hataki mpangaji mwenye gari

mkonowapaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,493
767
weekend hii nimetembelea jamaa zangu mitaa fulani .........amepanga na ana gari.Hiyo nyumba ina wapangaji wanne na wote wana magari y akutembelea....nyumba ina uwanja mkubwa tu wa kutosha kupaki hayo magari...kwa bahati mbaya au nzuri mwenye nyumba hana gari,bado ni mtu wa makamo na anafanya kazi...siku za hivi karibuni ameanza vituko vinavyoonekana kama ni wivu...achilia mbali kwamba huwa hataki lift za hayo magari ata kama mvua zinanyesha na amewanyima hadi wanae kuyapanda.......tabia mpya nipamoja na kudai watu walipie parking 1000 kwa siku,mara mlinzi,mara anahatarishiwa usalama wa nyumba yake,mara anakosa hewa ya kutosha kil ammoja anapewa sababu..wakat mwingine anasikika akiponda utanunuaje gari nyumba y akupanga.........huyu mzee kijana wanamheshimu sana;tunajua yupo hap aJF pia..AJIREKEBISHE au aweke madai mezani.....na wenye nyumba hapa JF mshaurini mwenzenu..........
 
Hiyo nyumba lazima ipandishwe kodi hivi karibuni!

Kwa sababu ni mwenye nyumba na ana wataka mlipie parking mnatakiwa mkatae lasivyo mkilipa tu ata kodi ata wapandishia mtalipa bila sababu!

Lakini swala la kuweka mlinzi ni swala la muhimu na kwa usalama wa magari yenu si mbaya!

Kama mmemshindwa mnahamia airtel!

Ila mwenye nyumaba huyo ana wivu sana siku mnaweza mkakuta mataili yana pancha wala msishangae.
 
Ndg yangu kwa kuwa unaishi nyumba ya kupanga, ni vyema kuwa mvumilivu maana wapangaji karibu wote wanaoishi na wenye nyumba zao, hufanyiwa vituko vya kila aina! Ni vyema ukatafuta mahali pengine kama kero hazivumiliki lakini kama ni kusemwa tu, haya mambo madogo atachoka na isitoshe mko wa nne wenye magari nyumba moja na hivyo si tatizo lako peke yako!
By the way, gari nne nyumba moja? Mnunulieni basi hata baiskeli kumpoza hasira!!!
 
Safi sana mzee utanunuaje gari huna nyumba upangishwe nyumba na packing upewe ,nenda kajenge kwako,mzee kama uko jf watese hivyo hivyo ili hao vijana wapate akili wajenge zakwao,naona unachochea maendeleo safi sana,

hivi jamani.....gari ni shs ngapi na nyumba shs ngapi.....?
 
kha nyumba za kupanga sina hamu, usinikumbushe hiyo kadhia! namshukuru MUNGU nilipofika, nilishawahi kupigana na mama mwenye nyumba, kila hausgal akija mgeni anamuondosha, mwenzie nina twins ilibidi niache kazi nilee, nilipokuja kujua ni yeye anafanya mahaugal hawakai, alijua kama samaki kwao ni baharini na kamwe hutawakuta ubungo ati wamekaa, lol!
 
hivi jamani.....gari ni shs ngapi na nyumba shs ngapi.....?
Preta ukizungumzia gari usichukulie tu buying cost also runing cost zinaweza zikazidi buying cost ,kwa hiyo gharama yake inazidi hata kiwanja nashauri vijana wajipange sana na maisha mikopo ya magari wajenge nyumba jamani kulilea gari ni kazi from my experience
 
Last edited by a moderator:
Kuna kero nyingi zinazosababishwa na magari kupaki nyumbani. Mpangaji mwenye gari atarudi home muda wowote na kusababisha kero kwa wengine waliolala mapema. Fikiria wapangaji wanne, kila mmoja kwa muda wake na makelele yake yatakuamsha, harufu ya moshi wa gari itakukera, magari yatapita karibu na dirisha lako na kutimua vumbi. Shida yote ya nini bana? kisa mpangaji?

Kapange nyumba ya peke yako!
 
Kujenga nyumba ni project ya muda wakuu, Kama sheria inasema kila mwenye gari awe na nyumba mbona hata hii project ya magufuli haitahitajika kwa jinsi jam itakavyopungua!
Na mbona kama ni kusubiri kujenga ndo uwe na gari watu watakufa bila kuenjoy raha za mwenye gari mjini hapa?
 
Namuunga mkono kwa maisha ya bongo, ni kukosa akili uwe na gari nyumba huna, hayo mengi duuuh huyo mzee ni dalili ya kukosa. Hebu mtajeni jamani tumjue huyo mzee.

Kuna mtu nafikiri atakuwa yeye
 
Mwenye nyumba naye ana kazi, sasa akianza kuwasimanga wapangaji haoni kama ugali wake mezani unaingia hati hati?
 
khaa!kwani mmelipia hiyo nyumba milele,hameni! ila mjue kukaa nyumba moja na mmiliki ni kazi!
 
Huo ni wivu ++, inabidi ukomaa naye hivyo hivyo . Hao ni wale wale zumbukuku wanaodhani kila mwenye gari ni bonge la tajiri.
 
Gari pia ni office.
Kuna mambo hayeendi bila ya usafiri.
Na nyumba huwezi jenga angani!
 
nivea mbona huruma jamani wengine nyumba zao wamepangisha kwa gharam ya juu alafu kiasi kidogo wameenda kupanga tena na zingine wamefanyia other issues
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom