hatari ya kuibiwa kwa watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hatari ya kuibiwa kwa watoto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 21, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ZAIDI ya watoto 80 wanaendela kusota katika uwanjaw a Sabasaba walipohifadhiwa ili wazazi wao waende kuwachukua mahali hapo.
  Watoto hao ambao wamehamishwa kutoka Uwanja Wa Uhuru na kuhamishwa katika uwanja wa Sabasaba bado wazazi ama walezi hawajaonekana kuwachukua waondoke mahalai hapo.

  Chama cha Msalaba Mwekundu kinaendelea kuwalea watoto hao na kuwa na hofu kubwa ya kuibiwa kwa watoto hao.

  Hata hivyo chama hicho kimetoa masharti ya kuchukua watoto hao, endapo mtu atajitokeza kuchukua motto anatakiwa awe na alama yeyote itakayomuonyesha kuwa mtoto anayemuhitaji kuwa ni wake kiukweli.

  Wamewataka kuwa na kama kitambulisho chochote ama kadi ya kliniki ya motto, picha yeyote ama alama nyingine yeyote itakayomtambulisha kama ni mtoto wake.

  Jana zaidi ya watoto 500 waliokotwa sehemu mbalimbali za jiji wakiwa wameachwa na wazazi wao katika harakati za kuokoa uhai wao.

  Watoto haow anaoanzia umri wa miezi sita na kuendelea.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Maskini!Natumaini wote watakutanishwa na wazazi au ndugu zao!
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hapo itabidi wawe macho sana kwani wale wezi wa watoto watakuwa washaanza kuwamendea!!
   
 4. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  kuna baadhi bado ni wagonjwa hospitarini hivyo hawajatok ahospitari na kuanza kufuatilia hatma ya watoto wao. Mungu awasaidie wapone haraka ili wakaungane na familia zao
   
 5. bigcell

  bigcell JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45

  Inatia huruma sana,huenda wazazi wengine wa watoto hao wamekufa au mmoja wake ni marehemu mwingine mahututi wodini,mi naomba hao red cross wawe na moyo wa huruma wasikate tamaa waendelee na moyo huo wa huruma japo kazi ni ngumu kwao kuwatafuta wazazi wa watoto hao. Inatia uchungu sana.
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  hv wakiwaiba hawa watoto huwa wanawapeleka wapi?
   
 7. R

  Rinsa Member

  #7
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 13, 2007
  Messages: 8
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mungu asaidie wakutsne na wazazi/walezi wao soon
   
Loading...