Hatari Bunge Lamhujumu Dr,.Slaa .

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
hivi sasa hotuba ya bunge na haswa ya Dr.slaa haipo live kama zilivyo nyingine ila wameamua kurudia ile ya Pinda ya asubuhi.

Dr.slaa atasoma ya kwake hivi punde.

Inatia uchungu sana someni na samabazeni hotuba ya slaa kwani ipo kwenye thread nyingine
 
TBC wanasema kuwa ni agizo wamepewa je?huyu ni nani anaweza kuwahujumu watanzania kiasi hiki?
tunakwenda wapi ,kumbukeni hata wakati wa kumtoa Zitto walifanya the same kuzuia matangazo kurushwa live...
 
hivi sasa hotuba ya bunge na haswa ya Dr.slaa haipo live kama zilivyo nyingine ila wameamua kurudia ile ya Pinda ya asubuhi.

Dr.slaa atasoma ya kwake hivi punde.

Inatia uchungu sana someni na samabazeni hotuba ya slaa kwani ipo kwenye thread nyingine

Ina maana ile tuliyo ona alikuwa hajaisoma LIVE ? Kumbe ni baada ya wao kuona imesha mwagwa hapa JF ndiyo wamekimbilia kuzima TV siyo ?Au mimi sijalewa hapa ? fafanua tafadhali .
 
Ndio kaanza kusoma hotuba na haionyeshwi wala kutolewa kwenye redio ni kuwa hakuna watanzania wanaoweza kumsikiliza kama zilivyo siku zote.
 
Chama cha mafisadi, tukiwaita hivyo wengine mnakuja juu, sasa kuna sababu gani muhimu za kutoonyesha hotuba ya Dk Slaa kama siyo kuendelea kutetea maovu yaliyofanywa na mafisadi wa chama na sirikali? Inasikitisha sana kwa kweli?
 
Wakuu msione ajabu hivi aliyoyazungumzia Dr. Slaa wanayoyafanya wako mbali? Si ndo hao hao tuliowaamini?
 
hivi sasa hotuba ya bunge na haswa ya Dr.slaa haipo live kama zilivyo nyingine ila wameamua kurudia ile ya Pinda ya asubuhi.

Dr.slaa atasoma ya kwake hivi punde.

Inatia uchungu sana someni na samabazeni hotuba ya slaa kwani ipo kwenye thread nyingine
Hiyo hotuba ipo kwenye thread gani naomba plz.
 
Watanunua hata magazeti yote lakini hawawezi kushindana na ukweli pamoja na nguvu za wakati zilizovaa matairi ya teknolojia.

Wachina wanashindwa kublock internet pamoja na ujanja wao wote (wameweza kuhack mpaka computer za serikali ya marekani) itakuwa sisi kina Ngumbaru Mwitu?

Maadam tushaipata hapa walie tu.Tena ngoja niikopi kabisa na kuituma katika email yangu.
 
wanajua tv na redio zina hadhira kubwa zaidi ya internet kwa tanzania.
ni ufisadi wa hali ya juu huu lakini hapo ndio unapokuja kuwavulia kofia ccm kwa kujua wapi wapige ili wauumize upinzani.
ingelikuwa upinzani una angalau redio yao, sasa hivi ingekuwa mambo mepesi kabisa. lakini wapi .
ccm ninawapa sifa moja (au unaweza kuiita ila ukipenda), wanajua wapi wahujumu upinzani.
 
nilipoipata otuba ya dr slaa, nilikuwa nasubiri kumsikiliza live. saa kumi na moja tbc wakawa wana piga muziki tu. nikasubiri mpaka baada ya muda, bila kutoa udhuru, wakaanza kurudia hotuba ya pinda ya asubuhi hadi sasa. kumbe kule bungeni dodoma slaa anahutubia. ni aibu kwa serikali yetu na sioni tunamlaumu nini mugabe kumbe mambo yetu ni yale yale.
macinkus
 
Kama mambo yataendelea hivi, basi kuna hatari ya wananchi(watanzania) kujichukulia sheria mkononi ili kuwaadhibu mafisadi wa ccm, familiya zao na marafiki wao.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATANZANIA WAZALENDO. TUNAKUOMBA HASIRA YAKO IWASHUKIE MAFISADI WOTE WA KILA AINA WAKUBWA NA WADOGO ILI WAO NA KIZAZI CHAO KIFUTIKE HAPA DUNIANI WAGEUKE KUWA HISTORIA.
 
