Dodoma.
Kwa hakika hatuna shaka na uthubutu huu, wakati Wizara karibia zote na baadhi ya Taasisi zikielekea kwenda Dodoma kwa asilimia 100% Serikali yetu sasa ianze kujipanga kuona ni kwa namna gani MAJENGO YALIYOKUWA YAKITUMIWA NA SERIKALI JIJINI DAR ES SALAAM HAYATABAKI TUPU. Ingeshaundwa timu kwa kuwashirikisha wataalamu Wahandisi, maafisa masoko n.k kwa kushirikiana na NHC kuweza kupata shughuli mbadala kwenye majengo hayo. Ni wazi kwamba endapo majengo hayo ya Serikali yatakaa tupu bila shughuli yoyote kuendelea humo, Serikali itakuja kuingia hasara kubwa sana ya ukarabati wake hapo baadae. Hivyo serikali ichukue hatua za haraka kuyapangisha ili yasigeuke makazi ya Popo na buibui na hata kuingiliwa na maji ambayo yanaweza kuharibu mifumo mbalimbali.
Tunajua kwamba hayo Majengo yanamilikiwa na Wizara mbalimbali, kitendo cha kuachiwa majengo hayo yaendelee na kusimamiwa na Wizara moja moja ilihali Watendaji wake wakiwa tayari wako Dodoma kutafifisha jitihada za kuyapangisha au kuyawekea kazi mbadala. Vilevile siyo Wizara zote zenye wataalamu wa masoko na Mikataba juu ya pango za majengo. Hivyo ni vema ingeundwa timu moja ikasimamia majengo yote na fedha za pango zikaelekezwa Wizara mama mwenye Jengo.
Ni mtazamo tu. "Tanzania kwanza wadau"