Hatari ya kupotea hifadhi ya Ngorongoro

Hatari ya kupotea hifadhi ya Ngorongoro

Wa kuondolewa ngorongoro Ni NCAA, wanawatesa na kuwanyanyasa wamasai., Wanaua wanyamapori na kuwasingizia wamasai. Ngorongoro Ni eneo.la asili la wamasai toka enzi za Yesu. Kuwaondoa Ni crime against humanity.
 
Nasema hivi, tukitaka kuinusuru hifadhi ya Ngorongoro lazima Wananchi Wafurushwe haraka sana...
Ukiondoa watu pale mbuga haitakua na maana tena savabu ile mbuga inashangaza dunia sababu watu. Na wanyama pori wakali wanaishi pamoja na binadamu peacefully ndio upekee wake

Ukiondoa watu mbuga inakuwa ya kawaida tu kama zilivyo mikumi,nk
 
Samia anataka kufanya ethnic cleansing eneo la ngorongoro, kuwatoa wamasai kuwaleta wasio wamasai kujenga mahoteli. Kama alivyotaka kufanya Bashir eneo la darfur kuwaua raia wasio waarabu na kulaaniwa na mataifa ikiwemo Tanzania
 
Umaarifu wa Hifadhi hiyo ni kwa sababu ya mfumo wa maisha Jumuishi (Wanyamapori na Jamii). Ukiondoa jamii pale, maana yake umeiondolea sifa Hifadhi yake ya multiple Land na umaarufu. Haitakuwa tofauti na Hifadhi ya Manyara na Tarangire. Haitakuwa tena moja ya maajabu ya Dunia.

Niliwahi kuona mkataba wao na serikali ya mkoloni muingereza wakati wanapisha kuanzishwa Hifadhi ya Serengeti, hivyo kisheria ni haki yao kuwepo pale. Babu zao kukubali kuachia Serengeti ni jambo kubwa walilofanya, hii ndiyo Hifadhi Bora Afrika kwa sasa.

Tanzania tunajivunia kuwa na maeneo mengi ya Hifadhi lakini ukijaribu kuangalia yalikuwa maeneo ya wafugaji zaidi wakiwa wamasai, kwa maandiki hiyo wanastahili kuheshimiwa na kudhaminiwa. Nina Imani ingekuwa makabila mengine hakika tusingekuwa na wanyama/hifadhi hao/hizo wengine tunakula mpaka konokono.

Shida nyingine huenda wahifadhi wa mle hawana mipango mizuri ya kuendeleza mfumo ule wa matumizi Jumuishi kama sheria inavyotaka, wakae na jamii wakubaliane watafute majawabu ya changamoto kwa pamoja, lakini pia ushirikishwaji na elimu uimarishwe. Serikali itazame hili huenda na wahifadhi wanashindwa majukumu yao ikiwezekana ibadilishwe mfumo wa usimamizi wa eneo hilo.
Tatizo lililopo sasa ni modernization ambayo sasa hivi hatuna masai asilia anayeishi ngorongoro kwa desturi za kimaasai za kuishi na wanyama bila kuwaaathiri. masai wa miaka ya 60 siyo masai wa leo hivyo mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kwa jamii zotewakiwemo masaai ndiyo inayokingana na malengo ya awali hivyo tubadilishe set up ya ngorongoro kulingana na context ya leo.
 
Nasema hao Wamasai wafurushwe haraka sana...

Tukiwachezea tutaisoma Ngorongoro kwenye historia soon
Unasema Kama Nani?
Ndugu yangu unapo ongelea swala la ngorongoro jaribu kua na ustarabu kiasi maana unaongelea maisha ya watu.
Pili watu hao hawajavamia hifadhi Bali hifadhi Ndio imewakuta pale walipo
Lakini naomba tujiulize hifadhi ya ngorongoro imeanza lini na wamasai Wana mda gani hapo yaani miaka 700 watu wameishi pale alafu uje useme kua wafurushwe kweli? Kua na huwakika na kile unachokiongea
 
Back
Top Bottom