ni aibu kwa serikali yetu kuzima tv na redio wakati upinzani wanatoa hotuba zao bungeni. hakuna tofauti na mugabe na sijui tuna mlaumu nini huyo mzee wakati sisi tunafanya mambo yale yale.

haishangazi kwani hata ile tv nyingine ya mwanza ambayo hutangaza bungeni live wanaendelea na vipindi vya ajabu ajabu tu.

macinkus
 
Kuna haja ya kuwahoji hawa vingunge wa hizi TV stesheni ni nani aliwapa amri ya kutoonyesha hotuba ya Dk Slaa, tulifuatilie hili mpaka tujuwe mwisho wake tusikubali kuchezewa na chama cha mafisadi katika juhudi zao za kwalinda mafisadi.
 
Hivi kweli amri kutoka serikalini bado zinaingilia utendaji wa TV?
kweli hii inatia huruma!. ni dhahiri huyu aliyetoa amri hii amekosea big tyme!. kwanza kwa kufanya hivi ni kuwadharau wananchi, ni kulidharau Bunge, ni kutumia madaraka vibaya
 
jamani naona zinafanana na ile ya TVT na Star TV, ni vyema zikaunganishwa. Ila nadhani hii ni ishara tosha ya kusoma alama za nyakati kwamba sasa CCM ama hata uongozi wa juu wa serikali sasa umeipa kisogo vita dhidi ya ufisadi na tujiandae kwa mauza uza zaidi kama vile akina Lowassa, Chenge, Mramba, Mkapa, Yona kuibuka mashujaa na kina Mzindakaya kuwa washauri wakuu wa "RAIS"
 
Hivi kweli amri kutoka serikalini bado zinaingilia utendaji wa TV?
kweli hii inatia huruma!. ni dhahiri huyu aliyetoa amri hii amekosea big tyme!. kwanza kwa kufanya hivi ni kuwadharau wananchi, ni kulidharau Bunge, ni kutumia madaraka vibaya


Na ndio maana nilishangaa niliposikia kauli ya Membe kuwa serikali ya Tanzania haiafiki matendo ya serikali ya Mugabe!! Kwangu mimi tunapozungumzia suala la "haki ya raia" matendo ya Serikali ya Tanzania na Mugabe yanaoana sawia!

Zimbabwe - raia wananyimwa haki ya kuchagua rais wamtakaye!
Tanzania - raia ananyimwa haki ya kuzungumzia uovu wa serikali ama wanaokwiba rasilimali za umma!
 
Msiogope hayo mambo madogo tu,hata kule Zenji mtindo ndio huo huo wa kuzuia CUF kupata matangazo na kujifaragua katika ulimwengu wa redio ,lakini wapi CUF walikuwa na redio vifua ambazo habari zikiwafikia wananchi hata haziwafikia waandishi na wanapoamua kutangaza na kuandika inakuwa ni marudio tu.
Ila tukichukua kauli ya Mh.Karume ..Mtazoea tu ndio mambo....
Hivyo msitumainie sana vyombo vya habari katika muamko huu vyombo vya habari vipewe umuhimu wa mwisho waachwe wao na hiari zao kama wataandika au watatangaza ,kazi kwao maneno kwa wapinzani ni kuongeza mikutano ya hazara kila kukicha na hii ndio dawa iliyowamaliza CCM kule Zenji ,CCM wakitumia sana redio na mihotuba mikubwa mikubwa ya viongozi wa CCM zisizo na vichwa wala miguu wenzao CUF walikuwa wakitumia ana kwa ana mtu kwa mtu na ujumbe ukifika na vikolomwezo juu ,Leo hii CCM inaogopa kuendesha uchaguzi ulio huru kila mwaka wao ni kubadili matokeo na kila wanavyojitahidi kutafuta wafuasi ndivyo wafuasi wanavyozidi kuwakimbia sasa hivi wapo tu hawajui wanamwongoza nani inasemekana wanaongoza mapolisi maana polisi wanapotumwa na watu hawa utafikiri sijui wameambiwa mtanunuliwa gari na kujengewa nyumba kila mmoja,polisi wenyewe hawasifiwi wala hawaonekani wachapa kazi kama hawajawakandamiza wafuasi wa CUF,lakini hakuna lisilo kuwa na mwisho na inaelekea mwisho wa watawala wa CCM ni mbaya maana wataanza kuumana wenyewe kwa wenyewe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom