Hatari ya kupotea hifadhi ya Ngorongoro

Hatari ya kupotea hifadhi ya Ngorongoro

PendoLyimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
1,059
Reaction score
1,133

Umoja wa wasomi wa vyuo vikuu wanaotokea wilayani Ngorongoro wamezungumza masuala mbalimbali kuhusiana na wilaya yao.

wameeleza sababu za wao kujaza mifugo hifadhini humo walipozungumzia habari iliyochapishwa na Gazeti la JAMVILAHABARI kuhusu changamoto ya muingiliano baina ya watu, uhifadhi na mifugo katika hifadhi ya Ngorongoro inayopelekea kuhatarisha kwa uhai na uwepo wa hifadhi hiyo.

Katika utetezi wake mmoja wa wasomi hao anayeonekana katika video hii, amekiri kuwepo kwa makundi makubwa ya mifugo hifadhini humo tofauti na hali ya uwezo wa hifadhi na hivyo kusema uwingi wa makundi ya mifugo hifadhini humo kwao upande wao ni jambo la kawaida kwani ndio chanzo chao pekee cha kujikimu na maisha na kwamba isingetarajiwa isingekuwepo mifugo hiyo.

Hivi karibuni gazeti la JAMVILAHABARI liliandika kuhusiana na Hatari inayoikumba hifadhi hiyo ya kipekee Nchini baada ya kujionea hali ilivyokuwa mbaya kwa muingiliano kuwa mkubwa baina hifadhi, watu, wanyamapori na mifugo.

waratibu wa wa Kituo cha wanahabari watetezi wa Rasilimali na Taarifa (Media Centre for Information and Resources Advocacy - MECIRA), wamesisitiza kuwa Hali ni mbaya Hifadhini Ngorongoro na jitihada za makusudi kunusuru tatizo hili zinahitajika ili pande zote zinazoihusu hifadhi hiyo ambazo ni watu, mifugo, mimea Maliasili zilindwe.
 
Tatizo ni ukame ulioikumba hiyo wilaya hivyo wameona wachungie huko hifadhini.....

Kwani hakuna mapori ya akiba yanayofaa kwa kuchunga mifugo?
 
Umaarifu wa Hifadhi hiyo ni kwa sababu ya mfumo wa maisha Jumuishi (Wanyamapori na Jamii). Ukiondoa jamii pale, maana yake umeiondolea sifa Hifadhi yake ya multiple Land na umaarufu. Haitakuwa tofauti na Hifadhi ya Manyara na Tarangire. Haitakuwa tena moja ya maajabu ya Dunia.

Niliwahi kuona mkataba wao na serikali ya mkoloni muingereza wakati wanapisha kuanzishwa Hifadhi ya Serengeti, hivyo kisheria ni haki yao kuwepo pale. Babu zao kukubali kuachia Serengeti ni jambo kubwa walilofanya, hii ndiyo Hifadhi Bora Afrika kwa sasa.

Tanzania tunajivunia kuwa na maeneo mengi ya Hifadhi lakini ukijaribu kuangalia yalikuwa maeneo ya wafugaji zaidi wakiwa wamasai, kwa maandiki hiyo wanastahili kuheshimiwa na kudhaminiwa. Nina Imani ingekuwa makabila mengine hakika tusingekuwa na wanyama/hifadhi hao/hizo wengine tunakula mpaka konokono.

Shida nyingine huenda wahifadhi wa mle hawana mipango mizuri ya kuendeleza mfumo ule wa matumizi Jumuishi kama sheria inavyotaka, wakae na jamii wakubaliane watafute majawabu ya changamoto kwa pamoja, lakini pia ushirikishwaji na elimu uimarishwe. Serikali itazame hili huenda na wahifadhi wanashindwa majukumu yao ikiwezekana ibadilishwe mfumo wa usimamizi wa eneo hilo.
 
Ukubwa wa Hifadhi haubadiliki lakini wamasai na mifugo yao wanaongezeka idadi, so watahitaji eneo kubwa zaidi. Utaratibu upo vipi hapo?
 
