Hatari ya mafanikio - CHADEMA/UKAWA & Lowassa


Umeandika hoja chanya kwa asilimia 75 na hoja hasi kwa asilimia 25.Hii inakufanya uwe na hoja chanya asilimia 50.Sio mbaya!

Kuna vitu tunatofautiana ufikiri,ntataja viwili:
#War on two fronts is the last thing a strategists would wish for.
#Na hoja ya kwamba ajenda ya mabadiliko ni ya Ukawa na sio Lowasa.

Hoja ya kwanza inapingwa tu na hali halisi duniani kwa sasa.Every individual,every nation,every political party has war on multiple fronts.Organization,discipline and leadership ndio determinants za mafanikio.
Ndio maana CCM inapaswa kujitafakari sana kwenye nafasi ya mwenyekiti na katibu mwenezi wa chama.Nape anawagarimu sana na matamshi ya mihemko.Magufuli is not mwenyekiti material!

Hoja ya pili nayenyewe haina tu uhalisia kwenye siasa,Muungano wa kisiasa is never a marriage made in heaven.Hizi ni dili za Muda mfupi.Kuna notion unataka kuileta kama Lowasa anaweza kutaka kujenga ufalme ndani ya Ukawa!
I strongly doubt that for 2 reasons:
1.He couldn't do that in CCM all his life time,how could he do it in Ukawa within 5 or 10 years?
2.The environment for empire building in short time is not there.Ukawa is too many pieces to glue together easly and I say this frankly given his age.
 

Imekaa vizur sna hongera.
 
Mkuu usiwe na wasiwasi. CCM ing'oke kwanza. Uozo mwingine unaobaki utashughulikiwa hatua kwa hatua. Kumbuka hata Roma haikujengwa kwa Siku moja.
 
Ulichosahau kuzungumzia ni kwamba Chama KUBWA kuliko Lowassa!.. Na ule mtandao wake sasa hivi umeshapigwa kombora la kwanza ambalo walitegemea Kikwete alikuwa upande wao wangepita CC bila kupingwa!..

2. Mtandao hatari wa Lowassa ulishatangaza kulipa kisasi kwa kambi ya Kikwete na familia yake hata kabla ya kuingia madarakani kuwa wakiingia madarakani watakiona cha moto sijui kwanza watamvua JK Uenyekiti na kinga zote!. Huwezi kuutafuta urais kwa kutishia watu hasa kumtishia rais wa nchi hata kama.. Kikwete kama mwenyekiti wa CCM na rais wa nch hii ana ushawishi mkubwa sana kwa wananchi kuliko mnavyofikiria na atahakikisha Lowassa haingii IKULU... Chama kubwa!

3. Mbali na kuwa na mtando mkubwa, Kukatwa jina la Lowassa CC haikuwa bahati mbaya, bali ilishapangwa na kukubaliwa kwa sababu ndani ya CC kuna wazee waheshimiwa ambao wanamjua Lowassa kiundani zaidi. Lowassa ana maadui wengi pia ambao kwa njia zake za uungu mtu aliyaweka maisha yao katika wakati mgumu sana haswa wale CCM Asilia toka Mkapa, Mwinyi, Sumaye, Warioba, Salim na wote hawa wanayajua madudu yake mengi hivyo wanamsubiri tu wakati wa kampeni.

4. Mtandano mkubwa wa Lowassa ni watu waloahidiwa vyeo, Kila mshirika ameahidiwa uongozi wa wizara, idara ama shirika na taasisi za Umma hata kabla ya kupimwa uwezo wake kama kiongozi. Hii ni hatari kubwa zaidi kiutawala ikiwa Cartel inajipanga tayari kuchukua nchi. Haya ni Mapinduzi ya nchi kupitia watu hatari kabisa. Mtu mmoja hawezi tishia amani nchini hata kama Apson yupo nyuma yake, .huu ni mwaka wa Usalama wa Taifa kuhakikisha amani inapatikana nchini.

Lowassa hawezi kuwa rais wa nchi hii, Uongozi haupatikani kwa kupitia ukubwa wa Cartel ingelikuwa hivyo Pablo Escoba angekuwa rais wa Colombia!..
 

Mr hero katika ubora wake
 
Mwambie JK naye awapige risasi wapinzani wake kama Kagame kisha uone kitakachotokea. Wapinzani wa Kagame wengi sio wa mfumo wa kidemokrasia bali ni uasi ambao mapambano yake yanakwenda kwa mtindo huohuo wa risasi.
Kwani Gabgo yuko wapi baada ya kuleta za kuleta baada ya uchaguzi? Uhalifu wa kivita ni huo wa kusababisha upotevu wa maisha ya wengine pasipo sababu ya msingi bali matumizi mabaya ya madaraka.
 

Low.....war....Sir
 
Kama waliweza kumkata akiwa CCM humo humo akiwa nje ya CCM atakuwa mlaini kama kate uliochovywa kwenye chai
 

Comment yako utasema vyama hivi vya siasa vinafanya kazi kinyume na taratibu
 
Dzerzhinsky

Hata Libya, Misri na Iraq nao walikuwa wanawaza kama wewe lakini kwa sasa hawawezi kuwaza kutamani kuwaza,kama wewe.
Achana na mifano ya nchi za kiarabu, zungumzia nchi za kariba yetu Kama Kenya, Zambia n.k hafu tuone Kama point yako itakua Na umuhimu!
 
Last edited by a moderator:
I Salute You My Brother,you Have Brains.The Best Of Analyses
 
Yaani unatumia malengo yetu kiondoa CCM madarakani kwa kumpigia Lowassa kampeni kujiunga CHADEMA na UKAWA hali yakuwa Lowassa ni fisadi........ Lowassa ni fisadi na ataenelea kuwa fisadi. Ye asubili tuchukuwe dora mwaka huu tumfunge na kumfilisi mali. Nae analifahamu hili ndio maana anahangaika kujinga CHADEMA ili kukwepa kifungo. Ashindwe na alege.... atuachie CHADEMA na UKAWA yetu!
 

Tumeona vyama dola vikubwa duniani vilivyoangushwa kwa sanduku la kura. Kama ccm ilikuwa na mwanzo pia ina mwisho wake. Na mwisho wake kwa asilimia kubwa mwaka huu.
 
Juhudi ni kubwa ili kuendelea kuficha mafisadi wa nchi. Chadema wajitambue, haingii akilini ganda la ccm kuwa mtaji wa chadema
 
Sumu haionjwi

Hii ni hatari kubwa!
Watu wanaonadiwa na mamluki wa kibiashara inaelekea watainunua UKAWA wakati wowote ule na ni kwa nia moja tu, kukamata dili zote za dola ili wanufaike kiuchumi.

Lakini wananchi makini wanaendekea kugutuka.
Tunajua kuwa hata wapinzani ni watanzania na huko kuna watu makini kitaifa.
Simpigii debe Dr Skaa lakini haingii akilini Dr Slaa kumtangaza Lowassa kuwa fisadi, halafu kula matapishi yake bila maelezo na kumkaribisha fisadi huyo huyo kukipigia debe chama chao.

Maendeleo ya Tanzania ni kuwa na upinzani makini utakao sahihisha kama sio kupiku chama tawala.

Kwa ujinga huu wa kukumbatia ufisadi ulio temwa na chama tawala, UKAWA unawakaribisha kina Rosta na Karamagi and co. iliwagawane rasilmali za nchi hii.

...... mpaka hivi sasa ndani ya UKAWA ni mtafaruku wa kukaribia kusambaratika kwani hawajui wanaenda Ikulu kufanya nini na kwa madhumuni gani kwa mwananchi wa kawaida.

Sumu haionjwi wanaukawa mutakufa bure!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…