Msiogope hayo mambo madogo tu,hata kule Zenji mtindo ndio huo huo wa kuzuia CUF kupata matangazo na kujifaragua katika ulimwengu wa redio ,lakini wapi CUF walikuwa na redio vifua ambazo habari zikiwafikia wananchi hata haziwafikia waandishi na wanapoamua kutangaza na kuandika inakuwa ni marudio tu.
Ila tukichukua kauli ya Mh.Karume ..Mtazoea tu ndio mambo....
Hivyo msitumainie sana vyombo vya habari katika muamko huu vyombo vya habari vipewe umuhimu wa mwisho waachwe wao na hiari zao kama wataandika au watatangaza ,kazi kwao maneno kwa wapinzani ni kuongeza mikutano ya hazara kila kukicha na hii ndio dawa iliyowamaliza CCM kule Zenji ,CCM wakitumia sana redio na mihotuba mikubwa mikubwa ya viongozi wa CCM zisizo na vichwa wala miguu wenzao CUF walikuwa wakitumia ana kwa ana mtu kwa mtu na ujumbe ukifika na vikolomwezo juu ,Leo hii CCM inaogopa kuendesha uchaguzi ulio huru kila mwaka wao ni kubadili matokeo na kila wanavyojitahidi kutafuta wafuasi ndivyo wafuasi wanavyozidi kuwakimbia sasa hivi wapo tu hawajui wanamwongoza nani inasemekana wanaongoza mapolisi maana polisi wanapotumwa na watu hawa utafikiri sijui wameambiwa mtanunuliwa gari na kujengewa nyumba kila mmoja,polisi wenyewe hawasifiwi wala hawaonekani wachapa kazi kama hawajawakandamiza wafuasi wa CUF,lakini hakuna lisilo kuwa na mwisho na inaelekea mwisho wa watawala wa CCM ni mbaya maana wataanza kuumana wenyewe kwa wenyewe.