Hatari sana vijana wenzangu

Hatari sana vijana wenzangu

Mimina wewe

Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
25
Reaction score
2
Ni kama mwezi mmoja uliopita tumemzika kijana mwenzetu kutokana na kifo cha ajabu kilichomshitua kila mtu kutokana na mazingira yake ilhali vijana wengine wawili wakiwa kwenye mateso na maumivu makali kutokana na tukio hilo lililomchukua kijana mwenzetu.

Hii imetokea mkoani Geita.

Kijana mmoja kapoteza maisha na wengine wawili wapo katika hali mbaya kutokana na kile kinachodaiwa kuwa imani za kishirikina.

Vijana hao watatu madereva pikipiki za abiria maarufu kama BODABODA walijikuta wapo katika hali mbaya kiafya hali iliyopelekea mmoja wao kupoteza maisha kutokana na maumivu makali ya kifua.

SIKU YA TUKIO.

Vijana hao wakiwa kwenye kijiwe chao ambacho hupaki pikipiki zao, ghafla alitokea mzee mmoja wa makamo akiendesha pikipiki yake akiwa amepakia abiria zaidi ya mmoja(mshikaki).

Vijana hao kwa mujibu wa taratibu walizojiwekea na kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani wakaona ni vyema kumsimamisha mzee na kutaka kujua inakuwaje amepakia abiria zaidi ya mmoja ilhali anajua anavunja sheria za usalama barabarani.

Yule mzee kwa utulivu na kwa kujua kafanya kosa akawaambia ''VIJANA NIMEWAELEWA NA NNAKUBALI KUWA NIMEFANYA KOSA, NAOMBENI MNISAMEHE ILA HII NI FAMILIA YANGU''.

Kama tujuavyo kwenye maeneo kama haya ya mikusanyiko hasa yanayowahusisha vijana waga hawakosekani watu wenye tabia za kihuni, BASI VIJANA KAMA SITA HIVI WAKAMVAMIA YULE MZEE NA KUANZA KUMPA MISUKOSUKO YA HAPA NA PALE NA MWISHO WAKAMSACHI MIFUKONI WAKACHUKUA PESA ALOKUWA NAYO.

KAULI YA KAWAIDA TOKA KWA MZEE YA CHANZO CHA TATIZO KUBWA!.

Vijana baada ya kumaliza vituko vyao kwa yule mzee wakamwacha aendelee na safari yake. Ila kabla hajaondoka mzee alitoa kauli ambayo kila aliyekuwa pale aliichukukulia kawaida ila madhara yake yalianza kuonekana baada ya muda mfupi na hapo ndipo watu walipoaanza kuyaamini maneno na kauli ya yule mzee.

MZEE WAKATI ANAONDOKA ALITAMTAMKA MANENO HAYA ''VIJANA NASHUKURU KWA HILI MLONIFANYIA ILA NAWAHAKIKISHIA WOTE MLIONIPIGA NA MTAKAOSHIRIKI KUIGAWANA HIYO HELA USIKU WA LEO UTAKUWA MBAYA KWENU NA MTANITAFUTA ILA HAMTANIPATA''.

Ukweli kila mtu aliichukulia kawaida kauli ile ila taarifa tulizozipata asubuh ya usiku alosema yule mzee zilmshtua kila mtu.

NI KWAMBA MIONGO MWA WALE VIJANA SITA, WATATU KATI YAO WALIPATA MATATIZO YA KIAFYA AMBAYO HAYAELEWEKI.

MMOJA AMBAYE ALIPOTEZA MAISHA ALIPATWA NA MAUMIVU MAKALI YA KIFUA YALIYOMSABABISHIA UMAUTI BAADA YA SIKU TATU TOKA SIKU YA TUKIO.

WAWILI WENGINE MMOJA ALIPATA MAUMIVU MAKALI YA MGUU WA KULIA NA MWINGINE ALIVIMBA TUMBO LILILOAMBATANA NA MAUMIVU MAKALI NA MPAKA LEO WAPO KWENYE MAUMIVU NA MATESO MAKALI KWA SABABU HOSPITALINI VIPIMO VINAONYESHA HAWANA MATATIZO YOYOTE KIAFYA.

MBAYA ZAIDI YULE MZEE ALIPITA KIJIWENI KWAO NA WALE VIJANA JIONI YA SIKU YA HIYO NA KUTAMKA MANENO HAYA ''VIJANA SI NILIWAAMBIA?!, MSIWE MNAWAKURUPUKIA WATU MSIOWAJUA. MIMI NAJUA PA KUWAPATA ILA NYIE HAMTANIPATA KAMWE NA HILO NI FUNZO KWENU MLIOBAKI''.
 
safi sana,msikulupuke kuchukua sheria mikononi mwenu.
 
tena wakome kabisa.
na hapo wala sio lazima uwe ni ushirikina,hata Mungu anaweza kuwaadhibu.
Safi sana Mungu/Mshirikina
 
Hiyo ni komesha kwa wale fuata mkumbo wasiokua na maana
 
Acheni uongo na hadithi zenu za Abunuwasi. Hivi mmechelewa wapi mpaka leo bado mnatuletea stori za mwaka 1952.
Mi nachukia sana mtu anayejiita kijana lakini mawazo na mitazamo yake imezama kwenye ushirikina. Nyi badala ya
kusoma au kufanya kazi kwa bidii,mnakwenda Loliondo kutafuta mafanikio. Kwa mawazo kama yenu,ndo maana wakina
Manyaunyau wanajiita madokta.P.u.m.b.a.v.u wakubwa.
 
Back
Top Bottom