HATARI: Dini inatumika na wanasiasa kama mwamvuli lakini tatizo liko hapa

HATARI: Dini inatumika na wanasiasa kama mwamvuli lakini tatizo liko hapa

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,202
Reaction score
25,377
Sikia kwa makini
Dini uliyonayo ni ujinga
Usijivunie dini
Dini ni udanganyifu
Dini ni upotofu
Dini ndio inakuzuia kufanikiwa
Dini ndio imefunga Afrika kuendelea
Dini inatumiwa na wanasiasa kama mwamvuli
Dini ni takataka kama zingine
Aliyoandika biblia ndiye aliyekuja kuipinga
Aliyeandikwa Qur'an ndiye aliyekuja kukiri ni maneno yake mwenyewe.

Dini haitakusaidia hata kidogo
Dini inakufanya kushindwa kutoka kwenye umaskini
Dini ni ukuta wa dhambi nyingi sana
Acha kurubunika kwamba dini ndio njia ya kumwona Mungu,

Mungu ni huyu hapa
Mungu ni wewe mwenyewe
Mungu ni jirani yako
Usipompenda jirani yako huna Mungu ndani yako,

Usidanganywe na dini yako ukifa utaoa wanawake wenye macho kama vikombe tambua pepo inaanzia hapa duniani, wala hakuna mahali baada ya kifo utaenda kuchukua hizo zawadi za wanawake wenye macho kama kombe.

Wala kuvaa taji isikupagawishe kuwa ukifa utanda kuvaa taji, hizo ni nadharia taji unaivaa kuanzia hapa duniani huwezi kuishi kwa shida na umskini na ukasema nitavishwa taji sio lazima uwe tajiri wa Mali na majumba utajiri wa nafsi na moto ndio utakufanya kuvaa taji hapa duniani huwezi amini Mungu ni wewe ILA ufahamu hauna ndio maana dini zinatumika kukufungu na kuamini matatizo yanakuja kama fursa ila toka gizani utambue dini ni kitamba cheusi usiamini katika dini.

"Mambo haya ni mazito sana"
 
Dini haitakusaidia hata kidogo
Dini inakufanya kushindwa kutoka kwenye umaskini
Dini ni ukuta wa dhambi nyingi sana

Na ongeza mimi:, DINI NI ZAIDI YA KONYAGI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dini haitakusaidia hata kidogo
Dini inakufanya kushindwa kutoka kwenye umaskini
Dini ni ukuta wa dhambi nyingi sana

Na ongeza mimi:, DINI NI ZAIDI YA KONYAGI.
Ukiwa na maana unalewa imani au ni ndiyo kukanyaga mafuta?
 
Unachokiamini kupata baada ya maisha ya hapa duniani ndio dini yako. Usijifanye huna dini.
 
Wewe mpaka sasa una mafanikio kiasi gani ukilinganisha na wafia dini? ili tuweze kupata uhalisia wa unachosema hapa.
 
"Usipompenda jirani yako huna Mungu ndani yako"
haya maneno yapo kwenye kitabu cha civics au???
 
TODAYS,

Dini ni mini?!?!?
Kwa lugha nyepesi kabisa tunaweza kusema mfumo wowote wa maisha tunaoamua kuuamini na kuufata. Kama mfumo wako hauamini dini hiyo pia ni dini. Imani yako ndio dini yako, hivyo dini haikwepeki.
Dini ni imani yako..... Na imani ni dini yako.........
Na Moja ya Maandiko ya Mzee Nyerere alisema " Ujamaa ni Imani" kumbe ujamaa nayo ni dini, kama vile usekula ni imani hivyo nayo ni dini. Na kama Diversity nayo ni dini.

Maana ya neno dini
kuna maana mbili ya neno dini; maana ya asili na maana ingine imekuja baada ya hizi dini kubwa kufisadiwa na kuingizwa mafunzo mapya. Mafunzo hayo mapya yamepotoa maana ya kale ya neno dini. Na athari hii imezipata dini kuu mbili yaani Ukristo na Uislam

Maana hii ya kiasili ya neno dini; ilitumika kipindi ambacho mitume ya mungu na wanafunzi wao walifata ambapo wao ndio walikuwa watawala wakuu wa mataifa.

katika Uislam ni kipindi cha mtume hadi kipindi kilichojulikana kama ni cha Ukwalifa.
Maana mpya ya neno dini ilokuja Baada ya muda kwa wanafunzi wa mitume kuanza kutia kalamu kwa vitabu vitakatifu na kutafsiri maandishi kinyume na hivyo kupotosha.

Dini ni nini
The word religion comes from the Latin word religare, which means “to bind.” It is related to the Latin word regula, which referred to a measuring stick, and is the root of our English word rule. A religion, therefore, is not merely a set of beliefs, but a set of beliefs that bind the believer. Religion imposes a kind of rule or regulation upon the believer’s life

Kwa ufupi neno Dini lina maana ya mfumo wa maisha wenye kanuni na ulioamua kuishi nao.

Maana ya pili ya neno dini ilianza baada ya dola zilizoongozwa na dini kusambaratika, na watu kuzikataa dini, mifumo inayoitwa Usekula ukaanzishwa.

Nguvu ya viongozi wa dini ikaporomoka, na viongozi wakabakiwa na kazi ya kuwaombea dua tu wenye matatizo kama maradhi nk.

Na maana ya neno dini ikawa ni mambo yanayohusiana na roho pekee.
Baada ya viongozi wa kidini kuwa chini ya tawala zenye nguvu zisizoamini mambo ya dini (Secularism) ndipo watawala hao wakaleta maana mpya ya neno dini kuwa;-
Dini ni imani inayohusiana na mambo ya kiroho kwamba kuna muumba ambaye aliuumba ulimwengu huu na kwamba ndiye mtawala wa kila kilichomo.

Kwa uoni wangu kama unaelewa neno dini sawa na ile ya asili, bila shaka utakubaliana nami kuwa dini hazina tatizo.

Bali tatizo ni mfumo wa Usekula. Usekula ndio umesambaratika.

Bali nitakuunga mkono kama neno dini kwako lina maana ile ya pili kuwa mambo yanayohusi roho pekee. Maana hii ni mbaya, potofu na haifai.

Kwa ni maana hii ya pili ndio inayotumika kuwanyonya watu.

Mzungu akikupiga Kofi shavu LA Julia MPE shavu LA kushoto.

Kugombania mafuta ya korie kwakuwa tu yamebadilishwa jina, na kwa ujinga ukaamini yatakupa utajiri. Ni ujinga na ujahiliya
 
Brother

Dini ni matendo mema. Nje na matendo mema hakuna dini.

Dini inabeba vitu vitatu (3) upendo, furaha na amani. Sasa ukiviweka hivi vitu vitatu katika matendo ndipo utaweza kusema hii ni dini.

Hitimisho

Upendo, Furaha na Amani = Imani

"Imani bila matendo imekufa"
 
Mkuu umeandika mambo mengi sana nakiufupi upo nje kabusa hata khusu dini, (mfano; NATO eti kuwa ni dini, NO)

Kabla ya ku_repply nimeangaika kufahamu kuhusu dini but sikupata maana nzuri ila nimeona kitu hapa inaweza kutoa mwongozo;

"Aina ya imani ya juu, maumbile ikiwa na kusudi kwa ulimwengu, haswa linapofikiriwa kama uundaji wa wakala au wakala wa kibinadamu, kawaida uhusisha sherehe za ibada na ibada, na mara nyingi zina kanuni za maadili zinazoongoza mwenendo wa mambo ya wanadamu."

Mohamed Abubakar,
 
TODAYS,
Only typing error imekutoa nje.....
Ok, NATO = nayo.....

Kwa ufupi imani yako yenye kanuni ndio dini yako. Na hata ukisema wewe ni mpagani, upagani utakuwa ndio dini yako.

Ukisema huna dini, huko kutokuwa na dini nako ni dini pia, kwani kuna kanuni za maisha huzifata kila kukicha.....

