Hatari: Nimenusurika kifo


Kikulacho ki-nguoni mwako.
 

Mkuu sasa ndio umewapa wabishi ndani ya bus nafasi ya kusema "NDIO MIJIZI YENYEWE, TUMEMSTUKIA KASHUKA"....Pole sana
 

Hapo ukaumia mara mbili.....1- kipigo cha wananchi wanaojiita wenye hasira kali......2- kunyimwa mzigo halafu unasikia kuwa alifuatwa na kidume mwingine tena ana gari
 
Ila outlook yako pia inakufanya uwe safe. Mfano ninavojipigiliaga napotoka nyumbani,siriazness napikua public transports, mapozi nini asee ukiniitia mwizi nahisi watu wote watakuhamaki.
 
Ni wiki sasa imepita kuna kijana wa miaka 17 kauawa huku kimara mwisho njia ya bonyokwa millenium. Huyu kijana alijiingiza kwenye ufundi wa bodaboda baada ya wazazi wake kushindwa kumlipia ada.

Siku ya idd tar 29/7/2014 marehemu aitwae lawrance alishinda nyumbani kwao tu maeneo ya mavurunza kimara, ilipofika saa kumi kuna kijana aitwae john alifika nyumbani kwa akina lawrance kwa lengo la kumuomba akamtebgenezee bodaboda. ilipofika saa moja jioni wakaanza safari kuelekea mahali bodaboda ilipo, kufika kule kijana lawrance akafanikiwa kutengeneza ile pikipiki sasa ile aijaribu akiwa amempakia john na kijana mwingine ambaye hakufahamika hatua chache mbele wakasikia mwizi mwizi, john na yule kijana mwingine wakafanikiwa kuruka na kutokomea, lawrance kwa vile alikuwa hajui chochote akabaki ameduwaa ndipo walipoanza kumshambulia

Akafanikiwa kuwachomoka akaingia kwenye nyumba moja bodaboda wakaizunguka ile nyumba kwa vitisho kuwa mwenye nyumba asipomtoa watachoma nyumba, wakaanza kuvuta mafuta toka kwa bodaboda zao, mwenye nyumba akaingia woga ikabidi lawrance atolewe wa bodaboda wakamtia mikononi kila alimshambulia anavyotaka mpaka mauti yalipomfika kila mtu akakimbia zake.

Baada ya uchunguzi ikagundulika kuwa john ndie aliyeiba bodaboda na wamemuua lawrance asiekuwa na hatia
 
Pole sana,
wakati mwingine angalieni na haya majina mnayotumia jamani KikulachoChako
kwetu wanasema jina linakufuata;
 
Last edited by a moderator:

Dah...! So sad.
 
Kwa reference zote hizi TAFAKARI KISHA CHUKUA HATUA, OKOA MAISHA KWA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI tunaposhuhudia hali hii, si kila aitiwaye mwizi ndiye.
 
Ila outlook yako pia inakufanya uwe safe. Mfano ninavojipigiliaga napotoka nyumbani,siriazness napikua public transports, mapozi nini asee ukiniitia mwizi nahisi watu wote watakuhamaki.

aaah wapi! kwa taarifa tu, wezi wa siku hizi wanavaa kama wanaenda maofisini posta mpya na maeneo mengine ya heshima
mkuu usiamini mtu kirahisi rahisi, kuna jamaa mmoja hivi ambaye sikudhani kabisa angeweza kuwa kibaka wa kutupwa,

jamaa alikuwa amevaa vizuri sana na kuonekana super smart, utadhani anaenda mkutanoni AICC, kumbe waapi ni kibaka mzoefu tu!

Basi bwana, kuna jamaa yangu alikuwa na sim mpya, miaka mitatu hivi iliyopita, ilikuwa ni nokia X2-01 enzi hizo zinatoka..

jamaa kakaa pembeni na simu yake anapata soft soft baridi huku ameweka simu pembeni na stori za hapa na pale.. huku pembeni naona jamaa halitulii, jicho lake liko kwenye simu tuu! najiluliza kimoyo moyo, vp jamani mbona hivi? au kibaka?

nikaamua tu kuichukua ile simu ya rafiki yangu nikawa nimesihikilia mkononi makusudi tu nione jamaa atafanya nini.. baadae jamaa akaondoka! kwa kweli hakuwa na kazi yoyote ya msingi eneo lile..

Baadae kuja kupeleleza, nikaambiwa huyo ni kibaka mzoefu!...

so, mavazi hayawezi kuniaminisha kwamba wewe ni msafi sana moyoni mwako!

Halafu pia kuna ule ukbaka unaokujaga kutokana na ushaiwshi tu wa ghafla wakati wewe si kbaka, hapo pia waweza iba!
 
Dah! Jamii forum baba lao. Nasoma experiences za watu najifunza mambo mengi sana. Poleni wote mliokutwa na hii mikasa.
 
Ila outlook yako pia inakufanya uwe safe. Mfano ninavojipigiliaga napotoka nyumbani,siriazness napikua public transports, mapozi nini asee ukiniitia mwizi nahisi watu wote watakuhamaki.

siku hizi hakuna kitu kamahiko, nakumbuka 1999 nikiwa kwenye kipanya kwajirani zetu wa +254, hukoo Kitale, nilivyoingia nikabahatika kukaa siti moja na jamaa mmoja ambaye kwa umri alionekana ni mdogo kwangu, lakini na mwili kunizidi na kitambi kimefutuka, kavaa vizuri suti yake ya dark blue, kanyoa vizuri amependeza ukimwangalia wala hauwezi kumtilia shaka, mimi nilikuwa kawaida tu kisafari na kijibegi changu cha mkononi nilivokaa kwenye siti nikaweka kibegi mapajani.

Tumeenda katikati ya safari nikawa nahisi kitu kinakwaruza kwenye bei upane wa huyo jamaa, akili ikafanyakazi haraka sana nikasema nisimshtue nisijekuwa namsingizia nikaumbuka mimi, nikawa kimya kama kausingizi kananipitia, akaungua zipu ya begi akaingiza mkono, alivyozamisha mkono tu nikaukamata, hakukurupuka wala kufanya purukushani yoyote, tukamshuka kwenye checkpoint tukaendelea na safari.

Katika story na abiria kumbe wanamjua ni wa eldoret na mimi jana yake tu nilikuwa Unga Limited Eldoret, nikajua atakuwa alinifuatilia akijua natembea na pesa kwenye begi kumbe sina kitu!

Wezi wa siku hizi wakomakini sana wanajitahidi kublend-in, ni ngumu kumshtukia ndiyo maana watu wasio na hatia wanauwawa!
 
Stering hauwawi ila chamoto atakipta

Lol! Ka movies za Van Damme, AWOL, sterring alikula kichapo kitakatifu, mwisho wa siku alishinda kwa kuchechemea. Kweli tujifunze kutokana na experiences za wenzetu.
 

yaani changudoa unataka tumwite shemeji?!!..tutake radhi!
pole sana lakini, siku nyingine ukichukua changu mpe maslahi mliyoelewana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…