Hati za utambulisho wa Dr. Ramadhan Dau zakataliwa Malaysia

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari wanaJF,

Katika pitapita zangu nimekutana na habari katika mtandao wa Africa Intelligence inayoonyetisha kuwa aliyekuwa kigogo wa NSSF na baadae akapangiwa kazi ya Ubalozi ndugu Ramadhan Dau, ingawa aliwasilisha hati za utambulisho wa kuwa balozi takribani miezi 7.

Lakini mpaka sasa bado hati zake za utambulisho wa kuwa balozi katika nchi ya Malaysia hazijakubaliwa na mamlaka/Serikali ya taifa hilo lenye makao yake makuu katika jiji la Kuala Lumpur

Tatizo likowapi mpaka mteule huyu akwame?
========
Sehemu ya taarifa hiyo inasema:

Ramadhan Dau not accredited in Kuala Lumpur.
Although he submitted his credentials seven months ago, Ramadhan Dau has still not been accredited by the Malaysian government.

=========

dau-png.396155


Wewe ndio umemaliza...Hii link ilikuwepo mtandaoni,The Citizen waliiona mapema,na hii huwa inaeleza habari nyingi za "chini ya kapeti" kuhusu Afrika.Ndio maana jana The Citizen wakamuuliza Dr Mahiga,na ametoa majibu ya "kidiplomasia" sana.

Kuna mtu huko juu anauliza,inakuwaje hao Malaysia wamkate kabla hajateuliwa,lkn ukweli ni kuwa kabla ya kutangaza fulani anaenda ubalozi wa nchi fulani,tayari taarifa za nchi anayoenda za kumkubali zinakuwa zimeshafika na muhusika kukubaliwa,hii ni baada ya "details" zake kuwa zimechunguzwa na nchi anayoenda.

Kawaida ukiona pale Rais Ikulu anapokea "Utambulisho" wa Balozi wa kutoka labda Italy,Somalia au Korea Kusini,ujue "Taarifa" zake zilishaletwa Tz na Mamlaka za Tz zilishamchunguza na kuona mtu huyu anafaa kuwa sehemu ya Wanadiplomasia wa Tz.Hivyo kuna wengi huwa wanaletwa na wanakataliwa kimyakimya.

Wakati wa JK tuliwahi mkaa balozi wa Uingereza(?) aliyetakiwa kuja Tz ambapo awali alihudumu Kenya.Tulimkataa kwa sbb alikuwa "shoga".Kuna wakati wa Nyerere alimkataa Balozi wa Malawi ambaye alikuwa ni kibaraka wa Makaburu wa South Africa,aliyewekwa kwa "mission" maalumu ya Makaburu na Kamzu Hastings Banda.

Kwa hiyo,ile ya kupokelewa mbele ya TV huwa ni "formality" tu,lkn balozi anakuwa amechunguzwa kabla na kwa muda mrefu.Hivyo kama jina la Dau limetumwa toka January hadi sasa,ujue mamalaka za Kuala Lampur zinachunguza,na ukifungua hiyo link baada ya kulipia utaona inasema kwanini MALAYSIA inasita kumthibitisha Dr Dau.

Mamlaka za Kuala Lampur zinasita kwa sbb wanasema kuna "sintofahamu" nyingi zinaendelea juu ya Dr Dau ktk nchi yake,ikiwemo maafisa wake wa chini katka taasisi aliyokuwa anaiongoza kuhusishwa na "ubadhirifu" wa miradi kiasi cha kuhojiwa na PCCB.Wanasita sbb wanajiuliza kwanini Rais JPM anayeonekana kupinga rushwa kaamua kumuoandoa kwenye Taasisi kubwa kama NSSF na kumpeleka ubalozini?Wanasita sbb Taasisi aliyoingoza inalalamikiwa kutekeleza miradi mikubwa yenye harufu ya rushwa.Serikali ya Kuala Lampur inataka kujiridhisha,ili ifanye kazi na mtu asiya na "mawaa".

Ukijua ni kwanini Mandela baada ya kuachana na mkewe baada ya kutoka Gerezani,Makomrade wa ANC na watu wake wa karibu,walimkabidhi Mandela kwa balozi wetu wa Tz nchini Afrika Kusini Kamaradi Mpungwe aje apumzike nae kwenye hifadhi ya Lake Manyara kwa week mbili "kisirisiri" ili akili imkae sawa.Ukilijua hili..utaona umuhimu wa balozi na nafasi ya kumchunguza maisha yake ya nyuma kabla ya kumthibitisha.

Jamhuri ya Watu wa Dominika,imemkataa balozi wa Marekani aliyepaswa kwenda kuhudumu kwenye nchi yao baada ya kuwa wamejiridhisha kuwa jamaa ni shoga na anapanga kwenda Dominika kuhudumu akiwa na "bwana" yake.Askofu wa Katoliki wa nchi hiyo,akishirikiana na Serikali wamepinga vikali ujio wake na USA imebadili uamuzi.Hii haijatokea kama "ajali",bali jina lilipelekwa kabla na mamlaka za Dominika zikachunguza na kujua ni nani atakuja nchini mwao.
 
Kituko kingine hiki mtu wa kawaida kama Mimi nilipokelewa tu siku moja nikala maisha ugaibuni iwe Dau ?
Why always you dad?
Haaaah
 
Back
Top Bottom