Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,013
- 10,170
hivi jamani.....gari ni shs ngapi na nyumba shs ngapi.....?
Kujenga nyumba ni project ya muda wakuu, Kama sheria inasema kila mwenye gari awe na nyumba mbona hata hii project ya magufuli haitahitajika kwa jinsi jam itakavyopungua!
Na mbona kama ni kusubiri kujenga ndo uwe na gari watu watakufa bila kuenjoy raha za mwenye gari mjini hapa?
kha nyumba za kupanga sina hamu, usinikumbushe hiyo kadhia! namshukuru MUNGU nilipofika, nilishawahi kupigana na mama mwenye nyumba, kila hausgal akija mgeni anamuondosha, mwenzie nina twins ilibidi niache kazi nilee, nilipokuja kujua ni yeye anafanya mahaugal hawakai, alijua kama samaki kwao ni baharini na kamwe hutawakuta ubungo ati wamekaa, lol!
hivi jamani.....gari ni shs ngapi na nyumba shs ngapi.....?
Hapa naona kuna hoja moja tete.
Kwanza, wenye nyumba nji hii wamekuwa kama Miungu watu...kuna watu wanadhani ukishajenga nyumba, ukamweka mpangajim ni kama 'mjakazi' wako...wanasahau kuwa mtu akishalipa kodi mkataba ni kuwa yeye ana nyumba anaitumia, wewe unatumia pesa zake? itakuwaje mpangaji akimwambia mwenye nyumba pesa alizompa asinywee bia? au asihonge nyumba ndogo?
Ni utamaduni ambao haujabalansi niseme....
Inabidi tufike mahali tujue na kujiuliza itakuwaje kila mtu akajenga nyumba.....kingine wenye nyumba tunachosahau ni kuwa mtu anapanga kwa sababu mbali mbali na sio kwamba yeye hana nyumba anayomiliki! Imagine wale wanaohama kikazi kutoka mji mmoja hadi mwingine..atajenga nyumba ngapi?
Kwa hili huyo mzee ni kilaza, ana kijiba cha roho na mbumbumbu wa maisha, Kuwa na gari siku hizi imekuwa kama basic need hasa kwa maeneo ya mijini kusiko na usafiri wa uhakika wa public. sasa huwezi kunipangisha nyumba then unambie nisiwe na gari kisa tu wewe huna?
Kuna mmoja anasema ni kuwatia wivu wa maendeleo sijui nini...kama ni hivyo basi mwenye nyumba naye angenunua gari yake ili akamilishe 'maendeleo'...maendeleo ni nini kwani hasa?
Haya ndo madhara ya kupanga nyumba mahali ambapo mwenye nyumba nae anaishi hapo hapo!!
utanunuaje gari nyumba ya kupanga......?
nimekupenda bila hela shemeji.......
Hiyo hai-justify mateso ya mwenye nyumba.
Wengine tumejenga tayari, ila tumehamishwa kikazi hadi mikoani, sasa mnataka uwe tunajenga kila mahali tunakohamishiwa?
weekend hii nimetembelea jamaa zangu mitaa fulani .........amepanga na ana gari.Hiyo nyumba ina wapangaji wanne na wote wana magari y akutembelea....nyumba ina uwanja mkubwa tu wa kutosha kupaki hayo magari...kwa bahati mbaya au nzuri mwenye nyumba hana gari,bado ni mtu wa makamo na anafanya kazi...siku za hivi karibuni ameanza vituko vinavyoonekana kama ni wivu...achilia mbali kwamba huwa hataki lift za hayo magari ata kama mvua zinanyesha na amewanyima hadi wanae kuyapanda.......tabia mpya nipamoja na kudai watu walipie parking 1000 kwa siku,mara mlinzi,mara anahatarishiwa usalama wa nyumba yake,mara anakosa hewa ya kutosha kil ammoja anapewa sababu..wakat mwingine anasikika akiponda utanunuaje gari nyumba y akupanga.........huyu mzee kijana wanamheshimu sana;tunajua yupo hap aJF pia..AJIREKEBISHE au aweke madai mezani.....na wenye nyumba hapa JF mshaurini mwenzenu..........
hapo sasa da preta! btw ulibadli avatar siku za karibuni ..?!
mzima kabisa ....hofu na mashaka ni kwako wewe usiyetaka kuja Yaeda........