Hata na Mimi Sijala! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata na Mimi Sijala!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by X-PASTER, Sep 30, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hata na mimi sijala

  Ndio, 'hata na mimi sijala, mwananchi' ni maneno yanayotamkwa na Permanent Secretary katika shairi la 'Building the Nation" lililoandikwa na Henry Barlow wa Uganda. Kwa ujumla shairi hili linatupa hadithi ya dereva wa Permanent Secretary (PS) ambaye anatueleza yeye mwenyewe kwamba leo alitekeleza wajibu wake katika kujenga taifa nao ni kumpeleka P.S. kwenye "hafla muhimu."

  Dereva huyu anatueleza juu ya hili kwamba hafla hii kwa kweli ilikuwa ni chakula cha mchana ambacho kilikuwa na kila kitu:- bia, kuku wa kuchoma, mvinyo, ice-cream, kahawa kiasi cha haja. Baada ya mlo huu dereva anamrudisha P.S. ambaye anapiga miayo mingi sana. Sasa ili kujizuia asilale anamuulize dereva wake. Je,umekula rafiki yangu?

  Dereva anamjibu, huku akitabasamu kwa siri, kwamba hajala. Baada ya jibu hili P.S. naye anasema kwamba naye hajala na kwamba alikuwa 'busy' kushughulikia masuala nyeti ya taifa. Kutokana na hali hii ya "kushinda na njaa", P.S. anasema kuwa inamsababishia vidonda vya tumbo . Na kwamba haya ndiyo matatizo ayapatayo katika kujenga taifa.

  Dereva anashangaa na mshangao huu unamuingiza kwenye mawazo, ambapo anaeleza kwamba vidonda vyake (dereva) vya tumbo vinauma pia lakini tofauti ni kwamba vimesabishwa na njaa na si vyakula visivyo na idadi. Shairi linamalizia na kurejea nyumbani kwa wajenzi wawili wa taifa jioni ile wote wakiwa na maumivu makali ya tumbo. Matokeo ya kujenga taifa kila mtu kwa njia yake tofauti.

  Wako viongozi na watendaji wa serikali ambao wana tabia kama za P.S, kutumia mali ya umma kwa maslahi yao binafsi huku wakijitangazia kuwa wanajenga taifa. Wale ambao wanatekeleza wajibu wao hawaonekani na wengine hunyanyaswa kama huyu dereva, hawapewi chakula bali hukejeliwa kwa masuali kama hili lililoulizwa na P.S.

  Unafiki kama huu wa P.S. unaonekana wazi ambapo viongozi wa vyama na serikali hususan wakati huu wa kampeni, ambapo huja na sura ya kuonyesha kwamba wana matatizo kama yetu wananchi wataonekana kama wanajali shida za wananchi na kwamba na wao wanateseka na wengine tunawasikia eti wanamwaga mapesa na misaada katika shida "kujali" shida za wananchi. Lakini watu wanaweza kujiuliza kwamba hivi hali hii haifanani na ile ya P.S. ya kumuuliza dereva wake iwapo amekula, si kama anamjali bali akinyamaza atasinzia. Labda pia hawa wanaotoa misaada sasa wanaogopa 'kusinzia'wasije wakakosa kura. Kama ilivyo kwa PS, watu hawa watakapokuwa wanafaidi matunda ya "jasho lao" hawataongea wala kusikika wakitoa misaada. Kama P.S. wataongea watakapomaliza.

  Wakati tunahudhuria mikutano ya kampeni tuwe macho kuna watu watakaotuambia "hata na mimi sijala" ili tuwaone kwamba ni wenzetu kumbe meza wanayotoka imechafuka. Watu hawa wana maradhi mabaya yanayotokana kula mno, maradhi yetu yanatokana na kukosa chakula. Tuwajue watu hawa na unafiki wao kama dereva alivyomjua P.S. na uongo wake.
   
 2. m

  magee Senior Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  NO WONDER MKULU ANAANGUKA MAJUKWAANI NIMATOKEO YA KUVIMBIWA MAUTAMU.........nimejifunza kitu kimoja ukila saana,unaanza kujishtukia shtukia sijui watashituka,sijui likibumbuluka itakuaje......sijui hivi sijui vile,mwisho shinikizo la damu,mwisho magonjwa ya moyo mara kuanguka kusiko elezeka.NASEMA ACHA WALE IKO SIKU INAKUJA TUTAWATAPISHA!!!
  i love purple.......king's color!!
   
 3. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ukishiba sana utaharibu hali ya hewa, no haiwezekani viongozi wetu wameshiba sana na hata kuanguka kwao ni kutokana na kuvimbewa.
   
 4. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  UMENIKUMBUSHA MBALI SANA MKUU,
  Nadhani ni vema tukawa tunafikiri haya, Kweli fasihi inafikisha ujumbe...
   
Loading...