Leta matokeo ya tafiti hapa kuonyesha Ardhi ya Ngorongoro umezidiwa na idadi ya watu na mifugo (carrying capacity), tuache kuwa bias watanzania kama tunataka kutatua matatizo yetu. Mbona husemi idadi ya wanyamapori kuongezeka? Uongozi wa Hifadhi walipaswa kuona mbali kuhusu ongezoko la mifugo, ikiwemo miradi ya kuboresha mifugo wachache na wenye tija, masoko ya mifugo watafutiwe automatically hii itapunguza mifugo kwa kuwa ndiyo shughuli yao pekee ya kiuchumi. Wahifadhi wamefanya nini kuwapa jamii shughuli mbadala rafiki na uhifadhi, ajira ikoje Ili kupunguza utegemezi kwa mifugo. Kuwapa elimu ya Uhifadhi ikoje huko, wapeleke shule watakwenda maeneo mengine kufanya kazi. Narudia kusema kama Ngorongoro inakufa huenda ni kwa sababu ya management failure
 
Ukubwa wa Hifadhi haubadiliki lakini wamasai na mifugo yao wanaongezeka idadi, so watahitaji eneo kubwa zaidi. Utaratibu upo vipi hap
Idadi ya wamasai na mifugo ni hoja kwenu. Mbona hamsemi loji na hoteli za kifahari walizojaza wahifadhi ukingo wa crater na hata kwenye mapito ya wanyamapori kwa maslahi yao? Hamsemi matumizi makubwa ya maji mpaka baadhi ya Misitu imekauka kukosa maji kisa mahoteli, hamsemi kuhusu idadi kubwa ya magari yanayoingia bondeni. Narudia kusema wahifadhi watekeleze majukumu yao kuendeleza Ngorongoro inawezekana
 
Taratibu hasira za nini...nime-reply kulingana na hoja ulizotoa wewe. Hayo mahoteli na shughuli nyingine za kibinadamu zipo.
 
Wasifurushwe. Utaratibu mzuri uwekwe wa namna bora ya kuishi bila kupata usumbufu kwao na mimeo na wanyama
Utaratibu upi?.Masharti yaliyowekwa kipindi cha nyuma hayawezi tena kufanya kazi sasa nakuendelea.maana utaratibu ulishawekwa toka zamani ila binadamu ndiye anayekiuka.Swala la ongezeko la mifugo na maendeleo ya watu ni mambo ambayo yanaleta changamoto na ili uweze kunusuru hilo eneo ni lazima kimoja kitoke.sasa je tutoe wanyamapori ili wafugaji wafuge kwa uhuru kwakujiachia au wafugaji watoke wanyama waishi kwa uhuru na serikali iingize fedha za kigeni zakuleta maendeleo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Umaarifu wa Hifadhi hiyo ni kwa sababu ya mfumo wa maisha Jumuishi (Wanyamapori na Jamii). Ukiondoa jamii pale, maana yake umeiondolea sifa Hifadhi yake ya multiple Land na umaarufu. Haitakuwa tofauti na Hifadhi ya Manyara na Tarangire. Haitakuwa tena moja ya maajabu ya Dunia.

Niliwahi kuona mkataba wao na serikali ya mkoloni muingereza wakati wanapisha kuanzishwa Hifadhi ya Serengeti, hivyo kisheria ni haki yao kuwepo pale. Babu zao kukubali kuachia Serengeti ni jambo kubwa walilofanya, hii ndiyo Hifadhi Bora Afrika kwa sasa.

Tanzania tunajivunia kuwa na maeneo mengi ya Hifadhi lakini ukijaribu kuangalia yalikuwa maeneo ya wafugaji zaidi wakiwa wamasai, kwa maandiki hiyo wanastahili kuheshimiwa na kudhaminiwa. Nina Imani ingekuwa makabila mengine hakika tusingekuwa na wanyama/hifadhi hao/hizo wengine tunakula mpaka konokono.

Shida nyingine huenda wahifadhi wa mle hawana mipango mizuri ya kuendeleza mfumo ule wa matumizi Jumuishi kama sheria inavyotaka, wakae na jamii wakubaliane watafute majawabu ya changamoto kwa pamoja, lakini pia ushirikishwaji na elimu uimarishwe. Serikali itazame hili huenda na wahifadhi wanashindwa majukumu yao ikiwezekana ibadilishwe mfumo wa usimamizi wa eneo hilo.
Iwafikie wagagagigikoko
 
Back
Top Bottom