hata sisi tukishinda tutafanya hivi

nellymlay

Member
Jul 5, 2016
16
15
SERIKALI YA MUNGU MTU INA CHAKUJIFUNZA HAPA"

Aliyekuwa mfungwa wa kisiasa nchini Gambia Ndg.Amadou Sanneh, mwenye umri wa miaka 72 ameteuliwa wa wa Waziri wa fedha, ikiwa ni siku 3 tu baada ya kuachiliwa huru na Rais Adama Barrow.

Amadou aliwekwa gerezani na Rais Yahya Jammeh kutokana na kushiriki maandamano ya kupinga utawala wake mwaka 2013. Tangu mwaka 1994 Rais Jameh aliposhika madaraka, Amadou amekuwa mfungwa maarufu wa kisiasa kwa kukamatwa, kuwekwa jela, na kuachiwa.

Amadou na viongozi wenzake watano wa chama cha UDC walikamatwa mara ya mwisho mwaka 2013 ambapo walitupwa gerezani kwa amri ya Rais Jameh na kuamuru kutumikia kifungo cha maisha. Licha ya mashirika ya kutetea haki za binadamu kama Amnesty International kutaka waachiwe, lakini Rais Jameh aliendelea kushikilia msimamo wake wa kutowaachia.

Amadou ni msomi wa masuala ya fedha mwenye shahada ya Uhasibu na Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa biashara (MBA). Ameshika nafasi mbalimbali za kisiasa ikiwemo kuwa mweka hazina wa chama cha upinzani cha UDP kabla ya kuswekwa gerezani mwaka 2013.

Amadou aliachiwa huru jumatatu January 30 mwaka huu, na siku 3 baadae ameteuliwa kuwa Waziri wa fedha wa nchi hiyo. Shirika la habari la ABC limeripoti habari ya kuachiwa Amadou na kuteuliwa kuwa Waziri kama mafanikio makubwa ya demokrasia kupitia taarifa yenye kichwa "From Jail to Cabinet Minister; Gambia's New Government Forms"
 
Back
Top Bottom