Hatari ya gesi

THEBADDEST

JF-Expert Member
Dec 22, 2019
247
135
Kama unatumia gesi tafadhali soma ujumbe huu muhimu.

Wanandoa walirudi nyumbani usiku baada kutoka matembezi, walipofika nyumbani na kufungua mlango mwana mama alihisi
harufu ya gesi na kumwambia mume wake.

Mume alienda mpaka jikoni na kugundua ya kuwa kulikuwa na harufu kali imetapakaa
jikoni, akili ikamtuma awashe taa ili ajue chanzo ni nini, jiko lililipuka na moto
ukatapakaa nyumba nzima.

Baba alifariki papo hapo (Lala Mahala Pema peponi) majirani waliwahi kuzima moto na bahati nzuri mama anaendelea vizuri hospitalini - ICU.

Funzo kutoka kwenye kaadhia hii

1. Unaposikia harufu ya gesi tafadhali usiwashe taa, fungua milango na madirisha polepole, kwa kufanya hivi utazuia vyanzo vya cheche za moto kuweza kutokea.

2. Funga taratibu gesi yako na usiwashe taa mpaka harufu kali ya gesi itakapoisha.

3. Ukisikia harufu kali ya gesi usifungue friji kwa sababu linaweza kusababisha mlipuko wa moto. (Pia hata feni inaweza kusababisha mlipuko wa moto kwa sababu ina eletric charges )

Usisome huu ujumbe peke yako, share uwezavyo kwa ndugu, jamaa na marafiki utasaidia majanga kutoweza kutokea na Mwenyezi Mungu atakulipa kwa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuongezea tuu..
Harufu unayoisikia pindi gesi inapovuja(Inaelekea kufanan na kabbeg lililooza), ni ya kuwekawa.

Gesi yenyewe(propane, butane & isobutane), haina hata chembe ya harufu.
Kwaio ile fume(Ethyl.M) inawekwa ili ikukere na pia uihisi inapotoka ili uchukue tahadhali.
 
Kama unatumia gesi tafadhali soma ujumbe huu muhimu.

Wanandoa walirudi nyumbani usiku baada kutoka matembezi, walipofika nyumbani na kufungua mlango mwana mama alihisi
harufu ya gesi na kumwambia mume wake.

Mume alienda mpaka jikoni na kugundua ya kuwa kulikuwa na harufu kali imetapakaa
jikoni, akili ikamtuma awashe taa ili ajue chanzo ni nini, jiko lililipuka na moto
ukatapakaa nyumba nzima.

Baba alifariki papo hapo (Lala Mahala Pema peponi) majirani waliwahi kuzima moto na bahati nzuri mama anaendelea vizuri hospitalini - ICU.

Funzo kutoka kwenye kaadhia hii

1. Unaposikia harufu ya gesi tafadhali usiwashe taa, fungua milango na madirisha polepole, kwa kufanya hivi utazuia vyanzo vya cheche za moto kuweza kutokea.

2. Funga taratibu gesi yako na usiwashe taa mpaka harufu kali ya gesi itakapoisha.

3. Ukisikia harufu kali ya gesi usifungue friji kwa sababu linaweza kusababisha mlipuko wa moto. (Pia hata feni inaweza kusababisha mlipuko wa moto kwa sababu ina eletric charges )

Usisome huu ujumbe peke yako, share uwezavyo kwa ndugu, jamaa na marafiki utasaidia majanga kutoweza kutokea na Mwenyezi Mungu atakulipa kwa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Taa gani aliwasha ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom