Hatari inayokuja CCM toeni Dira

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,427
Wakuu,

Ninachoona kwa Taifa letu ni kuondoka kwa mgawanyiko wa mawazo, itikadi na falsafa kulingana na mtizamo wa vyama vya siasa na kuingia kwenye mgawanyiko wa mlengo wa kimaslahi!

Hii ni hatari ya kuelekea wachache wenye nguvu kuamua hatma ya nchi yetu badala ya dira na msimamo wa chama kinachotawala na mawazo mbadala ya wapinzani.

Wapinzani hawakuwa huru kufanya siasa kwa miaka isiyopungua mitano lakini hili si kisingizio cha kubeba kila ajenda na kuelekea kupoteza dira ya uongozi uliobebwa na maono ya chama. Pamoja na kubanwa lakini mlipaswa kubakia na kile mnachoamini ambacho ndio sababu ya kuanzishwa vyama vyenu.

Kugawanyika kimaslahi ambayo ni malengo ya wachache ni hatari ambayo inaweza kupelekea mataifa yasiyotutakia mema kujipenyeza na kupata nguvu kupitia wachache wetu.

Tumuache Rais wetu Mama Samia afanye kile alichoagizwa na chama chake kupitia ilani aliyoinadi kwenye uchaguzi uliopita na kushinda. Ule ndio mkataba wake na wapiga kura wake. Utafika wakati ambao yeye mwenyewe ataongoza ajenda mpya na maono mapya kuelekea kule alikokusudia. Tuache kumchanganya na kila aina ya kelele kipindi hiki anapojipanga kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu kwa nguvu zaidi.

Hivi mjadala kama wa bandari ya Bagamoyo CCM hawana dira ya nini wanataka ili wabunge wao wajue dira ya chama? Hivi CCM hawajawahi kupitia huo mkataba na kutoa msimamo wao kwa serikali? Kwanini spika aje na lake na wengine waje na maoni tofauti kama vile swala kubwa kama hili lililoasisiwa toka enzi za Mh JK ni jipya na hamjawahi kulijadili?

Hili ombwe wanaloonyesha CCM na kushindwa kuonesha njia ambayo wadau na vyama vingine wanaweza kutoa maoni yao ni tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi haraka! Otherwise maswala mazito kama haya yataamuliwa na nguvu ya kelele zenye mgongano wa kimaslahi na si dira ya chama na nchi.

Hapa tulipofikia ndio tunakumbuka maneno maarufu ya hayati baba wa Taifa kuwa CCM ikiyumba nchi itayumba! CCM tupeni dira maana ndio mnatawala then wengine tuanzie hapo ili kuzuia lobbyists kuongoza mijadala mizito kama hii.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake
 
Hii pia ni moja ya effect ya mambo ya Jiwe , kimsingi jamaa alikuwa na dira yake mwenyewe Tu kichwani anayoijua yeye peke yake ,na ameondka nayo , waliobaki hawajui lolote waende wapi , warudi wapi ,waendelee na yaliyopo au warudie ya nyuma. Wote wapo confused , Wapinzani agenda zao walishazipaki kwenye makabati may be wazirudie wakizikuta hazijaliwa panya poa.
 
Hii pia ni moja ya effect ya Jiwe , kimsingi jamaa alikuwa na dira yake mwenyewe Tu kichwani anayoijua yeye peke yake ,na ameondka nayo , waliobaki hawajui lolote waende wapi , warudi wapi ,waendelee na yaliyopo au warudie ya nyuma ... Wote wapo confused , Wapinzani agenda zao walishazipaki kwenye makabati may be wazirudie wakizikuta hazijaliwa panya poa .....
Huyo hayupo tupo sisi NOW! Matusi na sifa kwake hazibadili chochote kwetu bali tunakwendaje mbele kuanzia hapa tulipo!
 
Huyo hayupo tupo sisi NOW! Matusi na sifa kwake hazibadili chochote kwetu bali tunakwendaje mbele kuanzia hapa tulipo!
Ili uende mbele lazima ujue chimbuko la tatizo chief , na kuna vitu lazima viwekwe Sawa ndo mrudi sehemu sahihi , na hii lazima high command ifanye reformation sababu Hadi sasa tunatembelea kwenye uelekeo wa jiwe japo hatujui dira ni ipi mana kasepa nayo
 
Kati ya vitu Magu aliweza ni kudhibiti madalali wa kisiasa..
Madalali wanapanga ya Bagamoyo na miradi yote isiyo na maslah nao wanataka ipigwe chini... na uzuri madalali wanajulikana, Rais Samia anawajua, ni juu take kuwadhibit au awalee tuingie shimoni.
 
Huyo hayupo tupo sisi NOW! Matusi na sifa kwake hazibadili chochote kwetu bali tunakwendaje mbele kuanzia hapa tulipo!
Upo sahii Sana mkuu, Yani tumefika sehem kwamba Maghufuli ndo alikua bora Kati ya watanzania ml 60, genge lake halitaki kuamini kwamba KWA Sasa tupo na uongozi mpya, that's hata kipindi Cha kwanza genge Hili lilitaka awam hii iwe ya tano badala ya sita
Nasema Kama BWANA haishivyo Maghufuli sio mda jina lake tz litabaki kinadhalia Sana na kubaki katika history Kama ilivyo Uganda KWA idd Amin , wa tz wameumizwa vya kutosha na utawala wake na Bado wengi wanalia KWA machozi ya dam KWA kubaki yatima,wajane, kufilisika, familia kuyumba kisa wazazi fukuzwa KWA vyeti feki, watumishi kutopata nyongeza ya mishahara, wakulima, majibu ya hovyo mfano baki na mavi YAKO yumbani, kesi za kubambikiwa KWA wapendwa wetu, kuteka ,kuhua, kuongoza nchi kikabila,kikanda,
Aisee, Maghufuli popote ulipo pata stahili YAKO kadri ya mungu anataka to ona inafaa ,
 
Bora CCT na CCJ na CCG
CCM watoe dira haraka! Now hawana katibu mkuu, mwenezi na mwenyekiti! Wasiache hili ombwe ni hatari! Wachukue hatua waoneshe dira NOW!

Hili ombwe linaweza pia kuwa misused! Mama Samia apewe uenyekiti haraka apange safu yake mambo yaende.
 
Back
Top Bottom