Hatari ya nchi yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatari ya nchi yetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bingu wa m, Sep 16, 2012.

 1. b

  bingu wa m Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru mungu kwa kunionyeshamengi duniani,Kuna jambo ambalo linani nyima usingizi na ni suala tunalolisikiala udini,nime bahatika kufanya kaziubalozi wetu wa Tanzania nchini Somalia miakaya mwisho wa utawala 1990 natulihamishia kazi zetu Ethiopia baada yahapo,Somalia ilianza kupoteza mwelekeo pale ukoo zingine zilipoanza kugawanywakwa misingi ya ukoo na bwana said bare akaona apendelee ukoo wake, jeshi likagawanyika na 1990 vita vilianza nanchi ya Somalia ilifikia mgawanyiko wa clan na clan na kisha sub clanikaendelea hadi sub sub clan,hawa ni watu wa kabila moja dini moja lugha moja, tumeona rwanda mauaji ya watusi yalianza 1959na yakarudi 1994,tumeona nchi ya sudan watu wakiuawa kwa ajili ya rangi yao audini yao,tunaona Burma,Yugoslavia n.k.
  Tutakua vipofu au wapuuzi tukiacha tugawanywe kwa misingi yakidini na wanasiasa au wahubiri wetu wa kidini,tutakua tunadanganya nafsi zetukwamba uchaguzi uliopita kwenye baadhi miskitina makanisa katika baadhi ya wilaya hazijatumika kisiasa,tumeanza kuona vituvipya mwaka huu,Napenda kuwasihi watanzania wenzangu kama tunaipenda nchi yetukwa dhati tuwasihi viongozi wetu wa kisiasana kidini waelewe hii ni nchi yetu nahatuna Tanzania ingine wa kiichoma hii,waache ubinafsi na waarithishe watotowao nchi kama walivyo ikuta wenyewe ,Tutakua tunatenda dhambi kubwa kama nchitulioikuta wakristo na waislamu wanakaa pamoja kwa amani na upendo na tukawawachia watoto wetu chuki ambayohaitokwishwa pindi ikiingia,Tusikubali upuuzi huu wana siasa wakituhadaa auviongozi wakidini,tunaomba vijana wote wanchi hii waanzishe kampeni ya kupinga mgawanyo wa kidini,na tarehe 9 mwezi 12 Iwe siku ya kupinga kupandikiziwa chukindani ya nchi yetu .kwani kila nchi ikianza machafuko wahubiri na wanasiasandio wakwanza kukimbia.TAFAKARI EWE MTANZANIA.
   
 2. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Well said mkuu. Hawa ccm wanapotupeleka siko kabisa...
   
 3. T

  Tenths Senior Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kwa kuanza mimi nimeanzisha NGO itakayokuwa na makao yake makuu hapa Dsm ikiwa na lengo kuu moja tu kuelimisha jamii kuhusu madhara ya udini na ukabila katika nchi.
   
 4. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Umeongea Jambo la busara ambalo Watanzania wengi tunalifumbia macho. UDINI na ukabila unashika kasi sana kadri siku zinavyozidi kuyoyoma. Na yote haya yanaletwa na WanaSiasa na siasa zao za kuchumia matumbo Yao. Ni kweli Kama ulivyosema yakitokea ya kutokea hao WanaSiasa ndio wa kwanza kukimbia nchi. Tujiulize kwa nini wanahifadhi PESA kwa wingi USWIZI na nchi nyingine!?

  Wakati umefika kwa Watanzania kutafakari kwa makini KESHO YETU Itakuwaje? Hawa wanaSiasa hawako kwa ajili ya manufaa yetu. TUSOME ALAMA ZA NYAKATI NDUGU ZANGU WATANZANIA.
   
 5. hodogo

  hodogo JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 239
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bingu hata mimi nashangaa serikali yetu kulifumbia macho jambo hili likingali changa! Nathubutu kutamka hivyo kuwa likingali changa kwani wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza na hata awamu ya pili na tatu, tumeshuhudia kauli kali za viongozi wa juu wakikemea udini kwa maneno makali! Msimamo wa Hayati Baba wa Taifa katika jambo hili la dini sina hata haja ya kulisema, kidogo nirejee kisa cha wakati wa "Mzee Ruksa", kisa kilichompa hilo jina, wakati ambapo waislamu walianzisha harakati ya kuvunja mabucha ya nyama za nguruwe! Utaratibu ule Mzee Mwinyi aliukemea kwa sauti kubwa japo yeye mwenyewe ni muumini mzuri wa uislamu!

  Leo nimesikia katika baadhi ya vyombo ya habari vikimnukuu Waziri Mkuu kuwa na wasiwasi na usahihi wa takwimu za sensa iliyofanyika juzi tu hapa, ili hali watu waliosusia sensa, kwa makusudi pamoja na kushawishi wengine wasihesabiwe, wanaachiwa huru na serikali kwa shinikizo la kidini na serikali iko "Comfortable"! Sasa mnalalamika nini? Kumbukeni mkicheza na nyani katika mashamba ya mahindi mtavuna mabua!


   
 6. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Udini, Ukabila na hata ui-tikadi wa kichama bila kuweka maslahi ya Taifa mbele ni janga la kitaifa
   
Loading...