Hata wakiona mchanga watatupa kura na CCM itapeta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata wakiona mchanga watatupa kura na CCM itapeta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Feb 9, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tunaposema viongozi wengi wa CCM wamechoka kuongoza si kwamba tuna chuki binafsi hebu angalia kauli hizi za viongozi wake

  "Jamani jitahidini hata watu waone malori ya mchanga yanaenda pale ili wakituuliza wakati wa kampeni na sisi tuseme subirini ujenzi unakuja hivyo ipeni kura CCM, watatupa na tutapeta," amesema Profesa Kapuya.

  WAZIRI wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya ameonya kuwa kusuasua kwa ujenzi wa daraja la Kigamboni, Dar es Salaam ambao umeainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005 kunaweza kusababisha wakazi wa kigamboni wakinyime kura chama hicho mwaka huu.

  Amelitaka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhakikisha wanaanza ujenzi wa daraja hilo mwaka huu ili wananchi waone kuwa yale ambayo CCM imeahidi yanatekelezeka.

  "Nataka mtambue kuwa CCM katika hili tuna deni na mwaka huu ni wa uchaguzi hivyo ni mbaya kwani daraja hilo tuliliahidi kwenye Ilani ya 2005, kwa bahati mbaya hadi leo hakuna hata mchanga pale Kigamboni," amesema Profesa Kapuya wakati akizindua Bodi mpya ya Udhamini ya NSSF.

  Alisema, iwapo daraja hilo halitajengwa, CCM itahitaji maelezo ya kutosha kuwaridhisha wapiga kura ambao wamekuwa wanataka kuona ujenzi wa daraja hilo unaanza kama ilivyoahidiwa katika ilani yake.

  "Jamani jitahidini hata watu waone malori ya mchanga yanaenda pale ili wakituuliza wakati wa kampeni na sisi tuseme subirini ujenzi unakuja hivyo ipeni kura CCM, watatupa na tutapeta," amesema Profesa Kapuya.

  Alionya kuwa wasifanye hivyo kama kuwadanganya wananchi kwani Watanzania ni watu ambao wanaheshimu ahadi zinazotekelezwa na serikali yao, hivyo kitendo cha NSSF kupeleka malori kwenye ujenzi huo imaanishe kuwa wamedhamiria kulijenga daraja hilo.

  "Hatuna haja ya kuwadanganya wananchi, cha msingi tambueni tu kuwa kule kunajengwa mji wa kisasa haiwezekani waendelee kutumia usafiri wa kupelekwa huko na feri," alisema na kuitaka NSSF isaidie serikali katika suala hilo.

  Katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2005, CCM iliahidi ndani ya miaka mitano kuhimiza maandalizi na ujenzi wa Daraja la Kigamboni chini ya uongozi wa NSSF ili kuunganisha Kigamboni na Jiji la Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau, amesema ujenzi wa daraja hilo utaanza mwishoni mwa mwaka huu baada ya shirika lhilo kwa kushirikiana na wabia wengine kukamilisha taratibu zinazotakiwa katika kutekeleza miradi inayojengwa kwa ubia kupitia mpango wa public, private partnership (PPP).

  Alisema, ujenzi wa mradi huo umechelewa kuanza baada ya kuamua kuitafuta kampuni ya ushauri wa mradi huo kwa kuwa ni wa kwanza kuendeshwa chini ya mpango wa PPP.

  Kampuni hiyo ni Crisl Risk Management ya India.
   
 2. M

  Magehema JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 449
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mtaji wa CCM ni UJINGA wa mtanzania!
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Bil 72 zinatakiwa kujenga hilo daraja lenye two lane hivi change yetu ya rada ni kiasi gani hakiwezi kusaidia hapa.
   
 4. R

  Ronaldinho Member

  #4
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama kweli wajinga ndio waliwao
   
 5. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Duu,umenikumbusha mbali sana ,hivi na vile vijisenti alivyotuachiaga Bush viliyeyukiaga wapi vilee!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...