So what is a possibility for a man to live without religion. Answer is No way to escape religion as long as u live
 
Inakuaje kutokua na dini iwe ndio dini ya mtu husika,asie na dini ni yule ambae haamini uwepo wa mungu mfano kama huyo aloweka bandiko hapo yeye hana dini kwasababu haamini uwepo wa mungu wenye dini ni waislamu na wakristo ambao wanaamini uwepo wa mungu
 
Ni vizuri kwanza tufahamu huyo anayeitwa Mungu ni nani au Mungu ni nini?!?!?

Pili tutambue na tukubali kuwa asili ya binadamu ameumbwa ili atumikie Mungu.

Hivyo binadamu akikosa Mungu wa kweli sawa na imani yako ni lazima aangukie kwa Miungu ya uongo.

Mungu ni mini?!?!?

Mungu ni chochote unachokiamini ndio komboleo la maisha yako, Mungu ni chcht unachokiamini kuwa kina nguvu ya ziada zenye kuweza usiowezwa. Mungu ni chchte chenye nguvu isiyofikirika.

Hivyo binadamu hana uwezo wa kuzkikimbia nguvu hizo.

Wako wanaoamini nguvu hizo zipo ndani ya pesa, wengine wakiamini kwenye jua, mwezi, ng'ombe, miti, sanamu, wapo wanaowatumikia binadamu wenzi wao, nk
Vitu vyote hivyo ni Miungu. Na wanaamini bila miungu hiyo wao wasingepata baraka walizonazo.

Mwisho nini maana ya kuabudu (ibada).

Tuabudu ni kutumikia, kunyenyekea nk

Hivyo mwanadamu hawezi kuishi bila kutumikia kitu, kitu anachoamini ndicho kinachompa jeuri ya kuwa kama alivyo. Hicho kitu ndie Mungu wake.

Na njia anayotumia kukitumikia kitu hicho na kuiamini ndio dini yake.
 
Hii Elimu ya hapa na pale!!!, Uhamuzi ni kitu gani sijui?
Ukiamini Mungu yupo ni suala jema na ukiamini hayupo ni suala jema ila angalia siku ukienda uko alipo ukaambiwa yule pale..!
 
Ni vizuri kwanza tufahamu huyo anayeitwa Mungu ni nani au Mungu ni nini?!?!?

Pili tutambue na tukubali kuwa asili ya binadamu ameumbwa ili atumikie Mungu.

Hivyo binadamu akikosa Mungu wa kweli sawa na imani yako ni lazima aangukie kwa Miungu ya uongo.

Mungu ni mini?!?!?

Mungu ni chochote unachokiamini ndio komboleo la maisha yako, Mungu ni chcht unachokiamini kuwa kina nguvu ya ziada zenye kuweza usiowezwa. Mungu ni chchte chenye nguvu isiyofikirika.

Hivyo binadamu hana uwezo wa kuzkikimbia nguvu hizo.

Wako wanaoamini nguvu hizo zipo ndani ya pesa, wengine wakiamini kwenye jua, mwezi, ng'ombe, miti, sanamu, wapo wanaowatumikia binadamu wenzi wao, nk
Vitu vyote hivyo ni Miungu. Na wanaamini bila miungu hiyo wao wasingepata baraka walizonazo.

Mwisho nini maana ya kuabudu (ibada).

Tuabudu ni kutumikia, kunyenyekea nk

Hivyo mwanadamu hawezi kuishi bila kutumikia kitu, kitu anachoamini ndicho kinachompa jeuri ya kuwa kama alivyo. Hicho kitu ndie Mungu wake.

Na njia anayotumia kukitumikia kitu hicho na kuiamini ndio dini yake.
Mungu ni yule ambae hafananishwi na chochote sio katika viumbe wala vitu,ibada ni jambo lolote jema analofanya mwanadamu linalompendeza mungu mfano kusali,kutoa sadaka,kusaidia wasiojiweza na mengine yanayompendeza mungu
 
Back
Top Bottom