Hata mimi ni mnyonge, ila sioni wa kunitetea


CHA The GREAT

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Messages
606
Likes
770
Points
180
CHA The GREAT

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined Nov 11, 2010
606 770 180
Utawasikia wakijinasibu kwa kusema wao ni watetezi wa wanyonge, lakini kwa yale yanayofanya niwe mnyonge wameyafumbia macho na kujifnya hawayaoni; They are turning a blind eye to what makes me be mnyonge.

Wote mashahidi, tumekuwa tukishuhudia sarakasi za mafao kwenye hii mifuko ya jamii. Wakati serikali ikisema fao hilo halipo na badala yake kutakuja fao la kukosa ajira, bado ipo mifuko inatoa fao hilo ila mingine haitoi fao hilo. Inasikitisha sana na kujenga hasira mioyoni mwa wale ambao wananyimwa mafao yao.

Mifuko hii yote ipo chini ya ssra, hii ni mamlaka inayosimamia na kudhibiti mifuko ya hifadhi ya jamii lakini mambo ya ajabu ni kwamba kila mfuko unajiendesha kivyake. PPF wanazuia mafao hayo mbaya zaidi wanatoa kwa ubaguzi, ila LAPF wanatoa fao hilo. Tumwamini nani, tusimwamini nani tena.

Vyama vya wafanyakazi vimekula ganzi, wabunge wamekula ganzi, vyombo vya habari ndiyo kama vipo likizo juu ya hili, yaani ni tabu tupu.

Hivi wanapozuia pesa za watu ilihali watu hao hawajajenga nyumba, wanadhani kodi za nyumba zinapatikanaje? Hivi wanapozuia pesa zetu ilihali wanajua hatukopesheki kwa jili ya kufanya biashara au kujiajiri, wanadhani tutaendeshaje maisha?

Naumia sana! Ee Mungu saidia juu ya hili, sijui nikiugua nitaendaje hospitali wakati sina hela. Sijui wanaonisaidia kulipa kodi ya chumba wakichoka nitaishi wapi?

Ee Mungu saidia, maana hawa wanaojiita watetezi hapa duniani ni wanafiki, wanakula vyakula vizuri, wanalala sehemu nzuri, akaunti zao za benki zimenona, wanasafiri kwa kutumia si tu magari bali magari ya kifahari, wanavaa vizuri wana nyumba sawa kabisa na za wafalme, lakini wanashindwa kunitetea mimi mnyonge. Naumia sana na mafao yangu kuzuiliwa na hawa PPF wakati ni haki yangu. Nimeamka alfajiri saa kumi ili kujiandaa kwenda kazini kutokana na adha ya usafiri, kuna wakati nimenyeshewa mvua, kuna wakati sili vizuri kwa sababu pesa yangu isingetosha kutokana na kukatwa kodi na nyingine kwenda mifuko ya jamii, lakini leo hii naumizwa kwa akiba yangu ya haki kuzuiliwa.

Sina la kusema, mengine nakuachia wewe Mungu, maana mateso, shida, karaha na kila aina ya taabu unaifahamu wewe Baba, amina.
 
B

Babati

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Messages
31,779
Likes
25,180
Points
280
Age
33
B

Babati

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2014
31,779 25,180 280
Hawa ni watetezi wa CCM wala hawana lolote.
 

Forum statistics

Threads 1,235,139
Members 474,353
Posts 29,213,143