Hata mawaziri hawaamini Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata mawaziri hawaamini Polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by armanisankara, Jul 29, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  JE, umewahi kujiuliza Jeshi la Polisi haliaminiki kiasi gani na kwa nini?

  Je, unajua kwamba hata mawaziri wa serikali hii ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hawana imani na Jeshi la Polisi?Hebu tutazame pamoja kauli za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe tangu akiwa mbunge tu wa Kyela hadi baada ya kuteuliwa kuwa naibu waziri wa ujenzi.

  Tangu Februari 2008, alipowasilisha bungeni ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza kampuni ya Richmond kupewa zabuni ya kufua umeme wa dharura, Dk. Mwakyembe pamoja na wabunge waliojitokeza kuwa wapambanaji wa ufisadi, walitoa taarifa kwamba wanatishiwa maisha yao.

  Mpaka leo, pamoja na Jeshi la Polisi kupewa namba za simu zilizotumika kutishia uhai, tuhuma hazikufanyiwa kazi, hivyo hakuna aliyenaswa.Mei, 2009 Dk. Mwakyembe alipopata ajali baada ya gari lake kupinduka eneo la Ihemi mkoani Iringa, polisi walichunguza tukio lile na kutoa ripoti ya ajali ile katika kipindi kifupi.

  Dk. Mwakyembe kwanza aliipinga ripoti ile ya polisi na pili akawashangaa kuvunja rekodi kwa kutumia muda mfupi sana kukamilisha kazi ya uchunguzi wa ajali ile. Hakika ripoti ile ilifutwa na haikutolewa nyingine.

  Mapema mwaka jana Dk. Mwakyembe alitoa tuhuma nzito dhidi ya watu, aliodai walikuwa wakiifuata roho yake wakifadhiliwa na mfanyabiashara mmoja. Pamoja na tuhuma hizo kuandikwa sana katika vyombo vya habari, polisi hawakuonyesha weledi wa intelejensia na uwezo wa kufuatilia na kuchunguza.Baadaye Dk. Mwakyembe aliteuliwa kuwa naibu waziri wa ujenzi na aliendelea kuwaambia Watanzania kuwa hana imani na Jeshi la Polisi katika kufanya uchunguzi.

  Mfano, alipougua ugonjwa wa "ajabu" na kupelekwa India kwa matibabu, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ndiye alipita kila mahali akidai anachougua Dk. Mwakyembe kina uhusiano mkubwa na kulishwa sumu.

  Ingawa tuhuma hizo nzito zingelitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi haraka na kuwanasa wahalifu, lilikaa kimya. Baada ya kushutumiwa kwa ukimya huo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha (sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), akaibuka na kusema polisi "wanachunguza" suala hilo.

  Siku iliyofuata Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, akajitokeza na kusema kwamba kadri anavyojua, na kwa mujibu wa taarifa walizopata kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mwakyembe hajalishwa sumu.

  DCI Manumba aliwaaminisha wananchi kwa ujumla kwamba wamefanya uchunguzi na kujiridhisha kwamba naibu waziri huyo hakuwa amewekewa sumu yoyote isipokuwa alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kawaida.

  Lakini aliyekuwa Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda, akajiweka kando na taarifa ya DCI Manumba akisema haijui na wala hajui mkurugenzi huyo alikopata ripoti hiyo.

  Maelezo haya ya Dk. Mponda yalikuwa yanathibitisha kwamba Jeshi la Polisi limepika ripoti. Dk. Mponda akawataka wote wanaofutilia suala hilo, wamuulize DCI Manumba alikopata taarifa hizo!Utata; Waziri Shamsi anasema polisi wanachunguza, DCI Manumba anasema wamepata ripoti ya ugonjwa wa Dk. Mwakyembe kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, lakini waziri mhusika anasema hana ripoti hiyo.

  Tujiulize, Jeshi la Polisi liliongopa? Kama liliongopa katika suala linalohusu afya ya naibu waziri, litaaminika vipi katika matukio yanayohusu raia wengine likiwemo la kutekwa na kuteswa karibu ya kufa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka?
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 3. tonnyalmeida

  tonnyalmeida JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  serikali imepoteza uaminifu machoni pa Raia wake inahitaji kujisahihisha.
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mi binafsi siwaamini police hata chembe!

  Siyo kwa mawaziri tu!

  IMANI imetoweka kwangu kwao kbs tangu mwaka 2005!!
   
 5. hengo

  hengo JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  critical investigation is not an overnight process
   
 6. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,282
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Hao mawaziri hawafuati sheria za usalama barabarani,. Je huwajahi ona magari ya mawaziri yakiover speed sehemu zilizowekwa speed limits?

  Jiheshimu uheshimiwe.
   
Loading...