Hatari: Mganga akutwa akiroga Mahakamani

Hatari: Mganga akutwa akiroga Mahakamani

lumumbai

Member
Joined
May 6, 2015
Posts
48
Reaction score
11
MGANGA mmoja wa kienyeji amekamatwa akifanya ushirikina katika Mahakama ya wilaya ya Bunda mkoani Mara kwa kutumia tunguli ili kuwezesha kushinda kesi.Mganga huyo ni moja kati ya waganga sita, ambao walikamatwa kwa kosa la kupiga ramli chonganishi na kufunguliwa kesi katika mahakama hiyo ya wilaya.

Mtuhumiwa huyo pamoja na wenzake hao, walikamatwa Machi 11 mwaka huu saa 6:00 mchana katika kijiji cha Kabasa wilayani hapa, wakipiga ramli chonganishi ya kuchonganisha wananchi kinyume cha sheria.Mtuhumiwa huyo aliyeshikwa juzi akifanya ushirikina huo katika mahakama hiyo ni Riku Wasaga Yahaya (50), mkazi wa kijiji cha Kabasa wilayani hapa.

Mtuhumiwa huyo pamoja na wenzake hao, walipokamatwa wakipiga ramli chonganishi, walifunguliwa kesi namba 86 ya mwaka huu katika mahakama hiyo. Mwendesha mashitaka wa Polisi, Athumani Salum, alidai kuwa juzi wakati watuhumiwa hao wakiwa mahakamani hapo, wakisubiri kesi yao kutajwa, mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Said Hamad Kasonso, mtuhumiwa Yahaya alionekana akifanya ushirikina kwa kutumia tunguli.

Ilidaiwa baada ya mtuhumiwa huyo kupekuliwa na polisi, walimkuta akiwa na vibuyu viwili vya tunguli na dawa ya ungaunga na mchanga mfukoni mwake, alivyokuwa anavitumia kufanyia ushirikina katika mahakama hiyo.

Hakimu Kasonso alisema mtuhumiwa huyo na wenzake watano, walikamatwa wakijaribu kufanya ushirikina wa kuroga mahakama hiyo, jambo ambalo ni la ajabu mno, kwani Mahakama ni chombo ambacho kazi yake ni kutoa haki na kutafsiri sheria kikamilifu na kwa kina zaidi ili haki iweze kutendeka.

Hakimu Kasonso alisema kuwa kitendo hicho cha ushirikina ndani ya chombo cha haki, kamwe hakiwezi kuvumiliwa na hivyo mahakama hiyo inawapeleka mahabusu watuhumiwa wote sita kwa muda wa siku 14 hadi Mei 22, mwaka huu, kesi yao itakapotajwa tena mahakamani hapo.

"Mahakama ni chombo cha kisheria ambacho kinatoa haki baada ya kuitafsiri sheria kwa kina zaidi na kisha kutoa maamuzi, sasa kitendo cha kuja kufanya ushirikina katika chombo ambacho kazi yake ni kutenda na kutoa haki, kamwe hakiwezi kuvumiliwa, hivyo watuhumiwa wote waende mahabusu siku 14," alisema.

Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Athuman Salum, aliwataja watuhumiwa wengine katika ile kesi yao ya awali ya kupiga ramli chonganishi kuwa ni Komoga Wasaga Msiba, Thomas Nyakojaribu, Oro Odewa Kalidoshi, Mariamu Thomas na Daud Thomas, wote ni wakazi wa kijiji cha Kabasa wilayani Bunda.

Chanzo: Habari leo
 
Ramli chonganishi inatafsirikaje kisheria? Hapo hakuna kesi tu zaidi ya uonevu!
 
yaani hapo wamewaingilia uhuru wao wa kuabudu!

Ramli chonganishi ni kama hizi;

1. Kumetokea msiba, na mganga anamtaja mtu fulani kuhusika na kifo hicho. Familia zinaparanganyika na chuki inatawala.

2. Nilisikia Mbeya, kijana amefanikiwa kimaisha kwa juhudi zake na bahati mbaya kuna vifo vilitokea maeneo hayo. Mganga akamtaja kuwa utajiri/kufanikiwa kwake kumetokana na kuua hao watu. Kilichofuata ni kuuliwa kwa kijana huyu na wananchi na mali zake kuharibiwa.

3. Kwenye migogoro ya ardhi tumesikia influence ya mauaji ikitokea kwa waganga...nk

NB: Msijifanye hamuelewi kwa kuuliza maswali ya kipuuzi km haya. Mnajua vzr mambo yalivyo...naiomba serikali wakati umefika mtunge sheria kudhibiti haya, nimeona damage kubwa kwenye jamii sbb ya waganga hawa wa ramli.

Kwa tuliokulia vijijini tunajua haya...nyie wa mjini endeleeni kujifunza & sio kubisha tu!
 
ivi kumbe mahakama imeanza kutambua ushirikina? ngoja na mimi nikamshtaki yule mtu aliyekuwa ananiloga maana ninausongo nae sana
 
Ramli chonganishi ni kama hizi;

1. Kumetokea msiba, na mganga anamtaja mtu fulani kuhusika na kifo hicho. Familia zinaparanganyika na chuki inatawala.

2. Nilisikia Mbeya, kijana amefanikiwa kimaisha kwa juhudi zake na bahati mbaya kuna vifo vilitokea maeneo hayo. Mganga akamtaja kuwa utajiri/kufanikiwa kwake kumetokana na kuua hao watu. Kilichofuata ni kuuliwa kwa kijana huyu na wananchi na mali zake kuharibiwa.

3. Kwenye migogoro ya ardhi tumesikia influence ya mauaji ikitokea kwa waganga...nk

NB: Msijifanye hamuelewi kwa kuuliza maswali ya kipuuzi km haya. Mnajua vzr mambo yalivyo...naiomba serikali wakati umefika mtunge sheria kudhibiti haya, nimeona damage kubwa kwenye jamii sbb ya waganga hawa wa ramli.

Kwa tuliokulia vijijini tunajua haya...nyie wa mjini endeleeni kujifunza & sio kubisha tu!

ewaaa, umekuja mulemule. hapo wewe unadhani mpumbavu ni nani? wewe unaweza kuamini maneno kama hayo?
serikali yenyewe haitambui uchawi, labda kama kuna marekebisho ya sheria yalinipita.
kwa hiyo waliokamatwa "wanawanga" mahakamani wanashitakiwa kwa kosa lipi?
wewe kama hauna imani na haushiriki mambo hayo mwache arukeruke wee hakufanyi lolote ancheza utamaduni tu.
 
hapo hakuna evidence ya moja kwa moja kuwa walikuwa wanawanga mahakamani na napata shida ni kifungu kipi cha sheria kimetumika kutoa hukumu dhidi yao laasivyo tuambiwe kama sheria zinatambua ushirikina
 
Mbona nyoka makengeza aliwanga bungeni lakini hakufungwa ama kuwekwa mahabusu?
 
Back
Top Bottom